Mtoto niliyemkataa miaka 4 iliyopita, anafanana na mimi. Sasa ameletwa karibu na ninapoishi

Mtoto niliyemkataa miaka 4 iliyopita, anafanana na mimi. Sasa ameletwa karibu na ninapoishi

Daah Mimi nilishampaga huyu demu million 1 nikamuambia tusijuane nashangaa karudi tena
Ohoo! Unashangaa amerudi tena! Kwani amekusemesha? Yeye si anaishi kwake na habari zake! Ila huyo mwanamke ni kiboko amejua kukutesa kisaikolojia!

Hapo lazima tu wewe ndio utakuwa wa kwanza kujiweka karibu naye ili kuua soo. Yeye wala hana hata habar na wewe mana silaha yake kubwa ni huyo mtoto kucheza na watoto wako!

Tena katika ulimwengu wa kiroho watoto wako na huyo dogo ipo nguvu inawaunganisha na ipo siku wataenda naye nyumbani kwako kutazama TV.
 
Namuonea huruma huyo mtoto asiye na hatia kuzaliwa na baba kama wewe.
Anyways huyo mtoto awe mtaani kwako au asiwe Mungu anaijua riziki yake na atamkuza kuwa mtu wa pekee maishani Hadi ushangae.
Dah baba anaogopa uwepo wako karibu nae 🙄🙄😭 nimevaa viatu vya huyo mtoto vinanibana
 
Wanajamvi aisee ni noma nilimKataa mtoto miaka kama minne imepita Sasa ubaya Leo kaja na mama yake sehemu ambayo karibu na kwangu mtoto anafanana na Mimi mpaka nimeona aibu nikaangalia pembeni Sasa ubaya mama yake sijui kafanya makusudi kahamia huu mtaa aisee yaani dogo Bora asingefanana na Mimi ni noma maana inapoelekea ndoa yangu itaharibika maana dogo anachezacheza na wenzake karibu na kwangu ubaya akija kuanza mazoea na wanangu naona kama nitaumbuka nishaurini nifanyaje wadau
Mchukue sasa unasubiri Nini?We Tahira kweli.Utaikimbia damu yako mpaka lini.
 
Duuh hii hatari dogo angekua hajafanana na Mimi ingekua kidogo afadhali au ningekua nimepanga mbona ningeacha Kodi ubaya nimejenga
Yatasaidia kitu hudumia mtoto wako naye akihudumiwa na wazazi wake ndio maana utamuona na kumuoa.hacha ujinga wa kusema mtoto wa nje ya ndoa hakuna kitu kama hicho,kwani shahawa zako zote ulimwaga ndani na sio nje.
 
Back
Top Bottom