Mtoto wa Kanye North: nitapenda kumchagua baba kuliko Mama

Mtoto wa Kanye North: nitapenda kumchagua baba kuliko Mama

Swensa

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
2,880
Reaction score
4,295
Mtoto wa Kanye West na Kim Kardashian aitwaye North amesema kama akiulizwa aishi na nani basi ni bora aishi na baba yake kuliko mama yake, tena atachagua hivyo hata akiulizwa mara elfu moja.

Anasema:

“Nitamchagua baba yangu siku yoyote ile nikiulizwa. Baba yangu ndiye shujaa wangu. Baba yangu yupo bize sana lakini hata awe bize kiasi gani huwa hasahau kama yeye ni baba.

“Hufanya kila kitu yeye kama yeye, ananipikia, ananijali na ananifanya niwe na usalama muda wote.

“Hatuna mfanyakazi wa ndani, mpishi wala mlinzi, ni sisi tu, na huwa ninapenda hivyo. Nilipokuwa naisha na mama mambo yalikuwa ni tofauti. Muda wote kunakuwa na watu wengine ambao hubeba vitu vyetu, hata tunapokuwa nyumbani, huwa wapo tu na sijui mama anafanya kazi gani.

“Lakini baba yangu? Najua yeye ni mwanamuziki, anarap, na nitakapokua, ninatamani kuwa kama yeye. Niwe na nguvu kama zake, niwe mbunifu na ninayependwa na kupenda watu. Ninampenda baba yangu sana, ni baba bora ambaye najivunia kuwa naye.”

JApokuwa Kim alimbeba North kwa miezi tisa, akamnyonyesha kwa miezi sita na nusu, bado North anamchagua baba yake dhidi yake. Mashabiki wamekuwa wakiuliza, kwa nini mtoto huyo anamchagua baba yake dhidi ya mama yake?
Screenshot_20251017-092930.jpg
 
Safi kabisa mtoto mzuri, wanawake wote ni mashetwani hasa mama yako amezidi kabisa, badala ya kukunyonyesha miaka 2 amekupa ziwa miezi 6 tu na nusu, hapana kabisa hii ni mbaya, wanaume kunapoint 3 za kunyakua hapa.
 
Watoto huwapenda watu wanaowajali na kua nao muda wote!
Wababa wengi wanalalamika kwanini watoto wanawapendelea kina mama sasa jibu mshalipata.
 
Mtoto kajionea mama anachofanya kaona ujinga tu,familia imejaa mijitu sijui wapishi Mara wabeba mikoba wa mama,wapiga picha wa mama,Mara wasaidizi halafu mama hajigusi hata kumjali mtoto unadhani hawaoni
Watu muelewe fedha sio kila kitu bali upendo
Kanye kachukua point hapo
 
Ukiishusha kwetu huku uswahilini wamama wamekuwa busy sana na mambo yao binafsi.

Mtoto anaweza kuita mama, mama,mama,mama zaidi ya mara kumi bila kuitikiwa au anaitikiwa bila hata KUANGALIWA USONI YAANI ILIMRADI AMEITIKA jitu lipo busy na simu tu tena anachofatilia ni upuuzi mtupu.

Mwanamke akitoka kazini ndio muda wa kushika simu vizuri.
 
Back
Top Bottom