Mwana Mtoka Pabaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 15,118
- 16,485
Mimi nitakushauri kwanza uzingatie ushauri uliopewa kuhusu lishe na diapers. Yawezekana muda huo mtoto anakuwa amekojoa mara kadhaa kiasi diaper imelowa. Muache alale bila nguo, cha muhimu mfunike. Kuhusu maziwa ya mama yake, yawezekana ni mengi lakini ni mepesi. Mama abadili diet, asile haya mambo ya kina Shilole na Diamond
JUU YA YOTE, mshirikishe Mungu. Ulimwengu tunaoishi umejaa mauza uza na kero. Yawezekana mna mambo yenu ya mila au mijitu mizima isiyo na haya inamchokonoa mtoto usiku asilale. Fanyeni maombi nyumbani na umtolee mtoto sadaka. Kama kuna maagano yalifanywa huko zamani basi yabatilishe kwa kumtolea mtoto sadaka.
Na kama umemfunga mtoto ule uchafu mnawafunga watoto kiunoni au mkononi, fungua...usimweke mtoto mipepo michafu.