Tetesi: Mtoto pendwa kapatwa na nini? Yuko hoi kwa Madiba, inadaiwa ni sumu
Hivi kwanini watanzania tumekuwa na roho za ajabu kiasi hiki ?

Habari za watu kuumizwa ndizo zinatupa faraja, na huwa tunazitoa kwa ushabiki sana. Nadhani hili siyo jambo jema sana!


Ni kweli kabisa.

Unajua maskini hua hawana visasi vikubwa sana na ni wepesi wa kusalehe na kusahau mana hawawazi mambo makubwa ya mbeleni kama matajiri.

Huwezi kusikia maskini anashangilia kifo cha mtu.
Tajiri akifa hata kama alikua na matatizo na roho Mbaya kiasi gani lakini mara nyingi maskini anaweka chuki pembeni na kwenda kumzika na hata kukesha kwenye msiba lakini Tajiri hasa mtu tajiri wa dhulma au wa uchawi hanaga kitu Msamaha au huruma .

Kuna kundi fulani la Wala nchi wanzoshirikiana na wafanyabiashara wakwepa kodi na wauza madawa. Hawa kila mpenda haki ni adui yao mkubwa . Hawa wakisikia kifo cha mtu hua hawasikitili zaidi ya kukaa na kunywa wine kwa furaha kubwa.

Ni kundi la waovu wanaoishi kwa damu za watu . Hawa ndio wanaosababisha mpaka mauaji ya albino na biashara za viungo vya binadamu.

Maskini mtoto wake anaweza akauawa,mke wake akachukuliwa na wakubwa , mtoto wake akalawitiwa na watu wenye majina makubwa lakini akanyimwa haki yake na akasamehe lakini matajiri na wakubwa wao hata kuwaambia ukweli ni kosa linalostahili mtu kufa.

Hii ni mifumo ya lishetani iliyopakwa rangi nje lakini ni kama makaburi yanayopendeza kwa kunakshiwa vizuri kwa nje lakini ndani yake kuna mifupa mitupu .

Nchi za magharibi na wazungu ni mfano wa watu waovu wanaopenda kutendewa mema tu huku wao wakiwatendea wanadamu wenzao maovu makubwa na kuwasababishia mauaji makubwa bila huruma.
 
Back
Top Bottom