Mtoto kushinda akitazama Televisheni siku nzima ni sahihi?

Mtoto kushinda akitazama Televisheni siku nzima ni sahihi?

Inatakiwa mtoto atazame program maalum kwaajiri yake. Ila shida ya siku hizi stations hazina usimamizi mzuri kama miaka yetu.

Back in the 1990's vipindi vilikuwa vya maadili na vya kufunza tamaduni za kitanzania na kiafrika. Ila kwasasa umagharibi mwingi sana watoto wanaona viroja na kujifunza mambo ambayo yanawashape vibaya sana kimakuzi.

Stations za sasa muda mwingi ni nyimbo za naijeria na za wasafi classic. Nyimbo zenyewe ni mapenzi 99%. Mameneja vipindi wamelala hawahangaiki kutafuta vipaji na project za kuonyesha ambazo zitakuwa na mlengo mzuri kwa watoto.

Media ndio namba one programing tool kwa sasa karne hii ya 21. Tusipokuwa makini 100 years from now tutafuta kila zuri la jamii hii na mabaya yatakuwa ni kawaida sana.

Kwa mfano kwa sasa tunashangaa why watoto wadogo wanaanza jihusisha na ngono yaani unakuta binti 14 years hana bikra , dogo wa miaka 12 tayari amesha chomeka mjusi wake ukeni kwa mwanamke tena mkubwa kwake. Haya ni matokeo ya media exposure na umakini mdogo sana wa hao programers huko mitambonii vipindi vinaporushwa hewani.

Watoto wapo exposed kwenye vipindi vyenye influence ya ngono nyuma ya pazia kama Pillow talk, sijui ala za roho, tamthiria za wanaojiita Bongo movie, miziki ambayo inahamasisha ngono yote katika kivuli cha Vipindi vya mapenzi.

Hakuna program za kujenga akili positive bali program za kupumbaza vijana wasiwe na makuzi ya ujenzi wa taifa bali kulidhoofisha na kuharibu ustawi wa jamii kwa mapana yote.

Hawa viongozi wenyewe tunaowaweka katika nyanja za uongozi huwa tunapofanya uchaguzi huwa tunawachagua kwa utaratibu wa kupuuza mabaya kumi na kuchukua zuri moja tunasahau kuwa uongozi ni dhamana ya wananchi wanaotaka mabadiliko chanya na kuweka msingi wa mfano wa kuigwa.

Leo ukimuona binti kama Jokate, kila mtu anasifia kuwa amejenga shule ya darasa tatu kisarawe kama mkuu wa wilaya ila tunasahau alipopanda pale jukwaa sijui la fiesta na kutwerk,au Namna ya mahusiano kuruka na watu maarufu kadhaa kwa kuwabadili moja na kuweka mwingine. Leo ukimsema huyu kandidate utaambiwa una chuki binafsi,unawivu sijui una nini ili mradi tu watu wakuzime,yote hii ni matokeo ya programs za media na kupungua kwa usimamizi wa maadili katika jamii tunaona ni sawa tuambo kwenda vile yanaenda sawa.

Sisemi kuwa watu hatukosei ila nasema hebu tujaribu kutafuta watu walioishi kwa maadili ya juu na wanaotoka familia za maadili mfano wa kuigwa ili wawe viongozi na sio kila anaeongea sana basi anapewa shavu. Uongozi ni standards na sio matamanio ya mtu kuwa pahala fulani.

So yote kwa yote kwasasa naona tumeshafika pabaya kuhusu tv na program zake. Kama hautazami watoto wako wanatakazama nini na kujifunza nini usishangae kuona mienendo yao ikibadilika.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mtoto anahitaji usimamizi hasa kwenye masuala haya ya TV na vifaa vinavyohusiana na kuonesha vidio kama kompyuta,simu nk.

Kwanini inatakiwa asimamiwe ni kutokana na maudhui yanayorushwa kwenye tv na chaneli husika, kuna baadhi ya maudhui hayafai kwa watoto wadogo yatamuathili kwa namna moja ama nyingine,kitabia na kiakili. Mfano; =>Maudhui ya ngono,
=>Matumizi ya vilevi na madawa ya kulevya,
=> Wizi na ugaidi(matukio ya mauwaji (unyama)),
Na kuna matukio mengine hata mtu mzima hayamfai kutokana na haiba yake, kama mapigano au mauaji ya kikatili, ajari mbaya.


Ushauri:
Ingekua kipindi cha nyuma 2005 kurudi miaka ya nyuma ningekushauri umuache tu aangalie hadi hamu ya TV imuishe (Ni hali tu ambayo angeizoea/adapt ndani ya miezi mitatu tu baada ya hapo ataona hakuna jipya, utizamaji wake utakua wa kawaida tu.

Ila kwakua kipindi hiki dunia ipo kasi sana, Midia zipo after money hazikujali wewe muangaliaji, na siku hizi kuna hizi tamthilia zimetengenezwa kwa ustadi mkubwa kanakwamba hata mtu mzima ukikaa vibaya zinakuteka na kukuendesha na ni ndefu zipo aina mbalimbali na haziwezi kuisha leo wala kesho ni saivi tuko hapa jukwaani kuna wasaniii wanaandaa kazi zao, sasa fikiria kwa mtoto ambaye ni mwanafunzi masomo sindio bye bye 👋,"mshika mawili moja humpokonyoka"

Pia tofauti iliyopo katika maudhui yanayohusu mapenzi hasa musiki ni ndogo sana ukilinganisha na ngono yenyewe halisi.

Sasa kwa hali hii nakushauri mtoto usimuachie TV aangalie pekeake na kwamuda wote huo.

Note : Watoto hawana akili au uwezo wakujitambua hivyo wanahitaji usimamizi wa hali ya juu kuanzia nyumbani hadi kwa makundi yawatoto wenzie anaoshinda nao (mtoto wako unaweza mmudu nyumbani safi kabisa kumbe anakoshindaga kunamitoto haina hayo makuzi na hakuna yasicho kijua kuanzia sigara bangi wizi hadi uku 18+).

Watoto wote wenye tabia mbaya, hata waliokua tayari ila wana tabia mbaya ambazo hazivumiliki, mtu wa kwanza kulaumiwa ni mlezi wake hao wengine watafuatia baadae.
 
Sio sahihi, Atengewe muda maalumu tena kwa uangalizi wako.
 
Wanaume wote wangekuwa baba Bora km wewe hakika jamii zetu zingefaidika sio siri hata nimetamani tungekuwa ndugu
Jamii bora inaanzia ngazi ya familia, sasa wengi wetu jukumu la malezi hatujalipa kipaumbele badala yake kila mzazi anahangaika kutafuta pesa huku na huko ili mtoto aende shule bora.

Trust me mtoto aliepewa malezi sahihi hata kama hakupata fursa ya kusoma shule bora huwezi mlinganisha kiufanisi na mtoto aliesoma shule bora ila malezi mabovu.
 
Tv binafsi siifagilii kwa MTT wala tablet Wala Simu.mpatie vitabu hard copy hata za picha vya kutosha.
Nasoma msome kitabu Fulani ivi mpaka kimenifanya nisiweke tv home Bali big library is my dream.
Yaani mavitabu na Yale madude ya practical za sayansi.
Afanye practical za light,sumaku,umeme, mechanics, pia na table tennis awe anacheza
 
Msimuondoe junior kwenye TV atalia
Watoto wakishua hao hata kama kuna mechi ukaangalie banda umiza ili junior asilie.
 
Mzazi/mlezi mzuri ni yule anayempangia mtoto ratiba.
Usafi kwanza na mengine ya muhimu.
Muda free, ndio wa kuangalia TV.
Muda mwingine unan'goa cable.
 
Aende shule na kurudi kwa school bus, akirud nyumban afuliwe hadi socks na beki 3, wakati huo yeye akiangalia TV, jioni awe anapikiwa chips kuku kwakua hapendelei kula wali maharage, hakikisha unamfungia ndani ya geti asizoeane na wenzake, mwezi ukatike ikiwa hajawahi kutembea hata klm 4 kwa mguu, hakikisha dogo akiwa na miaka 9 awe tayari na kitambi

Alafu baada ya hapo akishakua tuachie walimwengu tumfunze
 
Back
Top Bottom