Mtoto wa Kanye West na Kim Kardashian aitwaye North amesema kama akiulizwa aishi na nani basi ni bora aishi na baba yake kuliko mama yake, tena atachagua hivyo hata akiulizwa mara elfu moja.
Anasema:
“Nitamchagua baba yangu siku yoyote ile nikiulizwa. Baba yangu ndiye shujaa wangu. Baba yangu yupo bize sana lakini hata awe bize kiasi gani huwa hasahau kama yeye ni baba.
“Hufanya kila kitu yeye kama yeye, ananipikia, ananijali na ananifanya niwe na usalama muda wote.
“Hatuna mfanyakazi wa ndani, mpishi wala mlinzi, ni sisi tu, na huwa ninapenda hivyo. Nilipokuwa naisha na mama mambo yalikuwa ni tofauti. Muda wote kunakuwa na watu wengine ambao hubeba vitu vyetu, hata tunapokuwa nyumbani, huwa wapo tu na sijui mama anafanya kazi gani.
“Lakini baba yangu? Najua yeye ni mwanamuziki, anarap, na nitakapokua, ninatamani kuwa kama yeye. Niwe na nguvu kama zake, niwe mbunifu na ninayependwa na kupenda watu. Ninampenda baba yangu sana, ni baba bora ambaye najivunia kuwa naye.”
JApokuwa Kim alimbeba North kwa miezi tisa, akamnyonyesha kwa miezi sita na nusu, bado North anamchagua baba yake dhidi yake. Mashabiki wamekuwa wakiuliza, kwa nini mtoto huyo anamchagua baba yake dhidi ya mama yake?