Mtoto wa Hilal Sood, mzawa wa mkoa wa Shinyanga alamba ubalozi akiiwakilisha Oman. Hii imekaaje?

Mtoto wa Hilal Sood, mzawa wa mkoa wa Shinyanga alamba ubalozi akiiwakilisha Oman. Hii imekaaje?

Na ishi shinyanga. Kwetu na kwa phantom ni tofauti ya Nyumba 4-5 sijawah kumwona. Ni wake kweli lakini shy labda anakuja na kuondoka na kwenye misiba ambapo wakifiwa na sisi hatuendagi sbb wao hawaji yetu. Hivyo nampongeza
 
Labda jamaa wamemtanguliza aweke mazingira sawa ili Twiga waanze kukwea pipa.
 
Miaka iliyopita kulikuwa na jamaa mmoja anaitwa Alex Halid ndiye alikuwa mmiliki wa baa moja maarufu maeneo ya kibamba ilikuwa ikiitwa Makondeko, huyo jamaa aliwahi kuwa balozi wa heshima akiiwakilisha nchi ya shelisheli nchini ingawa alikuwa ni Mtanzania kutoka kusini mkoani Mtwara.
Hivyo hata huyo Mwarabu inawezekana naye kapewa ubalozi wa heshima japo sio raia wa Oman.
Nani kakwambia kua huyo balozi sio raia wa Oman?
Huyo ni raia wa Oman,hata wewe unaweza ukawa raia wa nchi yeyote ile,ni uamuzi wako tu.
 
Nani kakwambia kua huyo balozi sio raia wa Oman?
Huyo ni raia wa Oman,hata wewe unaweza ukawa raia wa nchi yeyote ile,ni uamuzi wako tu.
Nimetoa maoni yangu tu hivyo sina sababu ya kubishana na wewe kwani huenda unamfahamu zaidi,pole sana kama nimekwaza endeleeni na mjadala wenu.
 
Ni raia wa Tanzania au Omani? Ubalozi amepewa na Tanzania au Omani? na kuiwakilisha Tanzania au Omani wapi?
huyo ni raia wa oman hata baba yake hilal soud ni raia wa oman japo wazazi wao walitokea nzega na kuhamia shinyanga
 
Dunia ya sasa sio ile ya zamani ya sasa watu wanaangalia uwezo na utii kwa nchi, waingereza wana mawaziri wahindi kama Rishi Sunak (waziri wa fedha) na Priti Patel (mambo ya ndani) na pia waziri wa afya Sajid Javid mwenye asili ya pakistani. Kwahiyo ni sawa kabisa.
 
kuna siku mtanielewa....

issue ipo kwente uaminufu kwenye nchi ambayo sio asili yenu bali babu zenu walikuja au wenyewe mlikuja mkaaminiwa mkakubalika kuwa Raia.....JE NI WAAMINIFU KWA NCHI ILIYOWAAMINI NA KUWAPA URAIA KWA KUFUATA HISTORIA AU NDIO OPPORTUNITY YA KUTUMIA CHANCES NA KWASIRI MKITUMIKIA ASILI ZETU MTOKAKO HUKU MKIKANDAMIZA WALE WALIOWAAMINI KWA SIRI..?
 
Hawa watu ni waaminifu kwetu kama sisi tulivyowaaminifu kwao na kuwaita Watanzania....Utanzania kweli uko kwenye mioyo yao au wapo kwa manufaa lakini mioyoni wanaukana utanzania wakijua wapo kuchuma na kutumikia asili zao?...
 
RWANDES,

..unaweza kutueleza kwa ufupi Hilal Sood ni nani? Jinsi ulivyoiweka mada yako ni kama vile wasomaji wako tunao wasifu wa Hilal Sood.

..kwasababu unadai mteuliwa alizaliwa na kukulia Tz, je unafahamu lini aliachana na uraia wa Tz?
 
Watu weupe ni wajanja sana, kuna kitu wanakiona miaka mia kadhaa mbele, wanaanza kukitengenezea mazingira sasa
 
Naona waarabu wanaona kama Tanzania ni nchi yao kabisa ila wanahisi ni kama waliporwa hasa Zanzibar
 
Back
Top Bottom