Mtoto niliyemkataa miaka 4 iliyopita, anafanana na mimi. Sasa ameletwa karibu na ninapoishi

Wanajamvi aisee nilimkataa mtoto miaka kama minne imepita.

Sasa ubaya leo kaja na mama yake sehemu ambayo karibu na kwangu, mtoto anafanana na mimi mpaka nimeona aibu nikaangalia pembeni.

Sasa ubaya mama yake sijui kafanya makusudi kahamia huu mtaa aisee yaani dogo bora asingefanana na mimi, ni noma.

Inapoelekea ndoa yangu itaharibika maana dogo anachezacheza na wenzake karibu na kwangu ubaya akija kuanza mazoea na wanangu naona kama nitaumbuka.

Nishaurini nifanyaje wadau.
Wewe unaujinga sana damu yako unaionea aibu badala ya kutubu yaishe ili upate muda wa kulea mtoto bado unajishtukia ..
 
Hivi una miaka mingapi kwanza? Damu yako unakuja kuomba ushauri ufanyaje? Ndoa inaweza kuvunjika, mkeo akapata mwanaume mwingine. Ila damu yako atakuwa nawewe mpaka uzee wako na anaweza huyu pekee ndiye akakujali, kuliko hao wa kwenye ndoa.

Ulijua una ndoa, ukaenda kufanyana huko bila protection. Sasa mlee huyo mtoto. Mkeo utajuana naye jinsi ya kumwambia. Ila huyo Malaika anza kupeleka matunzo, umri wa shule ukifika lipa ada. Huwa mnapata laana sababu ya hawa watoto, mnaowatelekeza.
 
Hiyo inaitwa ubaya ubwela,
Inategemea mtoto ulimkataa katika mazingira gani ila kitu cha muhimu zaidi kaa nae mzazi mwenzako muyamalize ulee mtoto huyo.
 
Hivi una miaka mingapi kwanza? Damu yako unakuja kuomba ushauri ufanyaje? Ndoa inaweza kuvunjika, mkeo akapata mwanaume mwingine. Ila damu yako atakuwa nawewe mpaka uzee wako na anaweza huyu pekee ndiye akakujali, kuliko hao wa kwenye ndoa.

Ulijua una ndoa, ukaenda kufanyana huko bila protection. Sasa mlee huyo mtoto. Mkeo utajuana naye jinsi ya kumwambia. Ila huyo Malaika anza kupekeka matunzo, umri wa shule ukifika lipa ada. Huwa mnapata laana sababu ya hawa watoto, mnaowatelekeza.
Daah sawa
 
Msichojua ni kwamba Mungu anapokubariki analeta Baraka kulingana na majukumu yako yaani analeta Baraka pamoja na za watu wanaokutegemea wewe. Sasa unapokataa kumpokea au kuwa karibu na huyo Dogo sio kwamba hataishi Ila unajifungia milango ya Baraka zingine na kujijazia laana bure kwa malalamko ya mama yake na mtoto mwenyewe.
Kama unakuwa na mashaka Bora ulee mimba akizaliwa mtoto ufanye DNA Mara Mia kuliko kukataa mimba baada ya nyie wawili kula starehe
 
Wanajamvi aisee nilimkataa mtoto miaka kama minne imepita.

Sasa ubaya leo kaja na mama yake sehemu ambayo karibu na kwangu, mtoto anafanana na mimi mpaka nimeona aibu nikaangalia pembeni.

Sasa ubaya mama yake sijui kafanya makusudi kahamia huu mtaa aisee yaani dogo bora asingefanana na mimi, ni noma.

Inapoelekea ndoa yangu itaharibika maana dogo anachezacheza na wenzake karibu na kwangu ubaya akija kuanza mazoea na wanangu naona kama nitaumbuka.

Nishaurini nifanyaje wadau.
Acha ujinga unakataaje mtoto ?
 
Wewe ndiyo mjinga maana unakataa damu yako.....
Jipige kifua mara mbili sema mimi ni mjinga sana, nakataa damu yangu sababu ya mwanamke niliyenae
 
Msichojua ni kwamba Mungu anapokubariki analeta Baraka kulingana na majukumu yako yaani analeta Baraka pamoja na za watu wanaokutegemea wewe. Sasa unapokataa kumpokea au kuwa karibu na huyo Dogo sio kwamba hataishi Ila unajifungia milango ya Baraka zingine na kujijazia laana bure kwa malalamko ya mama yake na mtoto mwenyewe.
Kama unakuwa na mashaka Bora ulee mimba akizaliwa mtoto ufanye DNA Mara Mia kuliko kukataa mimba baada ya nyie wawili kula starehe
Duuh sawa nitaifanyia kazi huu ushauri
 
Wanajamvi aisee nilimkataa mtoto miaka kama minne imepita.

Sasa ubaya leo kaja na mama yake sehemu ambayo karibu na kwangu, mtoto anafanana na mimi mpaka nimeona aibu nikaangalia pembeni.

Sasa ubaya mama yake sijui kafanya makusudi kahamia huu mtaa aisee yaani dogo bora asingefanana na mimi, ni noma.

Inapoelekea ndoa yangu itaharibika maana dogo anachezacheza na wenzake karibu na kwangu ubaya akija kuanza mazoea na wanangu naona kama nitaumbuka.

Nishaurini nifanyaje wadau.
Mwanaume wa kweli hakatai mtoto....mwanaume wa kweli anaahidi hata kama ni uongo......mwanaume wa kweli hakimbiiii mtoto wake

Hakunaga straiker wa kweli akakataa goli jombaaa....goli linakataliwaga na refaa sio straiker.....

KAMA unajiaminisha ulikojoa basi mbona unamkataaa chaliii hebu beba mwanao acha mazingaombwe bana!
 
Back
Top Bottom