The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,778
- 8,232
WAZAZI "PARENTS =PAIR RENT
Katika ulimwengu mzazi ni yule aliyemleta mtoto duniani – mama na baba
Hiyo ni tafsiri ya kijamii na kibiolojia. Lakini katika ulimwengu wa kiroho na hekima ya ndani, jukumu la mzazi lina maana pana zaidi inayogusa roho na asili ya uhai.
Uumbaji wa maisha unahitaji muungano wa nguvu mbili – ya kiume na ya kike. Jozi hii inakuwa daraja la kuipitisha nafsi kutoka ulimwengu wa kiroho kuja duniani. Kila mmoja huchangia sehemu ya uhai, na kwa pamoja wanaunda lango la kuzaliwa kwa roho mpya. Hakuna uumbaji pasipo us hirikiano huu.
Mtoto anayezaliwa si mali ya mzazi, bali ni roho huru iliyopewa nafasi kupitia miili ya wazazi. Wazazi wanapewa dhamana ya muda ya kumtunza na kumlea mtoto, si kumiliki maisha yake. Ni kama walinzi wanaopewa jukumu takatifu la kuhakikisha roho hiyo inakua salama na inafikia makusudi yake duniani.
Hivyo, Mzazi ni Mshirika wa uumbaji aliyeaminiwa kwa muda kulea roho ya mtoto ili iendelee na safari yake duniani..
Ndani ya neno PARENT, tunakutana na sehemu mbili zenye uzito wa kiroho:
"Pair" humaanisha wawili – mwanaume na mwanamke, nguvu ya kiume na ya kike. Katika uumbaji wa maisha, hawa wawili hushirikiana kuleta roho mpya duniani. Kila mmoja anatoa sehemu ya kipekee ya uhai, na kwa pamoja wanakuwa daraja la kuipitisha nafsi kutoka ulimwengu wa kiroho hadi ulimwengu wa mwili. Uumbaji unahitaji muungano – huu ndio msingi wa "pair".
"Rent" ni kukodisha kwa muda mfupi. Katika muktadha wa kiroho, mtoto anayezaliwa si mali ya wazazi wake, bali ni roho huru iliyokodisha miili ya wazazi kwa muda ili kuja duniani. Wazazi wamepewa dhamana ya muda ya kuilea, si kumiliki maisha yake. Wao ni walinzi wa muda wa zawadi ya uhai. Ni kama chombo kinachoaminika kuifanikisha safari ya nafsi duniani.
Kwa hiyo, “Parent = Pair + Rent” humaanisha:
Mzazi ni jozi ya wanadamu waliokodishwa jukumu la kulea maisha ya roho kwa muda fulani.
Na kwa sababu hiyo...
Usilazimishe mtoto awe kama ulivyokuwa, Wala usimlazimishe awe vile unavyotaka awe. Mtoto hakuzaliwa kutimiza ndoto zako, bali ndoto zake mwenyewe. Mzazi ni mwanga wa njia, si kizuizi cha safari.
Saidia kulea kilichomo ndani yake, Hicho alichozaliwa nacho, sio unachotaka umuundie. Msaidie kukua kuelekea ukuu wake mwenyewe, Kwa maana ndani yake kuna mbegu ya kusudi lake la kipekee duniani.
“Watoto wako Maisha, yanayo ishi kupitia wewe. Wanapitia kwako, lakini hawatoki kwako. Unaweza kuwapa upendo wako, lakini si mawazo yako. Kwa maana wana mawazo yao wenyewe.” — Khalil Gibran
Mzazi sio tu mtu aliyemzaa mtoto, bali ni sehemu ya muungano wa kiungu, aliyepewa jukumu la muda (rent) la kulea roho ya uhai. Uzazi ni ibada. Ni huduma kwa Maisha. Ni daraja kati ya mbingu na dunia.
Kila mzazi anapaswa kulitafakari hili kwa moyo wa unyenyekevu, upendo, na heshima kwa safari ya kipekee ya mtoto wake.