Mtoto niliyemkataa miaka 4 iliyopita, anafanana na mimi. Sasa ameletwa karibu na ninapoishi

Mtoto niliyemkataa miaka 4 iliyopita, anafanana na mimi. Sasa ameletwa karibu na ninapoishi

Ohoo! Unashangaa amerudi tena! Kwani amekusemesha? Yeye si anaishi kwake na habari zake! Ila huyo mwanamke ni kiboko amejua kukutesa kisaikolojia!

Hapo lazima tu wewe ndio utakuwa wa kwanza kujiweka karibu naye ili kuua soo. Yeye wala hana hata habar na wewe mana silaha yake kubwa ni huyo mtoto kucheza na watoto wako!

Tena katika ulimwengu wa kiroho watoto wako na huyo dogo ipo nguvu inawaunganisha na ipo siku wataenda naye nyumbani kwako kutazama TV.
Duuh naomba isiwe hivyo aisee
 
Hamna sio kama naogopa ila naona nikimtambulisha dogo ataishi Kwa mateso sana namjua mke wangu
Kaa na mama yake muombe msamaha kisha umuombe uwahamishe mbali na hapo na uanze kutoa huduma kwa mwanao.
Narudia tena Mhudumie mwanao
 
Wanawake bwana wakiamua lao linakua. Ameona isiwe tabu utajileta mwenyewe na kweli umejaa maana ushaanza kuweweseka acheni kuchepuka na wanawake wasioeleweka. Halafu si ukae kimya tu kwani shida iko wapi? Mtego alioweka umeshaanza kuingia soon atakudaka acha kuwa mjinga
 
Mkuu kaa Chini na mama yake myaweke Sawa kisha tumia protokali za kifamilia mtoto atambulishwe nyumbani ( ila kusema ukweli mkuu inaonekana wewe ni mwanaume wa ovyo sana and very week)
 
Wanajamvi aisee ni noma nilimkataa mtoto miaka kama minne imepita.

Sasa ubaya leo kaja na mama yake sehemu ambayo karibu na kwangu, mtoto anafanana na mimi mpaka nimeona aibu nikaangalia pembeni.

Sasa ubaya mama yake sijui kafanya makusudi kahamia huu mtaa aisee yaani dogo bora asingefanana na mimi, ni noma.

Inapoelekea ndoa yangu itaharibika maana dogo anachezacheza na wenzake karibu na kwangu ubaya akija kuanza mazoea na wanangu naona kama nitaumbuka.

Nishaurini nifanyaje wadau.
Tubia hii dhambi
 
Wanawake bwana wakiamua lao linakua. Ameona isiwe tabu utajileta mwenyewe na kweli umejaa maana ushaanza kuweweseka acheni kuchepuka na wanawake wasioeleweka. Halafu si ukae kimya tu kwani shida iko wapi? Mtego alioweka umeshaanza kuingia soon atakudaka acha kuwa mjinga
Daah yaani huyu demu sijui anatafuta nini Mimi nilishasahau hii ishu tangia mwaka 2020 na yeye ndio alifosi mpaka akapata mimba
 
Mkuu kaa Chini na mama yake myaweke Sawa kisha tumia protokali za kifamilia mtoto atambulishwe nyumbani ( ila kusema ukweli mkuu inaonekana wewe ni mwanaume wa ovyo sana and very week)
Daah nilishaga muambia tusijuane tangia mwaka 2020 yaani kama nikikaa Naye chini kwenye kumhudumia si ndio atatumia fimbo ya kumleta mtoto karibu na ninapoishi Ili kunichapia
 
Back
Top Bottom