Mtoto wa Marehemu Kibonde aomba msaada wa Kisheria kuhusu mirathi ya baba yake

Mtoto wa Marehemu Kibonde aomba msaada wa Kisheria kuhusu mirathi ya baba yake

Mtoto wa marehemu Ephraim Kibonde aliyekuwa Mtangazaji wa Clouds FM, Hilda Kibonde amejitokeza mtandaoni akiomba kusaidiwa kwenye ishu ya mirathi inayoendelea katika familia yao tangu baba yake afariki miaka 7 sasa.

"Habari zenu Watanzania,

Ninakuja kwenu leo kwa sababu nimevumilia kwa miaka saba, na sasa nimefikia hatua ambayo nimeona ni muhimu kuomba msaada. Nimewaza na kufanya kila nilichoweza, lakini leo nimefika hapa.

Kama wengi mnavyofahamu, tulimpoteza Baba yetu, (Ephraim Samson Kibonde) tarehe 7/3/2019. Baada ya msiba, kikao kilifanyika na wasimamizi wa mirathi walichaguliwa (ambao walikuwa wamevuka umri wa miaka 18), na kesi ya mirathi ilifunguliwa katika Mahakama iliyopo Temeke.

Hata hivyo, tangu kipindi hicho kumekuwa na uzembe ambao umeleta maumivu makubwa kwangu na kwa mdogo wangu. Inauma sana kuona kwamba kuna watu wanaamua kupuuza suala hili kwa makusudi, labda kwa sababu haliwanufaishi wao moja kwa moja au kwa kiwango wanachotaka. Au pengine kwa sababu mimi ni mtoto wa kike na bado ni mdogo, hivyo sipatiwi uzito ninaostahili.

Kwa muda wote huu nimekuwa nikijitahidi kusemea mema kwa kila mtu, huku sisi tunaoumia na wenye uhitaji tukibeba maumivu yetu kimya kimya. Mpaka leo hii nimekuwa nikiomba taarifa muhimu kama namba ya kesi (case number)bila mafanikio, hali ambayo imenifanya hata kujiuliza kama nina haki ya kujua au kama sistahili kupata taarifa hizo za msingi.

Mimi ni binti ambaye bado najitafuta kwa ajili yangu na mdogo wangu, ambaye kwa sasa bado ni tegemezi. Inauma sana kuishi katika hali hii wakati Baba yetu mzazi aliacha vitu ambavyo vilipaswa kutusaidia katika masomo yetu, maisha yetu ya baadaye, makazi na mahitaji yetu ya msingi.

Mimi ni binti mdogo tu ambaye jambo hili limekuwa zito sana kwangu, na kwa sasa naomba msaada kutoka kwa yeyote anayeweza kusaidia iwe ni msaada wa kisheria, mtu binafsi, au mashirika ili kuweza kufikia suluhisho la changamoto hii.

Nina imani kwamba Mahakama za Tanzania na Serikali kwa ujumla zinataka wananchi wapate haki zao za kisheria. Natumaini ujumbe huu utawafikia watu husika na kutuwezesha kupata msaada, suluhisho na haki tunayostahiki.

View attachment 3615023

Ahsanteni Sana.🙏" - ameandika Hilda.
Nisaidieni kum tag yule waziri machachari Dorothy Gwajima.
Dorothy Gwajima yupo humu na ataweza kusoma
 
Aliacha wosia wa kughushi ndo maana mambo hayajaisha bado yeye na Mercy hawakufikia final settlement ya 35% ya mgao wa mali kwahiyo kukawa na ttzo kwenye kesi iliyotokea
Aliyefanya hivyo ni yule Jackline kushurikiana na shoddy lawyer.
Walifanya makusudi kubadilisha wosia wakijua marehemu hayupo sawa kiafya.
 
Aliyefanya hivyo ni yule Jackline kushurikiana na shoddy lawyer.
Walifanya makusudi kubadilisha wosia wakijua marehemu hayupo sawa kiafya.
Na mahakama iliweza kutupilia mbali wosia ule, licha ya kukata rufaa japo aliomba mahakama iwape muda wa marejeo kwenye maamuzi ya mahakama kuu hivyo sijajua wamefikia wapi naona bado bila bila

Maake nadhani mwaka Jana aalishusha waraka huko Instagram kwa mama samia akiomba iwasaifie wajane na mayatima wanaodhulumiwa haki zao aliweka general hakuwa specific sjui aliogopa nn 🤔

Nadhani alitambulika mke wa late Reg ni issue ya kukaa chini na familia wafanye settlement sasa yeye akitaka achukue yote huo ni uwongo

kwa kuwatoa watoto wengine wa marehemu bila sababu,

Na mali za mtalaka wa mengi kujumuishwa kuwa ni za kwakwe hapo bibiye alichemka kama mharage

Afu wanasheria aseeh wanamlia tuu hela daaah atafika amechoka
 
Ana kijana mkubwa ndio first born, ila ni kwa mama tofauti na hawa wadogo. Na huyo first born ndie anaeleta vikwazo sasa.
1. Mtu anadai haki yake utasemaje analeta vikwazo ??? i ???

2 Wanaolwamisha kesi ni mahakimu corrupt and incompetent, hawajui sheria nahawako accountable.

Mirathi haiendeahwi na
hiari za warithi Vkwazo vya mrithi havina nafasi au nguvu ya hasimamisha na kuua kesi isiendelee.

Hakuna requirement kwamba mkubaliane ndo uamuzi wa mahaka utoke.

Shauri linakwama pale mahakama inapowaambia rudini mkakubaliane mgao ndo mje tena.

SHERIA YA MIRATHI KAMA ZILIVYO NYINGINE ZOTE ZA COMMON LAW, NI ADVERSARIAL PROCESS.

MAHAKAMA INATEGEMEA WATU WASIKUBALIANE, NA INAPASWA KUTOA MAAMUZI HIVYO HIVYO
 
Ina maana kibonde kwa umri ule hakuwa na mtoto alievuka miaka 18!?
Kama alikuwa nae wa kiume, huyo ndie mrithi halali!

kwetu wakurya..., binti hana URITHI! kwa baba wala mama yake!, URITHI WA BINTI UKO KWA MUMEWE! HUKO ATAKAKO-OLEWA!

PERIOD!.
Na asipoolewa inakuaje, au kafiwa kabla ya kuolewa utaratibu ukoje?
 
Na mahakama iliweza kutupilia mbali wosia ule, licha ya kukata rufaa japo aliomba mahakama iwape muda wa marejeo kwenye maamuzi ya mahakama kuu hivyo sijajua wamefikia wapi naona bado bila bila

Maake nadhani mwaka Jana aalishusha waraka huko Instagram kwa mama samia akiomba iwasaifie wajane na mayatima wanaodhulumiwa haki zao aliweka general hakuwa specific sjui aliogopa nn 🤔

Nadhani alitambulika mke wa late Reg ni issue ya kukaa chini na familia wafanye settlement sasa yeye akitaka achukue yote huo ni uwongo

kwa kuwatoa watoto wengine wa marehemu bila sababu,

Na mali za mtalaka wa mengi kujumuishwa kuwa ni za kwakwe hapo bibiye alichemka kama mharage

Afu wanasheria aseeh wanamlia tuu hela daaah atafika amechoka
Ile kesi haitibiki tena kisheria, imeshakufa kifo cha mende.
 
1. Mtu anadai haki yake utasemaje analeta vikwazo ??? i ???

2 Wanaolwamisha kesi ni mahakimu corrupt and incompetent, hawajui sheria nahawako accountable.

Mirathi haiendeahwi na
hiari za warithi Vkwazo vya mrithi havina nafasi au nguvu ya hasimamisha na kuua kesi isiendelee.

Hakuna requirement kwamba mkubaliane ndo uamuzi wa mahaka utoke.

Shauri linakwama pale mahakama inapowaambia rudini mkakubaliane mgao ndo mje tena.

SHERIA YA MIRATHI KAMA ZILIVYO NYINGINE ZOTE ZA COMMON LAW, NI ADVERSARIAL PROCESS.

MAHAKAMA INATEGEMEA WATU WASIKUBALIANE, NA INAPASWA KUTOA MAAMUZI HIVYO HIVYO
Chanzo ni wazazi, hasa Kibonde hakufanya estate planning akiwa hai.

To plan your estate while alive is to die responsibly.
 
Jamii zetu hizi za kimaskini za kipuuzi sana.

Hao wasimamizi wa mirathi wanajua kabisa hao bado wadogo, wana mahitaji lakini wanaamua kunyamaza makusudi.

Hivi mtoto kajitokeza hadharani, wataanza kumpigia simu wamdanganye na maneno matamu asiwe na wasiwasi, then baada ya hapo watakaa kimya tena. Miaka saba ni mingi sana.

Naamini mashirika ya kisheria, hasa NGO's the likes of LHRC watajitokeza kuwasaidia hawa watoto wapate haki zao.
Ni sahihi kabisa. Sema huyu binti nae ameshindwa vipi kufika ofisi za msaada wa sheria hapohapo Mahakama ya familia Temeke, wangemsaidia kupata namba ya kesi. Au hata masjala tu, angetaja jina la baba yake, wangepata namba ya kesi
 
Unampa mtu mali yako kama zawadi na inasajiliwa kwa jina lake unayempa

Kuna Mazingira mawili.

1. Kumzawadiwa mtu mali yako pindi upo hai ( GIFT INTERVIVOS). Hapa mtu anapata chake pindi wewe upo hai, unatumia DEED OF GIFT kufanya uhamisho wa umiliki wa mali unayotaka umpe mtu kama zawadi. Nyie wenye michepuko na watoto wa nje, hii njia inawafaa sana.

2. Kutoa zawadi ya mali pindi ukiwa hai lakini unaona unakaribia kufa na hivyo, hii njia inafanya kazi ukiwa umefariki immediately ( GIFT IN CAUSA MORTIS)
Yaani unaona una ugonjwa ambao hutoboi wiki, miezi au mwaka unakufa. So, unaandaa DEED OF GIFT kufanya uhawamisho wa umiliki wa mali zako na uhamisho wa mali unafanya kazi tu pale utakapo kufa, usipokufa mali zinabaki zako na ukifa tu, muda ule ule mali zinaenda kwa mtu uliyempa zawadi kwa masharti tu ukiwa umekufa ndio ziwe zake.
Kweli elimu bahari, mkuu muwe mnatupatia hizi elimu tuwe wateja wenu, migogoro kama hii itapungua
 
Back
Top Bottom