Mstahiki Mea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 6,559
- 12,518
!!Wanaume kuna ujumbe wenu hapa...
✍Ripoti mpya ya Taasisi ya Vinasaba ya Smart DNA iliyo na makao yake nchini Nigeria imefichua kuwa kati ya watoto wanne, mmoja anakuwa sio mtoto halali wa baba anayedhaniwa na hivyo kuchochea kile ambacho wengi sasa wanakielezea kama mgogoro wa uzazi.
✍Ripoti ya Mwaka 2025 ya Uchunguzi wa DNA inaonyesha kuwa asilimia 25 ya vipimo vilivyofanywa kati ya Julai 2024 na Juni 2025 vilithibitishwa kuwa baba waliodhaniwa hawana uhusiano wa kibayolojia na watoto hao. Maombi mengi ya vipimo vya DNA yaliwasilishwa na wanaume ambao karibu nusu yao walikuwa na umri wa miaka 41 na zaidi.
✍Jambo la kustaajabisha zaidi ni kwamba, asilimia 64 ya vifungua mimba—hasa wavulana—waligunduliwa kutokuwa na uhusiano wa kibiolojia na waliodhaniwa kuwa baba zao, kiwango kikubwa zaidi kuliko cha watoto waliozaliwa baadaye.