Mtoto niliyemkataa miaka 4 iliyopita, anafanana na mimi. Sasa ameletwa karibu na ninapoishi

Mwanaume wa kweli hakatai mtoto....mwanaume wa kweli anaahidi hata kama ni uongo......mwanaume wa kweli hakimbiiii mtoto wake

Hakunaga straiker wa kweli akakataa goli jombaaa....goli linakataliwaga na refaa sio straiker.....

KAMA unajiaminisha ulikojoa basi mbona unamkataaa chaliii hebu beba mwanao acha mazingaombwe bana!
Sawa mkuu
 
Acha kuwa na matatizo na kujitakia laana zisizo za lazima. fanya mazungumzo na mama yake mzazi, then na mkeo ili umchukue mtoto apate malezi ya pamoja na wanao. Unaweza kuta rais wa Taifa la kesho.
 
Ushasema mama wa kambo atatamtesa...
Usimchukue mtoto
Kwa kuwa mama yake yuko hai wewe mhudumie huko huko Ila familia yako I mean ndugu zako wajue kuna mwana ukoo ameongezeka.

Mke wako atajua taratibu sio lazima kwa hatua za awali
 
Sawa dada nimekuelewa vizuri aisee
 
Sawa mkuu
Asante kwa kunielewa. Mimi nina majembe matatu (wawili jembe na moja dada yao) niliowapata nje ya 18 but wote nakaa nao na wanasoma shule sawa na ndg zao waliopatikana ndani ya 18. Tena hatari yangu wawili nilikuja kuwapata wakati tayari nipo kwenye kiapo. Ilikuwa hatari kwelikweli but mwishowe mama yoyo alikuja kunielewa ingawa mwanzoni nilikula makwenzi kidogo ya hasira za mama yoyo.
 
Wanajamvi aisee nilimkataa mtoto miaka kama minne imepita.

Sasa ubaya leo kaja na mama yake sehemu ambayo karibu na kwangu, mtoto anafanana na mimi mpaka nimeona aibu nikaangalia pembeni.

Sasa ubaya mama yake sijui kafanya makusudi kahamia huu mtaa aisee yaani dogo bora asingefanana na mimi, ni noma.

Inapoelekea ndoa yangu itaharibika maana dogo anachezacheza na wenzake karibu na kwangu ubaya akija kuanza mazoea na wanangu naona kama nitaumbuka.

Nishaurini nifanyaje wadau.
Kwa hiyo unataka tukusaidieje mpaka hapo kwa mfano? Tumchukue mkeo?
 
Wanajamvi aisee nilimkataa mtoto miaka kama minne imepita.

Sasa ubaya leo kaja na mama yake sehemu ambayo karibu na kwangu, mtoto anafanana na mimi mpaka nimeona aibu nikaangalia pembeni.

Sasa ubaya mama yake sijui kafanya makusudi kahamia huu mtaa aisee yaani dogo bora asingefanana na mimi, ni noma.

Inapoelekea ndoa yangu itaharibika maana dogo anachezacheza na wenzake karibu na kwangu ubaya akija kuanza mazoea na wanangu naona kama nitaumbuka.

Nishaurini nifanyaje wadau.
usikubali kufanya kitu cha kijinga kwa mara ya pili.
huyo dogo kuhamia karibu ni fursa ya pili kwako.
usiogope ndoa kuvunjika kipi bora ndoa ivunjike au upoteze mtoto?
ninachoweza kukushauri kama utaelewa:-
kaa kwanza na mama wa mtoto muelewane na mwonyeshe nia yako ya kumkubali mtoto
jitambulishe kwa wazazi wake kuwa wewe ndiye baba halali wa mtoto (tena watume watu wazima wakaongee)
kuwa tayari kulipa fidia iwapo watahitaji na inawezekana usilipe zote lakini sehemu tu ya hicho utakachopangiwa
ahidi kumtunza mtoto na kumsomesha.
tafuta upatanishi wa wewe na mtoto kwakuwa nafsi yake inajua ulimkataa na hakuelewi.
ukilimaliza nje ndani liache lilipuke lenyewe ukiulizwa majibu yatakayotoka muda huo ndio yanafaa kwa bahati mapenzi na ndo hayahitaji sana majawabu bali majibu ambayo sio lazima yawe sahihi sana.
 
Daah sawa mkuu nimekuelewa nitafanya hivyo
 
Back
Top Bottom