Makonda ni kiongozi mzuri sana, ila shida inakuja maadui zake Huwa hawapendi Yeye kung'ara, na mara nyingi Huwa wanamsubiri akiwa mbele za watu, kuna namna wanafanya anaongea mambo yanayomshusha Yeye mwenyewe.
Sidhani kuna BAYA litampata.
Aongeze umakini tu.
Ila ni kiongozi mkubwa sana, sababu anawapenda watu wa ardhi anayoiongoza sio anapenda uongozi.
Ingekuwa anapenda uongozi tungeona vile anatoka Uenezi kwenda RC akififia.
Anapenda kutatua matatizo na ni nadra sana jamii kuwa na watu wa namna hii.
Alishughulikie Hilo kuthibiti kuchezewa kauli anapokuwa mbele za watu na kuongozwa akili nje ya mapenzi yake.
Jamii ilipaswa kumlinda Paul Makonda na si vinginevyo, hivyo ndivyo nionavyo Mimi.