Mtoto wa Malecela Le Mutuz amvaa January Makamba na Tanesco yake

Mtoto wa Malecela Le Mutuz amvaa January Makamba na Tanesco yake

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Screenshot_20221126-090554_Instagram.jpg

Hapo juu ni ukurasa maalum wa mitandao ya kijamii wa mtoto wa Malecela ukiwatuhumu Viongozi hasa wahusikao na nishati ya umeme inayoongozwa na Makamba kwa kufanya mambo yasiyo na u-muhimu huku wakiacha Samia akisemwa kuhusu tatizo la mgao wa umeme.

'....unarushaje live mikutano ya mama ili hali umeme haupo sasa wananchi wake watamwona vipi?!' Amehoji Le Mutuz.
 
Mama yao aonewe huruma vipi wakati nae ameridhika kuwa na hao wasaidizi feki, hiyo pesa ya matangazo inayopotea aiache tu ipotee, ndio tozo zetu hizo tunazokatwa kwenye miamala ya simu kila siku.

Mimi naona Samia ndie hana huruma na wananchi anaowaongoza, kitendo cha wizara ya Nishati kuendelea kuongozwa na waziri aliyefeli, licha ya malalamiko yote ya kila siku, ni dharau kwa anaowaongoza, wacha aendelee kutukamua tozo ili zitumike kuonesha vile visivyoonekana.
 
Huyu aliyekuwa anaumwa moyo akaenda kutibiwa kwa ufadhili wa JPM .....sijui na yeye kawekewa kifaa Cha umeme wa moyo, hawa ndio wanasababisha mgao wa umeme
 
Najua JM ataandaa bahasha kumnyamazisha. Naye atanyamaza

Ahaaa!! Kumbe ukimsema tu unatumiwa bahasha?

Kwani shida ipo wapi mpaka anashindwa kurekebisha hapo Tanesco mambo yakawa sawa?

Na mbona mama anamwacha tu ni kwamba hana habari kuwa mtaani hamna umeme ama?

RC Dar kasema mvua zimenyesha na vyanzo vya maji vimerudi sawa na mgawo wa maji haupo tena? Ina maana hayo mabwawa yanakuwaga mvua yake special tu?

Watanzania siyo wajinga hata wakikaa kimya wanakuchora tu na upuuzi wako? Makamba wizara ilishakushinda hiyo tayari!! Je ukipewa nchi utaweza?

Tulikuwa na imani na wewe ila baada ya kupewa hii wizara imekuumbua hautoshei kwenye kiti cha Urais!! Sahau kabisa lile jambo lako!!
 
Huyo February ni Mkono wa Mwenye Enzi Mungu uingilie kati tu walahi [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Hata yeye pia let Mutuz haelewi bado nani anakata umeme na maji kwa na kwa nini, analaumu wasiohusika!
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Hapo juu ni ukurasa maalum wa mitandao ya kijamii wa mtoto wa Malecela ukiwatuhumu Viongozi hasa wahusikao na nishati ya umeme inayoongozwa na Makamba kwa kufanya mambo yasiyo na u-muhimu huku wakiacha Samia akisemwa kuhusu tatizo la mgao wa umeme.
Na yeye ni walewale ukoo wa panya
 
View attachment 2427760

Hapo juu ni ukurasa maalum wa mitandao ya kijamii wa mtoto wa Malecela ukiwatuhumu Viongozi hasa wahusikao na nishati ya umeme inayoongozwa na Makamba kwa kufanya mambo yasiyo na u-muhimu huku wakiacha Samia akisemwa kuhusu tatizo la mgao wa umeme.

'....unarushaje live mikutano ya mama ili hali umeme haupo sasa wananchi wake watamwona vipi?!' Amehoji Le Mutuz.

Le Kiba100z katika ubora wake
 
Back
Top Bottom