Mtoto mchanga kulia sana usiku wa manane

Mtoto mchanga kulia sana usiku wa manane

Mimi nitakushauri kwanza uzingatie ushauri uliopewa kuhusu lishe na diapers. Yawezekana muda huo mtoto anakuwa amekojoa mara kadhaa kiasi diaper imelowa. Muache alale bila nguo, cha muhimu mfunike. Kuhusu maziwa ya mama yake, yawezekana ni mengi lakini ni mepesi. Mama abadili diet, asile haya mambo ya kina Shilole na Diamond

JUU YA YOTE, mshirikishe Mungu. Ulimwengu tunaoishi umejaa mauza uza na kero. Yawezekana mna mambo yenu ya mila au mijitu mizima isiyo na haya inamchokonoa mtoto usiku asilale. Fanyeni maombi nyumbani na umtolee mtoto sadaka. Kama kuna maagano yalifanywa huko zamani basi yabatilishe kwa kumtolea mtoto sadaka.

Na kama umemfunga mtoto ule uchafu mnawafunga watoto kiunoni au mkononi, fungua...usimweke mtoto mipepo michafu.
 
Kaka pole sana....hii suala iliwahi kunitokea kwa mtoto wangu...yeye alikuwa Amalia kuanzia saa 4/5 usiku-10 alfajiri.
Mama watoto alibembeleza akachoka akawa analia na yeye...nikabembeleza sana kama kawaida wapi, majirani wawili wakasaidia wakachoka. Wakaanza Mpe jina lingine nk..
Nikazama google, nkagundua mie si wa kwanza kukutana na hilo tatizo, wataalamu wao wana formula yao kabisa wanaiita 3*3*3. Yaani wanasema katika kipindi Fulani cha ukuaji wa mtoto kuanzia wiki ya 3 na kuendelea mtoto anaweza akawa analia kama kichaa kwa Masaa yasiyopungua 3 kwa siku 3 ndani ya wiki moja kuendelea kwa majuma yasiyopungua 3.

Wanatoa na mbinu pia za kusaidia kupunguza kadhia hiyo ikiwa ni pamoja na kutumia pacifier, kuhakikisha mtoto anapolala analala kwa wakati na ikiwezekana mlaze kifuani pako..kaache katoto kakukumbatie...pia make sure kama ananyonya anyonye na ashibe ndi...make wengine wanashiba na bado wanalia sana! Ratiba yake ya kulala izingatiwe ukicheza nayo tu ujue unakesha naye mpaka kuchee.

Pia wakashauri ushauri wa kichaa wakasema ikiwezekana kuwa naye bize sana mchana ili kajamaa kajamaa kakiangukia menyu ya jioni kanazimika mpaka chee sababu kanakuwa kamechokaa!
Na pia wakasema hakikisha mazingira ya nyumba no rafiki kwa mtoto kwani mtoto hajazoea kelele zenu za subwoofer na home theatre wanamiziki yao ambayo haina midundo mingi na makelele mliyozoea, huku piki,huko honi ya gari, huku sahani imevunjika nk. Wanasema wao wamezoea mziki wenye ala mmoja tu Mayo in mapigo ya Moyo wa mama yake wakati akiwa tumboni.,.ndio maana wanakushauri umlaze kifuani pako pia.

Nilisoma mengi Siku nzima...usiku wa siku alila SAA NNE asbh akastuka Saa sita tukakesha naye mpaka saa kumi...

The next day I did what google told me....I see Dogo alizimika Majira ya saa nne hivi akashtuka ngoma tisa akanyonya akazimika akastuka saa kumi na moja akanyonya akazimika mpaka asbh. Nilifurahi sana mpaka majirani wakàanza kuuliza kulikoni leo!
The next day nikamuweka mama watoto kando kabisa kazi take ikawa ni kulisha na kufua nguo..the rest nikadeal naye Dogo...Hapo nikajitangazia ushindi baba la baba
 
Ndugu Jerrymsigwa,
Pole sana kwa mtoto wako kuwa analia usiku wa manane.

Hapa kuna moja ya mambo haya mawili tu.

1. Labda mtoto hashibi.
Kuna mwana JF mmoja ametoa sababu hii ambayo hata mimi naungana naye.
Jaribuni kuhakikisha kuwa ananyonya maziwa ya mama na kushiba kabisa kabla hajalala, lakini pia mama anaweza kumwamsha mida ya saa 5 za usiku na kumnyonyesha.
Kama shida haitakwisha basi, atakuwa ana tatizo lingine ambalo nimelielezea hapa chini.

2. Huenda anasumbuliwa na mapepo.
Suala hili ni la ki imani zaidi. Kwa vyovyote vile mapepo au wengine wanaita mashetani yapo, wala hakuna ubishi. Kwasababu suala hili ni la ki imani, linahitaji kufanya maombi kwa Mungu ili yeye mwenyewe aingilie kati. Binafsi nina uhakika sana na maombi yanayofanywa na watu waliookoka ki ukweli kweli. Watu hawa wapo. Watu hawa wakimwomba Mungu huwa anawasikia kabisa na huwa anajibu maombi yao.
Kwahiyo nina kushauri uwatafute watu hawa ili wakusaidie. Kama utaamini ushauri wangu na kuwatafuta hawa watu ikawa ni vigumu kwako, naomba ufanye mrejesho halafu nitakupa contact za watu ninao wafahamu na kwamba wamesaidia watu wengi.

Mungu akusaidie uondokane na tatizo hilo maana hayo siyo mapenzi ya Mungu.
 
Mkuu asante sana kwa uzoefu huo, umenifumbua macho sana. Nitachanganya na ushauri wa wengine ili nifanikiwe, asante sana sana.Hapa nipo na google kujua kulikoni hiyo mambo
 
Ndugu Jerrymsigwa,
Pole sana kwa mtoto wako kuwa analia usiku wa manane.

Hapa kuna moja ya mambo haya mawili tu.

1. Labda mtoto hashibi.
Kuna mwana JF mmoja ametoa sababu hii ambayo hata mimi naungana naye.
Jaribuni kuhakikisha kuwa ananyonya maziwa ya mama na kushiba kabisa kabla hajalala, lakini pia mama anaweza kumwamsha mida ya saa 5 za usiku na kumnyonyesha.
Kama shida haitakwisha basi, atakuwa ana tatizo lingine ambalo nimelielezea hapa chini.

2. Huenda anasumbuliwa na mapepo.
Suala hili ni la ki imani zaidi. Kwa vyovyote vile mapepo au wengine wanaita mashetani yapo, wala hakuna ubishi. Kwasababu suala hili ni la ki imani, linahitaji kufanya maombi kwa Mungu ili yeye mwenyewe aingilie kati. Binafsi nina uhakika sana na maombi yanayofanywa na watu waliookoka ki ukweli kweli. Watu hawa wapo. Watu hawa wakimwomba Mungu huwa anawasikia kabisa na huwa anajibu maombi yao.
Kwahiyo nina kushauri uwatafute watu hawa ili wakusaidie. Kama utaamini ushauri wangu na kuwatafuta hawa watu ikawa ni vigumu kwako, naomba ufanye mrejesho halafu nitakupa contact za watu ninao wafahamu na kwamba wamesaidia watu wengi.

Mungu akusaidie uondokane na tatizo hilo maana hayo siyo mapenzi ya Mungu.

Sawa asante sana kwa ushauri wako mkuu, nimesikia na nimeelewa
 
nimejaribu kupitia comments zote naona hakuna itakayokusaidia Mkuu..

mimi nilikuwa na Mtoto mchanga na alikuwa Amalia pengine kuliko wa kwako..

na kuna siku nyingine ilinibidi kufidia usingizi ofisini maana usiku sikulala kabisa..

sasa shida nini?...mimi nilimpigia mama yangu kijijini akanishauri kitu..
1.muda wa kuoga kwa Mtoto badilisha yaani muogeshe usiku kama saa 3 hivi ili avute muda wa kulala..

lakini hii pia sio dawa ni kama first aid tu..

kwa ujumla mama alidai hakuna dawa ya kumfanya Mtoto mchanga asilie usiku..

Alidai Mtoto mchanga mifupa yake inavutika au kutanuka usiku na hali hiyo humfanya ajisikie maumivu...lakini

akishafikisha mwezi mmoja na nusu hali hiyo itaisha so usijisumbue kumnywesha dawa..may be grip water tu....

nataka nikuambie Mtoto wangu alivyofikisha mwezi mmoja na siku kadhaa ile hali iliisha kabisa...

sasa ni wewe mwenyewe.
 
Pia kama uto jali chukua punje 1 ya vitunguu swaumu kitoange akitaka kulala mpake kwenye viganja vyake na kwenye paji la uso kidogo tu
Or chini ya mto wake Wa kulalia weka kakipande kadogo ka mkaa
Ukishindwa kabisa mwekee biblia pembeni yake or msahafu(sijui nimepatia kuandika ) kutegemea na dini yako
Mwangalie kama kakojoa kila anapo anza kulia
Angalia my bee mmemjazia minguo ata watoto wanasikiaga joto
Wangu alokua analia ila ukiwasha feni ananyamaza we kaanza pigwa na feni kuanzia ana mwezi mpaka kesho bila feni alali.
 
Wakuu mtoto ananipa wakati mgumu sana, ana wiki 6 sasa na amekua analia sana usiku yani kilio cha yowe kabisa.

Nimejaribu kumpa dawa 'infacol' na bonnisan lakini tatizo bado liko pale pale shida itakua nini? Hizo dawa nimepewa baada ya kumuona pediatrician.
Alafu mida yake sasa ni kuanzia sa 7,8, 9 mpk sa10 tu kila siku. Mchana halii kabisa kabisa, daah ananipa wakati mgumu sana huyu mtoto.

Naomba uzoefu please
ni kawaida kwa watoto wachanga sio tatizo ni uchanga huo! achana na midawa!
 
choo kawaida tu, ila gesi ni mojawapo ya sababu coz huwa anajamba jamba sana. Hata ivyo niliambiwa na Doc kua Bonissan ndio inamaliza gesi tumboni. Cha ajabu ni kuwa mchana anakua poa sana isipokua ikifika sa 6-10 ni balaa mtoto anapiga yowe ni vile tu naishi nyumba sehem ambapo sio rahisi kusumbua jirani

Jaribu gripe water nzuri sana kwa gesi

Hongera sana kupata mtoto
 
hata wa kwangu alikua hivo huwa wakifika miezi 3 wanaacha
 
Dah sasa hivi nimekonda kweli maana silali usiku mtoto Analia na asubuhi job; ndy maana ukipiga mtoto wa mtu aisee mtu anakutoa mavi
Yaani mtoto anauma bwana tena ukianzia ata kwenye mimba inavyo sumbua uje uchungu uje akiwa na wiki up miezi3 anavyo sumbua bado hatua kila atua anaumwa akianza kukaa aumwe akianza kutambaa aumwe akianza kisimama aumwe akianza kutembea ndo kidogo unapumua alafu atokee tu boya anampiga piga bila ratiba maalumu duu inauma
 
Kuna uwezekano mkubwa hashibi hasa kama wa kiume,hiyo ni kisayansi,kama kiiimani aisee omba sana mtoto atakua anaona vitu vyakutisha,mda mbaya hu
 
nimeshauriwa asile vitu vyenye asidi mfano maziwa mgando, broccoli, cauliflower, malimao, machungwa, maharage, juice, lemonade nk viepukwe. Chips nooo hali
Kinachotengeneza maziwa ni protini,maharage na vitu vikali asile,ila machungwa na mtindi vinasaidia sana kufanya maziwa mazito,broccoli ni vegetable aliekuelekeza ajiongeze kaka,mimi ni mzazi wa watoto sita
 
Back
Top Bottom