Mtoto wa kike akiwa ugenini

Mtoto wa kike akiwa ugenini

Zile siku anazokuja likizo unamwambia asafishe chumba chake na kuandika kitanda, unamfundish kupika vitu kama wali, kuchemsha nyama au maharage, kukata vitunguu
Dah na unadhani utambadilisha kwa likizo ya mwezi mmoja tabia ambayo anafanya kwa miezi kumi akiwa shule!bottom line tulee watoto wetu wenyewe ili wawe na hizo tabia tunazozitaka ili wasipokua nazo tusijilaumu
 
Mimi nilipata shida Sana course nilisoma boarding kuanzi primary Hadi advance...Kuna kipindi nilikuwa sijui sauti ya mzee au mama...yani asingekuwa Bibi yangu dah sijui leo ningekuaje!!
 
Wamama wazaman walipata Mafunzo kwa wazazi wao. Ndio maana walikuwa wazazi na walez bora watoto wa siku hizi wanafundwa whatsapp Kwenye groups huko, wakati ni elimu ya bure angeipata kwa mama yake au mlez aliyemlea

Kama mama yake kashindwa kumfunda, acha ulimwengu umfunde.
 
Mkuu siku ya kwanza tu ukishaosha sahani yako unauliza sahani zinakaa wapi, asubuhi unadust nyumba na kuuliza upike nini?
Ndio maana nikasema kusoma mazingira na kuwa karibu na wenyeji itakusaidia kujua wenyeji wako lifestyle yao ikoje,.wengine hawataki kabisaa wageni wajihusishe na vitu vyao na kuna family zingine ukifika basi ndio ule msemo wa"mgeni njoo mwenyeji apone"hutumika kwahiyo kila mahali na utaratibu wake,lakini kwa mtt wa kike ni vema kusoma mazingira mapema ili kuepuka kuacha sifa mbaya unapoondoka.
 
Hakuna kitu kinanishinda kama madada wa siku hizi.Yan mtu anakuja kukutembelea lets say mpenzi halafu mkoba umejaa SEASONS.Akifika ni mwanzo wa kuangalia seasons tu.
Hawezi kuona kama pachafu asafishe au kuna nguo chafu afue yeye ni seasons na kuomba apewe chips.Akipanda kitandani zero kabisa.
Sasa kama wewe mwenyewe huoni pachafu yeye ataona vipi?
 
well said mkuu, malezi yana changamoto sana siku hizi ukijumlisha na mambo ya internet ndio balaa tupu.
 
Naona unajipa matumaini mrudishe mtoto nyumbani umlee mwenyewe!Yaani mtoto wa miaka 5 aanze boarding hadi anafika Chuo na awe na tabia sawa na mtoto aliyelelewa vizuri na wazazi?Unamlea mwanao miezi miwili kwa mwaka na analelewa na Ulimwengu miezi 10;Mtoto peleka boarding akiwa secondary kidogo inaelezeka acheni kukimbia majukumu
Wala hakuna mzazi anaekimbia kumlea mwanae hata cku moja na mtoto anaweza akawa day na bado akawa mvivu wa kujishughulisha hapo ni mzazi kumkazania mwanao kusaidia kazi na kumpangia, kwani akitoka boarding unashindwa kumuelekeza au kumpangia ratiba ya kufua kudeki kuosha vyombo???? Ni malezi boarding day sio swala la mtoto kua mvivu ni malezi ya wazazi
 
Kuna tatizo kubwa katika jamii jamani, mabinti hawawezi kuwa hivyo wao wenyewe tu.

Kuna kiini kilichowafanya wao wawe hivyo na wengine wawe tofauti. Ni nini?

Mmomonyoko wa maadili katika jamii? Kuvunjika kwa familia zenye baba na mama wanaojielewa? Uhamiaji wa watu wengi kutoka vijijini kuja mijini bila maandalizi mazuri ya kielimu? Msongo wa mawazo kutokana na mabadiliko ya maisha ambayo hayajatolewa elimu nasaha? Mlipuko wa urahisi wa upatikanaji habari na teknolojia rahisi inayosababisha watu waone tamaduni za kigeni kuwa kama zetu?
 
Back
Top Bottom