Mtoto wa Magufuli (Jesca) sijui alifikaje Chuo Kikuu?

Mtoto wa Magufuli (Jesca) sijui alifikaje Chuo Kikuu?

Wewe akili zako ziko huko nyuma aisee!
Fanaya tafiti tena ndiyo urudi na pumba zako. Je kama alilisiti hiyo form four na kupata dalaja la kumuwezesha kusoma certificate to diploma then degree?? Au kama alilisti hiyo form four then akaenda form five na six then akafanya certificate then degreee?? Unajua nyie wengine akili zenu zimekaa kizembe kizembe. Mi kuna kijana namfahamu alipata zero kabisa akaristi akapata div four ya 28, then akaenda certificate then diploma sasa yupo degree. Ktk mazingira hayo ukiangalia ule mwaka aliofanya mtihani wa form IV mara ya kwanza utakuta ana zero, na hiyo scenario inaweza kuwa kwa huyo Jesca. Nitakuita kilaza mpaka utuletee ushahidi kuwa hajawahi kuristi.
 
Jesca Kilaza Magufuli.....

Hayo ndo madhara ya kutosoma hotuba.

Wewe hotuba ushaandikiwa lakini unakataa kuisoma na unaamua kuongea mambo bila mpangilio maalum wakati hauko mzungumzaji mzuri.

Matokeo yake unatumia lugha ya dhihaka ambayo inakuja kuathiri hata watu wa karibu yako.

Magufuli saa ingine huwa hana busara kabisa.
 
MASWALI "FIKIRISHI" vs MASWALI "CHOKONOZI.!"

By Malisa GJ,

Rafiki yangu Comrade Rashid Chilumba kaniuliza maswali yaliyonitoa jasho kidogo. Maswali ya kufikirisha.

Katika kuchangia hoja ya binti anayedhaniwa kuwa ni mtoto wa Rais Magufuli aitwae "Jesca John Magufuli" Comrade Chilumba ameniuliza maswali kadhaa na kunitaka niweke ushahidi (Evidence) wakati nikijibu maswal hayo.

Sehemu ya maswal hayo Chilumba anauliza, Je huyo binti anayetajwa kwa jina la Jesca Magufuli ni mtoto wa Rais Magufuli kweli au ni mfanano wa majina? Kuna ushahidi wowote kuwa Magufuli ana mtoto aitwae Jesca? Kama yupo, je ana uhusiano na Jesca anayetajwa kusoma St.Mathew's?

Anahoji Chilumba na kuendelea; Je Jesca aliyedahiliwa UDOM na yule wa St.Mathew's ni mtu mmoja? Je hayo matokeo yanayodaiwa kuwa ni ya Jesca sio editing? Kwanini picha ya matokeo inayotembea mtandaoni ni moja tu?

Nimeyapenda maswali haya ya Chilumba kwa sababu yamenifanya "nifikirie sana" na mimi napenda kufikiria (Thinking is my hobby).

Maswali ya Chilumba yana mantiki sana kwa sababu jibu lolote kati ya maswali hayo linaweza kubadilisha mijadala yote inayoendelea mitandaoni kuhusu Jesca.

Kwa mfano swali la kwanza la Chilumba majibu yake yakiwa ni HAPANA basi yote tunayojadili huku mtandaoni ni bure. Yani kama Magufuli hana mtoto aitwae Jesca basi tunapoteza muda kujadili mambo ambayo ni "dhahania"

Na ikiwa jibu la kwanza litakua HAPANA basi hata hayo maswali mengine yaliyobaki yanakuwa hayana maana (yanakufa naturally). Huo ndio utamu wa critical thinking.

Kwa hiyo nimpongeze Comrade Chilumba kwa maswali haya mazuri ambayo yamedhihirisha kwamba alikua hasinzii kwenye vipindi vya Critical Thinking vya mwalimu wake Crispin Isaboke.

#MAJIBU
Nimefanya utafiti kidogo na kupata majibu ya maswali ya ndugu Chilumba. Nami napenda kuyajibu kama ifuatavyo kwa kuambatanisha na evidence kama alivyohitaji;

1. #SwaliLaKwanza
Je Rais Magufuli ana mtoto aitwae Jesca John Magufuli?

#JIBU
Ndio. Jesca John Magufuli ni mtoto wa kuzaliwa wa Mhe.Rais John Magufuli na mkewe Janeth Magufuli. Rais Magufuli ana watoto 7. Watatu wa kiume na wanne wa kike.

#Evidence
Katika orodha ya kuzaliwa Jesca ni mtoto wa 4. Watoto wengine wa Rais Magufuli ni kama ifuatavyo;

1. Suzzan John Magufuli
2. Edna John Magufuli
3. Joseph John Magufuli
4. Jesca John Magufuli
5. Lucy John Magufuli
6. Jurgen John Magufuli
7. Jerry John Magufuli

#EvidenceNunber2
Tembelea anuani hii ya Ikulu kufahamu zaidi juu ya familia ya Rais Magufuli na familia yake, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Rais

2. #SwaliLaPili
Je Jesca ambaye ni mtoto wa Rais Magufuli amesoma sekondari ya St.Mathew kwa kipindi tajwa?

#JIBU
Ndio. Jesca John Magufuli binti wa Mheshimiwa Rais Magufuli amesoma sekondari ya St.Mathew na kuhitimu kidato cha 4 mwaka 2011.

#Evidence,
Mkurugenzi wa shule hiyo Bw.Thadeo Mutembei anaweza kudhibitisha hilo. Unaweza kumpigia kupitia simu yake nambari 0754 698845.

3. #SwaliLaTatu
Je, Jesca Magufuli aliyepata division four ya alama 30 ndiye huyo mtoto wa Rais Magufuli? (Au ni mwingine).

#JIBU
Ndiye huyo.

#Evidence;
Hakukuwa na Jesca Magufuli wawili katika sekondari ya St.Mathew.

4. #SwaliLaNne
Je matokeo yanayosambazwa mitandaoni kwamba ni ya Jesca ni matokeo halisi au ni photoshop?

#JIBU
Ni matokeo halisi, hakuna photoshop wala editing.

#Evidence
ingia kwenye website hii utaona matokeo yote ya sekondari ya St.Mathew's kwa mwaka 2012 na utaona jina la Jesca katika orodha hiyo. Nambari yake ya mtihani ilikua S.1071/102 http://196.44.162.33/necta2011/CSEE 2011/s1071.htm

#SwaliLaTano
Je ni kweli kuna mtu aitwae Jesca Magufuli alidahiliwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mwaka 2014 kusomea shahada (degree) ya biashara ktk Rasilimali watu?? (Bachelor of Commerce in Hunan Resource Management).??

#JIBU
Ndio. Mwaka 2014 miongoni mwa wanafunzi waliodahiliwa kujiunga na Cho Kikuu cha Dodoma ni binti mmoja aliyejulikana kwa jina la Jesca John Magufuli.

#Evidence
Ingia kwenye website hii kisha tafuta Admisdion number 230. Pitia hapa http://41.93.31.136:8080/Selections/UnderGraduate.jsp?InstCode=DM

6. #SwaliLaSita
Je, Jesca Magufuli aliyedahiliwa UDOM mwaka 2014 ndio yule Jesca aliyemaliza St.Mathew's mwaka 2011 ambaye ni mtoto wa Rais Magufuli.

#JIBU
Ndiyo. Jesca anayesoma UDOM ndiye Jesca yuleyule aliyemaliza kidato cha 4 mwaka 2011 sekondari ya St.Mathew ambaye pia ni mtoto wa Rais Magufuli.

#Evidence
Unaweza kumpigia Mkuu wa Chuo cha UDOM Prof.Idrisa Kikula kudhibitisha kama kweli Jesca Magufuli aliyepo chuoni hapo ndiye yule binti wa Mheshimiwa Rais Magufuli. Namba ya Prof.Kikula ni 078 455 5655.

#HITIMISHO
Comrade Chilumba nafikiri nimekujibu maswali yako yote kama ulivyoniuliza. Na nimejitahidi kukupa evidence kama ulivyonitaka kufanya hivyo.

Sasa nakuomba na wewe unisaidie vimaswali vyangu vidogo kama ifuatavyo;

1. Hivi ilikuaje Jesca akasoma degree wakati alipata Division four ya point 30?

2. Je ana foundation course yoyote labda Diploma? Kama anayo amesomea chuo gani? Na aliwezaje kupata diloma ndani ya miaka miwili? Ina maana hakusoma certificate?

3. Na ilikuaje Udahili wake wa UDOM ukapitia NACTE wakati muongozo wa NACTE wa mwaka 2005 unazuia vyuo vilivyopo chini yake kudahili wanafunzi wenye alama chini ya 28?? Yeye ana 30 alidahiliwaje?

4. Amewezaje kusoma Bachelor of Commerce wakati somo la Commerce alipata "F" kidato cha 4??

5. Kwanini Serikali ilipotimua wale "Vilaza" (Form four failures) waliokua wamejazana vyuo mbalimnali kikiwemo St.Joseph, mbona hawakushughulika na Jesca? Je yeye ana "immunity??"

6. Je kauli ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa JPM kwamba kuna watoto wa vigogo waliofeli form four wamejazana vyuo vikuu na kuziba nafasi kwa watoto wa maskini wenye sifa na vigezo, je haimlengi Jesca? Hasa ukizingatia kuwa yeye ndiye mtoto wa kigogo mkubwa zaidi nchini? (Mtoto wa Mheshimiwa zaidi). Kama haimlengi Jesca ilikua inalenga akina nani?

Tafadhali Comrade nisaidie majibu ya viswali vyangu hivyo hapo juu. Naamini viswali vyangu hivi sio vigumu kama maswali yako ya Critical Thinking.

Wasalaam,

Malisa Godlisten E.J
 
Amna kumuonea mtu huruma,upanga uliotumika kuwakata hao 7802 utumike kumkata uyu mmoja.Ni lazima apitie maumivu wenzake waliyopitia haijalishi ni mtoto wa nani.
Haki lazima itendeke na nasikia anapelekwa kwa gari chuo na ana ulinzi mkali.Kwahiyo kodi zetu zinatumika kumlinda na kumpeleka chuo wakati watoto wetu 7802 walifukuzwa kama mbwa bila kufikiria watafikaje makwao.
 
Watanzania tunapenda maneno matamu hata pale tunapofanya vibaya, hatutaki kuambiwa kweli. Mtu akifeli abembelezwe na kusema bahati mbaya. Vilaza wapo kweli na wanafunzi wenyewe wanaitana vilaza
Ndo maana pia watanzania kutumia JF wakaweka ukweli wa "UKILAZA" wa Huyo binti na kuhoji amefikaje mwaka wa pili na wala hawakuficha. Raisi na wafuasi wake pia wapende kuambiwa ukweli unapojidhihiri maana sasa jino kwa jino, mguu kwa mguu, jicho kwa jicho.
 
wakati mnataka mfunge mjadara wa jESCA, mimi nilitaka nilete ya mtt wake mwingine, ili kuonesha kuwa mganga hajigangi, na kauli aliyoitoa alikosea, ila jmani naomba muamini kuwa jamaa naskia hata kwnye familia yake ukifeli anakuita kilaza, tu na kunauwezekano akakufukuza.

malizeni wahuyo mkimaliza niambieni nilite wa mtt wake mwingine niliyesoma nae mcheke mpaka mapsuke mbavu. jamaaa alishindwa kurisisha kipaji cha kukalili kwa woto sjui kakiperekka wap?

teh teh.... hatari sana
 
Hapa ni suala la hesabu tu ndio utaelewa, chukua mwaka aliomaliza form four, plus mwaka wa kurisit, certificate, diploma na baadae mwaka aliodahiliwa UDOM utajua pumba ni ipi na mchele ni upi. Ni dhahiri umenipotezea muda wangu kujibu ambacho hakistahili kujibiwa but pole kwa kukupa kazi nzito japo naamini utakuwa umeelewa

Una huruma sana. Huyo hakutakiwa kujibiwa.
 
Naona UKAWA mmepata pa kupumulia. Rais Magufuli alikuwa sahihi kuwaita vilaza kwa vile mnaoneka a mmetekwa na mjadala wa vilaza
kilaza upo busy kujibu comment za vilaza.kilaza + vilaza= ma-vilaza
 
Story ya Juma KILAZA na Mbaraka Mwishehe....
-Juma KILAZA alijikuta ni fundi wa kupiga gitaa kuliko Mbaraka. Wakaandaliwa mchuano nani zaidi. Juma KILAZA alibagwa vibaya sana. Kuanzia hapo mtu asiyejua vitu akaanza kuitwa KILAZA. Na wakiwa weng waliitwa VILAZA.[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

-Kilaza lazima ajadiliwe maana siyo dhambi. Mbona wengine wameitwa na hakuna aliyejitokeza kuwatetea???

Wewe kama unamhurumia bhasi usichagie ila anayejisikia kusema chochote aseme.
 
samahani mkuu hivi ku resit ndo kurudia darasa ama ukiresit lazima uanzie form three?? kuna shule nazifaham hua wana utaratibu flan unasoma masomo ya form v huku unarisit form iv (siwezi kuzitaja) ukipata credit zako unaunganisha form six ila ukikosa unabakia form v huku ukiendelea kurisit ila unasoma kama private candidate.. best explanation kwa huyo dada labda atakua alitumia huo utaratibu akapata credit wakati huo huo tayari ameshasoma form five kwaiyo akaingia form six moja kwa moja akafanya mtihani kisha akasoma cheti kwa mwaka mmoja (labda ndo maana ikabid apitie NACTE badala ya TCU) ndo maana leo yupo second year chuo kikuu. kuhusu kusoma bcom inawezekana cheti alisomea mambo ayo ama alikisafisha cha form four baada ya kurisit.. kuna explanation nyingi sana za kwanini awe mwaka wa pili isipokua mi namshauri yeye ama watu wake wa karibu asijisumbue kujibu ama kuweka kumbukumbu sawa kuhusiana na huu "udaku" make hua ni adhabu nzuri sana kwa mpumbavu unapoamua kukaa kimya kama husikii anachoongea.. samahani kama nimevuka red lines za watu mniwie radhi
Mleta mada kamwaga ushahidi wa kutosha juu ya hoja yake.

Hebu na wewe tuwekee huo ushahidi wako.

1: hiyo shule aliyorisit inaitwajwe?

2: Je! Baada ya kurisit matokeo ya lineage?

Kama huna ushahidi zip ur mouth
 
moderators wana double standards. matokeo ya mbowe hawakutaka tujadili walifunga mjadala huu wanauacha ukiendelea kudhalilisha watu sio sawa kabisa.
 
adi baba ake aombe radhi kuwaita watoto wa wenzie vilaza wakat ata wake ni kilaza
 
Fanaya tafiti tena ndiyo urudi na pumba zako. Je kama alilisiti hiyo form four na kupata dalaja la kumuwezesha kusoma certificate to diploma then degree?? Au kama alilisti hiyo form four then akaenda form five na six then akafanya certificate then degreee?? Unajua nyie wengine akili zenu zimekaa kizembe kizembe. Mi kuna kijana namfahamu alipata zero kabisa akaristi akapata div four ya 28, then akaenda certificate then diploma sasa yupo degree. Ktk mazingira hayo ukiangalia ule mwaka aliofanya mtihani wa form IV mara ya kwanza utakuta ana zero, na hiyo scenario inaweza kuwa kwa huyo Jesca. Nitakuita kilaza mpaka utuletee ushahidi kuwa hajawahi kuristi.
Hatutaki majibu ya "kama", tuambie ali resit wapi, lini na kwa muda gani.

Ikiwa hujui kitu juu ya elimu ya Jesca bora kukaa kimya usome comment za wanaojua.
 
Back
Top Bottom