Mtoto wa Marehemu Kibonde aomba msaada wa Kisheria kuhusu mirathi ya baba yake

Mtoto wa Marehemu Kibonde aomba msaada wa Kisheria kuhusu mirathi ya baba yake

Mtoto wa marehemu Ephraim Kibonde aliyekuwa Mtangazaji wa Clouds FM, Hilda Kibonde amejitokeza mtandaoni akiomba kusaidiwa kwenye ishu ya mirathi inayoendelea katika familia yao tangu baba yake afariki miaka 7 sasa.

"Habari zenu Watanzania,

Ninakuja kwenu leo kwa sababu nimevumilia kwa miaka saba, na sasa nimefikia hatua ambayo nimeona ni muhimu kuomba msaada. Nimewaza na kufanya kila nilichoweza, lakini leo nimefika hapa.

Kama wengi mnavyofahamu, tulimpoteza Baba yetu, (Ephraim Samson Kibonde) tarehe 7/3/2019. Baada ya msiba, kikao kilifanyika na wasimamizi wa mirathi walichaguliwa (ambao walikuwa wamevuka umri wa miaka 18), na kesi ya mirathi ilifunguliwa katika Mahakama iliyopo Temeke.

Hata hivyo, tangu kipindi hicho kumekuwa na uzembe ambao umeleta maumivu makubwa kwangu na kwa mdogo wangu. Inauma sana kuona kwamba kuna watu wanaamua kupuuza suala hili kwa makusudi, labda kwa sababu haliwanufaishi wao moja kwa moja au kwa kiwango wanachotaka. Au pengine kwa sababu mimi ni mtoto wa kike na bado ni mdogo, hivyo sipatiwi uzito ninaostahili.

Kwa muda wote huu nimekuwa nikijitahidi kusemea mema kwa kila mtu, huku sisi tunaoumia na wenye uhitaji tukibeba maumivu yetu kimya kimya. Mpaka leo hii nimekuwa nikiomba taarifa muhimu kama namba ya kesi (case number)bila mafanikio, hali ambayo imenifanya hata kujiuliza kama nina haki ya kujua au kama sistahili kupata taarifa hizo za msingi.

Mimi ni binti ambaye bado najitafuta kwa ajili yangu na mdogo wangu, ambaye kwa sasa bado ni tegemezi. Inauma sana kuishi katika hali hii wakati Baba yetu mzazi aliacha vitu ambavyo vilipaswa kutusaidia katika masomo yetu, maisha yetu ya baadaye, makazi na mahitaji yetu ya msingi.

Mimi ni binti mdogo tu ambaye jambo hili limekuwa zito sana kwangu, na kwa sasa naomba msaada kutoka kwa yeyote anayeweza kusaidia iwe ni msaada wa kisheria, mtu binafsi, au mashirika ili kuweza kufikia suluhisho la changamoto hii.

Nina imani kwamba Mahakama za Tanzania na Serikali kwa ujumla zinataka wananchi wapate haki zao za kisheria. Natumaini ujumbe huu utawafikia watu husika na kutuwezesha kupata msaada, suluhisho na haki tunayostahiki.

Ahsanteni Sana.🙏" - ameandika Hilda.
Nisaidieni kum tag yule waziri machachari Dorothy Gwajima.
Joseph ameshindwa kutoa msaada, hapo ndipo Ruge(RIP) angechukua points zote kama angekuwa hai, angetumia connections jambo lingemalizwa fasta.
Wale tulio na watoto wa like tuwe makini sana, huwa wanateseka sana pale wanapobaki bila ya wazazi.
 
Back
Top Bottom