Dah na unadhani utambadilisha kwa likizo ya mwezi mmoja tabia ambayo anafanya kwa miezi kumi akiwa shule!bottom line tulee watoto wetu wenyewe ili wawe na hizo tabia tunazozitaka ili wasipokua nazo tusijilaumuZile siku anazokuja likizo unamwambia asafishe chumba chake na kuandika kitanda, unamfundish kupika vitu kama wali, kuchemsha nyama au maharage, kukata vitunguu
Wamama wazaman walipata Mafunzo kwa wazazi wao. Ndio maana walikuwa wazazi na walez bora watoto wa siku hizi wanafundwa whatsapp Kwenye groups huko, wakati ni elimu ya bure angeipata kwa mama yake au mlez aliyemlea
Kama ni boyfriend hajanioa simfulii nguo, ninaweza kumsaidia kusafisha nyumba na kupika. Atauona usafi wangu akija kwangu. Mkizoeshwa kufuliwa, kupigiwa pasi na kupewa vitamu mnasahau kuoa
Ndio maana nikasema kusoma mazingira na kuwa karibu na wenyeji itakusaidia kujua wenyeji wako lifestyle yao ikoje,.wengine hawataki kabisaa wageni wajihusishe na vitu vyao na kuna family zingine ukifika basi ndio ule msemo wa"mgeni njoo mwenyeji apone"hutumika kwahiyo kila mahali na utaratibu wake,lakini kwa mtt wa kike ni vema kusoma mazingira mapema ili kuepuka kuacha sifa mbaya unapoondoka.Mkuu siku ya kwanza tu ukishaosha sahani yako unauliza sahani zinakaa wapi, asubuhi unadust nyumba na kuuliza upike nini?
Ulimwengu unakuharibu alafu unajifunza kutokana na makosaKama mama yake kashindwa kumfunda, acha ulimwengu umfunde.
SanaMafunzo ya ulimwengu ni makali sana
Ulimwengu unakuharibu alafu unajifunza kutokana na makosa
Sasa kama wewe mwenyewe huoni pachafu yeye ataona vipi?Hakuna kitu kinanishinda kama madada wa siku hizi.Yan mtu anakuja kukutembelea lets say mpenzi halafu mkoba umejaa SEASONS.Akifika ni mwanzo wa kuangalia seasons tu.
Hawezi kuona kama pachafu asafishe au kuna nguo chafu afue yeye ni seasons na kuomba apewe chips.Akipanda kitandani zero kabisa.
Wala hakuna mzazi anaekimbia kumlea mwanae hata cku moja na mtoto anaweza akawa day na bado akawa mvivu wa kujishughulisha hapo ni mzazi kumkazania mwanao kusaidia kazi na kumpangia, kwani akitoka boarding unashindwa kumuelekeza au kumpangia ratiba ya kufua kudeki kuosha vyombo???? Ni malezi boarding day sio swala la mtoto kua mvivu ni malezi ya wazaziNaona unajipa matumaini mrudishe mtoto nyumbani umlee mwenyewe!Yaani mtoto wa miaka 5 aanze boarding hadi anafika Chuo na awe na tabia sawa na mtoto aliyelelewa vizuri na wazazi?Unamlea mwanao miezi miwili kwa mwaka na analelewa na Ulimwengu miezi 10;Mtoto peleka boarding akiwa secondary kidogo inaelezeka acheni kukimbia majukumu