Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Nilisoma kisa cha dada mmoja anaitwa Jane, kilichapishwa gazetini wiki mbili zilizopita. Jane ni mchanganyiko wa damu nyeupe na nyeusi. Baba yake ni Mzulu na mama ni mzaliwa wa Uingereza.
Mama yake Jane alikutana na raia wa Afrika Kusini miaka ya mwisho wa 60 na mwanzoni mwa 70. Huyu Muafrika ya Kusini alikua Kaburu aliyekwenda kusoma Uingereza. Baada ya masomo alirudi kwao Afrika Kusini akiwa na mke wake mpya.
Mama Jane alipata shida sana kuzoea maisha ya Afrika Kusini na mume wake akiwa mtaalamu alitumia muda mwingi kazini. Yule mama alijikuta katika penzi zito la Mzulu aliyekuwa mpishi katika hoteli ya nyota tano.
Mama Jane alipata ujauzito, aliomba Mungu uwe wa mume wake. Siku zilitimia na mtoto wa kike alizaliwa na kupewa jina la Angela. Mtoto akiwa mdogo hakuweza kutambulika kama alichanganya damu ya jamii mbili. Nyumbani ndugu na marafiki walimwaga zawadi na sherehe ya kumkaribisha mtoto ilifanyika.
Wiki mbili baada ya kujifungua mama Jane akiwa anamuogesha mtoto, aliona masikio yanaanza kubadilika rangi, pale aliona kabisa na pua pana ya Kizulu. Mama alipata hofu kubwa sana. Fikiria Afrika Kusini yeye ni mgeni na hana familia.
Mama alipiga simu kwa daktari wa watoto na kuweka miadi. Alihakikisha miadi ile inaendana na muda wa mume wake ili wawe pamoja. Walipofika kwa daktari, mama alisema Nina kitu cha kuweka wazi, huyu mtoto sio wa mume wangu. Alifanya vile akijua mbele ya daktari maisha yake yatakua salama.
Mume alipata mshtuko lakini daktari alisema taharuki tuiache nyuma, kipaumbele hapa ni uhai wa mtoto. Wote walikubaliana kumpeleka mtoto Uingereza kwa kuasiliwa. Daktari alifanya mipango yote na wazazi waliwaambia ndugu na marafiki kuwa mtoto amepata rufaa Uingereza kutokana na matatizo ya moyo.
Kule Uingereza walimkabidhi mtoto kwa wakala wa uasili. Walipumzika kwa wiki mbili wakitafakari ndoa Yao. Walirudi Afrika Kusini na kuwataarifu ndugu na marafiki juu ya kifo cha Angela akiwa hospitali huko Uingereza. Waliomboleza kifo cha Angela na kumaliza msiba.
Wazazi wapya waliishi kijijini, walisafiri mpaka London ilikokua ofisi ya wakala na kukabidhiwa mtoto. Walifanya sherehe ya ubatizo na kumpa mtoto jina la Jane. Jane alimkuta kaka yake aliyekua na umri wa miaka miwili kumzidi yeye. Wote wawili waliasiliwa ila kaka yake Jane alikua Mzungu.
Jane na kaka yake walilelewa kwa mapenzi makubwa sana. Matatizo yalianza katika umri wa balehe Jane akiwa shule ya upili, pale Kijijini hakukuwa na mtoto mweusi au aliyechanganya rangi. Jane alijiona yuko tofauti na wenzake na kujihisi mnyonge.
Jane alijikata mikono na kutokwa na damu, alipata msongo wa mawazo. Akiwa na umri wa miaka 14 akiwa anapekua chumbani kwa wazazi wake aliona bahasha na ndani ya bahasha kulikua na rating ya chakula na maelezo ya kumuaga. Mama yake alimuambia anamtoa alelewe na watu wengine lakini hii yote nikwasababu anampenda sana.
Jane aliandika barua kwa mama yake mzazi, mama alijibu barua kwa maneno mafupi sana, Jane aliandika barua ya pili na kumtaka mama yake waonane, mama alimtaarifu kuwa ule uwe mwisho wa mawasiliano yao. Maumivu ya Jane yalizidi.
Jane aliamua kumalizia maumivu yake katika masomo. Alihitimu shahada yake vizuri na kupata kazi Dubai. Tatizo lake liliendelea kumkabili na akiwa Dubai alikua mlevi mbwa. Alipoteza kazi kutokana na ulevi uliokithiri.
Aliamua kutafuta kituo cha kutibu tatizo lake la uraibu wa pombe. Aliona nyumba nzuri Afrika ya Kusini na alijiandikisha na kuanza tiba. Akiwa Afrika Kusini alifanikiwa kukutana na kaka yake wa baba mmoja kupitia tweet.
Ilimchukua mwaka mmoja tangu kufahamiana na kaka yake mpaka kumuona baba yake. Familia ya Kizulu ilimpokea kwa furaha kubwa na Jane ameamua kuhamia huko kabisa, ameanza miradi inayompa pesa na anafuraha kubwa kuwa na familia inayomuelewa na kumpenda.
Hizi DNA ni rahisi kumwagika lakini zina madhara makubwa sana mipango ikikosekana.