Mtoto wa kiume hasa hasa graduate kamwe usikubali kuishi kwa shemeji yako ( mme wake na dada yako) ni laana

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Wakuu kwema

Hizi mvua mvua zinazonyesha hapa Bariadi leo nimeshuhudia graduates anayeishi kwa dada yake akipewa maelekezo na shemeji yake (mme wake na dada yake), ahamishe trip nne za mchanga (matipa/malori manne) kutoa nje kifusi cha mchanga kuingiza uwani (ndani ya fensi/ uzio).

Sababu mvua zinanyesha mchanga unasombwa na maji, jamaa ana mwili mdogo halafu kapewa amri ya kuingiza mlima mkubwa wa mchanga peke yake 🥺 aisee. Yaani mchanga wa kuzungushia mawe tu kisha hautabebwa na maji ila dogo kaambiwa wote uingie ndani tena kwa kutumia ndoo za lita tano tano.

Mimi Omoyogwane kwa ule mlima ukiniambia niubebe wote ngetumia hata mwezi mzima ila dogo kaambiwa aungize mchanga wote ndani ya siku moja 😆 .

Aisee mtoto wa kiume usikubali kuishi kwa shemeji yako ni laana ni kheri kuwa mfungwa ila sio kukaa kwa shemeji yako.

Niliyoyaona leo yamenifikirisha sana kuna vijana wanapitia magumu sana.

Nawasilisha.
 
Hakuna laana yoyote.

Hakuna anaependa kuishi kwa mtu, hata nyumbani tu watu hawapendi kuishi. Ni mtu kukosa alternative ndio anaamua kuishi kwa watu.

Kuishi kwa shemeji hakuna ubaya wowote as long as unaishi pale temporarily huku ukiweka michongo yako sawa.
 
Unakuta wanavutwa masikio na vi~kina "junia"na kupokonywa nyama wanabaki kuchekacheka sababu ya kupenda mserereko!!heri urudi kwenu ukakae kuliko kwa shemeji maana unapelekea dadako kukazwa kwa hasira ili usikie uondoke ila unakuta mtu na mzuzu wake yupo tu....inasikitisha sana!
 
How did we reach to this foolish mentality as a country ?
 
Haya hutokea kwa familia masikini na fukara dada mtu anapoolewa na mtu mwenye uwezo mzuri kiuchumi ukoo mzima hukumbilia huko kusaidiwa, ukute dada naye ana kazi ni muajiriwa mshahara upo basi wadogo zake humuona ni mkombozi wao kuwasomesha. Itabidi wapige kambi hapo mpaka na wao wajitegemee bila kuona aibu kwa shemeji yao hata akiwanunia wanaona poa tu
 
Umeshasema hao watu wanatokea familia masikini, halafu unataka waone aibu, kipi bora, uwe arrogant ufe na njaa ama uwe humble uishi kwa shemeji huku ukila na kutafta alternative ya maisha?. Uone aibu ufe njaa ama usione aibu uishi? Mimi nitachagua kuishi, aibu ni ya muda kifo ni cha milele.
 
Wakuu kwema

Hizi mvua mvua zinazonyesha hapa Bariadi leo nimeshuhudia graduates anayeishi kwa dada yake akipewa maelekezo na shemeji yake (mme wake na dada yake), ahamishe trip nne za mchanga (matipa/malori manne) kutoa nje kifusi cha mchanga kuingiza uwani (ndani ya fensi/ uzio).

Sababu mvua zinanyesha mchanga unasombwa na maji, jamaa ana mwili mdogo halafu kapewa amri ya kuingiza mlima mkubwa wa mchanga peke yake 🥺 aisee. Yaani mchanga wa kuzungushia mawe tu kisha hautabebwa na maji ila dogo kaambiwa wote uingie ndani tena kwa kutumia ndoo za lita tano tano.

Mimi Omoyogwane kwa ule mlima ukiniambia niubebe wote ngetumia hata mwezi mzima ila dogo kaambiwa aungize mchanga wote ndani ya siku moja 😆 .

Aisee mtoto wa kiume usikubali kuishi kwa shemeji yako ni laana ni kheri kuwa mfungwa ila sio kukaa kwa shemeji yako.

Niliyoyaona leo yamenifikirisha sana kuna vijana wanapitia magumu sana.

Nawasilisha.
unaweza kuishi popote kama hauna namna. ni bora upewe chumba kwa shemeji ili ujipange kuliko kuhamia kwa mishangazi, kwa washkaji na kwengine. hakuna anayependa ila ni mchakato wa maisha. nimeshawahi kuishi kwa dada enzi hizo, alinisaidia sana hadi nilipojipanga na kusimama. sioni shida.
 
Mkishayapatia maisha mnajisahau sana ndio kama kuna muda nilikua kwa group fulani kukawa na mchango wa 10k kwa kila memba kuna mmoja akasema hana kuna bwege mmoja akasema mtoto wa kiume unakosaje 10k kukaa kwa shemeji sio dili ila wanaokaa hawapendi
 
Sijaona kitu kibaya kwa mdogo mtu kwenda kukaa kwa dada yake ni ubinafsi kusema mdogo mtu hawezi kukaa kwa dada yake hata kwa muda mfupi.Hakuna anayependa kukaa kwa watu ni vile vitu havijakaa sawa na pia kumbuka shida humpata kila mtu duniani
 
Hakuna laana yoyote.

Hakuna anaependa kuishi kwa mtu, hata nyumbani tu watu hawapendi kuishi. Ni mtu kukosa alternative ndio anaamua kuishi kwa watu.

Kuishi kwa shemeji hakuna ubaya wowote as long as unaishi pale temporarily huku ukiweka michongo yako sawa.
Nasemaje kijana toka hapo kwashemej yako yasije kukukuta
 
Back
Top Bottom