Mtoto wa kiume hasa hasa graduate kamwe usikubali kuishi kwa shemeji yako ( mme wake na dada yako) ni laana

Kijana akiwa na kazi na pesa yake unadhani atalazimika kukaa kwa dada yake? Ukiona hivyo ujue sio kwa kupenda kwake, Bali maisha yanamlazimu. Tujifunze kuwaonea huruma na kuwapa moyo vijana wanaopambana kujitafuta, kama msaada hakuna basi angalau tusiwavunje mioyo.
 
kwa hiyo alikuwa alikuwa anakufanyia.......
 
Wengi wao hawapendi ila maisha yanawalazimisha sema hakuna shida ya kudumu
 
Maisha hayana kanuni moja!

Sio vizuri kufanya hitimisho kwa scenario moja!!

Kuna baadhi ya ndugu wa make huwa no majinga sana!!
 
Wengi wao hawapendi ila maisha yanawalazimisha sema hakuna shida ya kudumu
shida ni mindset kwamba ukisoma lazma uajiriwe,ila ukijitosa mtaani mbona kuna kazi za nguvu na watu tumepatia mitaji huko na maisha yanaenda....hata mimi ilinitesa japo sikuwahi kuishi kwa mtu,shida wasomi vijana hawatak kuanzia chini
 
 
Naungana na mleta mada
NB;Muda mwingine unakosa chaguo unalazimika kukaa
 
 
Afanye hata bodaboda siyo mbaya, boda wanathaminiwa sana na wake za watu ndo maana wanatunukiwa sana. Aache uzembe.
 
Hapa mzee umefanya kama vile kwenye maisha watu wote wanapitia similar situations. Ila basi
 
Hapa mzee umefanya kama vile kwenye maisha watu wote wanapitia similar situations. Ila basi
ninachopinga mimi ni mtu kukaa kwa shemeji huku hana effort yeyote kujikwamua wakat kuna vibarua mtaani na watu wanafanya wana family,wamepanga na wanasomesha plus kusaidia wazazi,sasa iweje wew kijana ukae,ule msosi wa shemeji,this is not right hasa kwa maisha ya sasa!...karibu %80 ya watu wameanzia chini na kukua!maisha ni magumu mkuu ila tusibweteke!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…