😊Labda angekuwa wa kiume mm nmelala na mshua had miaka 13 (m)Mimi ni single mother wa mtoto wa kike wa miaka 10. Nipo kwenye mahusiano ya kimapenzi na single father mwenye binti wa miaka 9.
Watoto wetu wanasoma shule moja madarasa tofauti. Tulikutana kwenye mkutano wa wazazi shuleni. Hali ya kuwa single parent ilituunganisha, tukajikuta tupo mapenzini. Tumekuwa msaada kwa kila mmoja wetu kwenye malezi.
Hatuishi pamoja officially ila tunatembeleana na sleepovers za mara kwa mara.
Tatizo ni huyu mtoto wangu kupitia mpenzi wangu, anapenda kulala na babake. Babake anasema ndio yuko hivyo kwani ameanza kumlea toka ana miezi 6 na hivyo kubidi kulala nae toka umri huo. Ameshindwa kum'wean'.
Akilala peke yake au na mwanangu hapati usingizi, inabidi aje chumbani kwetu tulale nae, either hadi asubuhi au tumhamishe kwa kumbeba akiwa ameshalala.
Naomba ushauri nifanye nini kumsaidia huyu mtoto aweze kujitegemea.
Natanguliza shukran wapendwa.
Mtoto umleavyo ndivo akuavyo