Habari wana jamvi!
Kwa heshima naomba tuufunge mjadala wa binti wa raisi!
Hakuna shaka kuwa Mkuu alikosea kuwaita wanafunzi wa UDOM vilaza! Achilia mbali wale wa UDOM hata waliobaki nyumbani kwa kupata div0! Mkuu wa familia abezi anguko ndani ya jamii yake Bali hutoa support kwa kila mwenye changamoto!
Ndani ya nyumba moja hata "mlevi mbwa" hifarijiwa, mwizi au jambazi Sugu akikamatwa hutembelewa mahabusu, sembuse aliyefeli shule! Haukuwa wito sahihi kwa Mkuu wa nchi!
Wote tunarejea makosa yaleyale kwa Jesca, kumbukeni naye dunia itamuelemea kwà makosa ya baba yake, atapoteza amani ktk dunia kwa dhambi tunazomlazimisha arithi!
Kwa wale wenye imani, mtakumbuka viongozi wa dini wengi walitoka ktk familia zenye matatizo lkn jamii haziku waadhibu kwa makosa ya familia zao!
Hebu jukwaa hili nalo liwe considerate, hebu great thinker kaeni muone mnamuumizaje Yule binti! Yes, kuna mabinti na vijana 7802 wanaumia equally lkn ktk hili jesca si aliyetukosea, yawezekana naye alilia na kujutia kauli ya baba yake kama sisi! kuna kila sababu ya kuchukizwa na aliyoyasema raisi lkn kama yupo anayeweza kumshambulia "baba Jesca" afanye hivyo atakuwa sahihi zaidi kuliko kumuumiza mtu innocent!!!, please JF tuachane na huyu binti..!
Viongozi wameelewa mno na watachukua hatua stahiki, lkn ifike point nasi tuone dhambi tunazofanya dhidi ya mtoto wa mwenzetu! Tuko wapi wale wa samehe 7*70!