Mtoto wa Marehemu Kibonde aomba msaada wa Kisheria kuhusu mirathi ya baba yake

Mtoto wa Marehemu Kibonde aomba msaada wa Kisheria kuhusu mirathi ya baba yake

Comrade nadhani unazijuwa familia zetu za Kiswahili zikishajuwa kuwa kuna jambo litakunufaisha mbeleni lazima wawe na roho za korosho. Ukiona mpaka binti ameamuwa kutafuta msaada kwa umma basi ujuwe hali ni tete sana.
Anakwensa kwenyen ofisi za wakili, wanaandika mkataba , kwamba fedha za miradhi zikitoka , basi walau hata milioni 5 alipwe wakili?
Mbona dalali anadai kodi ya mwezi na hakuna anayelalamika?
 
Mtoto wa marehemu Ephraim Kibonde aliyekuwa Mtangazaji wa Clouds FM, Hilda Kibonde amejitokeza mtandaoni akiomba kusaidiwa kwenye ishu ya mirathi inayoendelea katika familia yao tangu baba yake afariki miaka 7 sasa.

"Habari zenu Watanzania,

Ninakuja kwenu leo kwa sababu nimevumilia kwa miaka saba, na sasa nimefikia hatua ambayo nimeona ni muhimu kuomba msaada. Nimewaza na kufanya kila nilichoweza, lakini leo nimefika hapa.

Kama wengi mnavyofahamu, tulimpoteza Baba yetu, (Ephraim Samson Kibonde) tarehe 7/3/2019. Baada ya msiba, kikao kilifanyika na wasimamizi wa mirathi walichaguliwa (ambao walikuwa wamevuka umri wa miaka 18), na kesi ya mirathi ilifunguliwa katika Mahakama iliyopo Temeke.

Hata hivyo, tangu kipindi hicho kumekuwa na uzembe ambao umeleta maumivu makubwa kwangu na kwa mdogo wangu. Inauma sana kuona kwamba kuna watu wanaamua kupuuza suala hili kwa makusudi, labda kwa sababu haliwanufaishi wao moja kwa moja au kwa kiwango wanachotaka. Au pengine kwa sababu mimi ni mtoto wa kike na bado ni mdogo, hivyo sipatiwi uzito ninaostahili.

Kwa muda wote huu nimekuwa nikijitahidi kusemea mema kwa kila mtu, huku sisi tunaoumia na wenye uhitaji tukibeba maumivu yetu kimya kimya. Mpaka leo hii nimekuwa nikiomba taarifa muhimu kama namba ya kesi (case number)bila mafanikio, hali ambayo imenifanya hata kujiuliza kama nina haki ya kujua au kama sistahili kupata taarifa hizo za msingi.

Mimi ni binti ambaye bado najitafuta kwa ajili yangu na mdogo wangu, ambaye kwa sasa bado ni tegemezi. Inauma sana kuishi katika hali hii wakati Baba yetu mzazi aliacha vitu ambavyo vilipaswa kutusaidia katika masomo yetu, maisha yetu ya baadaye, makazi na mahitaji yetu ya msingi.

Mimi ni binti mdogo tu ambaye jambo hili limekuwa zito sana kwangu, na kwa sasa naomba msaada kutoka kwa yeyote anayeweza kusaidia iwe ni msaada wa kisheria, mtu binafsi, au mashirika ili kuweza kufikia suluhisho la changamoto hii.

Nina imani kwamba Mahakama za Tanzania na Serikali kwa ujumla zinataka wananchi wapate haki zao za kisheria. Natumaini ujumbe huu utawafikia watu husika na kutuwezesha kupata msaada, suluhisho na haki tunayostahiki.

View attachment 3615023

Ahsanteni Sana.🙏" - ameandika Hilda.
Nisaidieni kum tag yule waziri machachari Dorothy Gwajima.

Nimesoma makala yote lakini ni kama sijaona anahitaji msaada upi...

1. Amedhulumiwa mali za baba yake?
2. Amefikia umri kisheria unaompa uhalali wa kusimamia mali za baba yake?
 
Hii nina experience nayo Kuns Mzee nilikuwa namfahamu aliandika wosia akagawa mali vizuri ila kuna watoto wakubwa kama watatu aliwatoa nje alikuwa na bifu nao akawa treat kama sio watoto wake.

Hilo balaa lake baada ya kufa ni noma wale watatu waliufanya ule wosia kukosa maana.
Hii kitu ilishawahai kutokea kwa jamaa zangu wa karibu, walijidai kichwa ngumu wakati mzee wao akiwa mgonjwa matokea yake wakapishana na Wosia halafu wao ndio watoto wakubwa.
 
Pia inaweza isisaidie. Kwani Marehemu Mengi si aliacha wosia na kila kitu. Ila bado pakachimbika.
Mkuu angusha uzi wa haya mambo Deed of Gift ikoje kwa mfano
Unampa mtu mali yako kama zawadi na inasajiliwa kwa jina lake unayempa

Kuna Mazingira mawili.

1. Kumzawadiwa mtu mali yako pindi upo hai ( GIFT INTERVIVOS). Hapa mtu anapata chake pindi wewe upo hai, unatumia DEED OF GIFT kufanya uhamisho wa umiliki wa mali unayotaka umpe mtu kama zawadi. Nyie wenye michepuko na watoto wa nje, hii njia inawafaa sana.

2. Kutoa zawadi ya mali pindi ukiwa hai lakini unaona unakaribia kufa na hivyo, hii njia inafanya kazi ukiwa umefariki immediately ( GIFT IN CAUSA MORTIS)
Yaani unaona una ugonjwa ambao hutoboi wiki, miezi au mwaka unakufa. So, unaandaa DEED OF GIFT kufanya uhawamisho wa umiliki wa mali zako na uhamisho wa mali unafanya kazi tu pale utakapo kufa, usipokufa mali zinabaki zako na ukifa tu, muda ule ule mali zinaenda kwa mtu uliyempa zawadi kwa masharti tu ukiwa umekufa ndio ziwe zake.
 
Kwa nini suala la mirathi kwa watu weusi ni Tatizo hivi Tanzania??

Mbona huwa hatuwasikii Wahindi na Waarabu wakigombania mirathi?
Nani kakudanganya wanagombania mirathi kama wengine tu
 
Ukute ana watoto wengine Kwa mwanamke mwingine, hapo ndio Ngoma inazidi kuwa mbichi maana documents lazima tu ndio zitakazoleta utata...

Watoto wa mwanamke mwingine, Mawifi na ndugu wa mume plus wajomba, Haya makundi manne ndio sumu ya mirathi Kwa watoto wako utakaowaachia urithi, ukiwa uko Hai haya makundi yote unaona hawana shida, siku ukifa kundi moja ndo hapo ndo litaanza tabu, mbaya zaidi ww ndo ulikuwa Una afadhali kiuchumi, watagawana Hadi vijiko...

Haya mambo usichukulie rahisi hata kidogo, wamatumbi mambo yako ukiyaweka Kwa kuficha ficha ndo unazidi kuharibu...Chunga Sana mambo ya kuzaa zaa hovyo na wanawake tofauti kama Panya...
 
Mifumo yetu haipo wazi na inaendeshwa Kwa Connection na kujuana Sana. Wenzetu Ulaya mambo yako wazi na Sheria zinafuatwa na hata legal challenges zinakwenda Kwa uwazi na utaratibu unaohitajika, so ukiwa umatumbini lazima uwe makini kwaajili ya future ya wanao...

Watz wa kiasia mambo ya mirathi wanamalizana kifamilia vizuri tu incase ikitokea sintofahamu coz ukoo mzima hauna shida ndogondogo halafu mfano kuna wale wahindi (bohora) baadhi Yao wanakatiana urithi kabisa ukioa au kuolewa Tu ili Kila mtu akafie mbele na chake,sasa njaa zinakuja pale ambapo ww na ndugu zako umewapiga gepu kubwa, wenzio ni maskini wa kutupwa kabisa lazima Tu kitawaka dadeki...
 
Ukute ana watoto wengine Kwa mwanamke mwingine, hapo ndio Ngoma inazidi kuwa mbichi maana documents lazima tu ndio zitakazoleta utata...

Watoto wa mwanamke mwingine, Mawifi na ndugu wa mume plus wajomba, Haya makundi manne ndio sumu ya mirathi Kwa watoto wako utakaowaachia urithi, ukiwa uko Hai haya makundi yote unaona hawana shida, siku ukifa kundi moja ndo hapo ndo litaanza tabu, mbaya zaidi ww ndo ulikuwa Una afadhali kiuchumi, watagawana Hadi vijiko...

Haya mambo usichukulie rahisi hata kidogo, wamatumbi mambo yako ukiyaweka Kwa kuficha ficha ndo unazidi kuharibu...Chunga Sana mambo ya kuzaa zaa hovyo na wanawake tofauti kama Panya...
Actually, anaeleta hiyo mizengwe kwenye hii ishu ni msimamizi wa mirathi, ambae ndo kaka yao mkubwa, first born wa Kibonde, ila ni wa mama mwingine huyo. Ndo mziki ulipo.
 
Unampa mtu mali yako kama zawadi na inasajiliwa kwa jina lake unayempa

Kuna Mazingira mawili.

1. Kumzawadiwa mtu mali yako pindi upo hai ( GIFT INTERVIVOS). Hapa mtu anapata chake pindi wewe upo hai, unatumia DEED OF GIFT kufanya uhamisho wa umiliki wa mali unayotaka umpe mtu kama zawadi. Nyie wenye michepuko na watoto wa nje, hii njia inawafaa sana.

2. Kutoa zawadi ya mali pindi ukiwa hai lakini unaona unakaribia kufa na hivyo, hii njia inafanya kazi ukiwa umefariki immediately ( GIFT IN CAUSA MORTIS)
Yaani unaona una ugonjwa ambao hutoboi wiki, miezi au mwaka unakufa. So, unaandaa DEED OF GIFT kufanya uhawamisho wa umiliki wa mali zako na uhamisho wa mali unafanya kazi tu pale utakapo kufa, usipokufa mali zinabaki zako na ukifa tu, muda ule ule mali zinaenda kwa mtu uliyempa zawadi kwa masharti tu ukiwa umekufa ndio ziwe zake.
Bado wanaweza kui challenge kwa court (see screenshot), hasa kama uli exclude baadhi ya warithk wako kwenye hiyo gift. Au AI kanipotosha?
 

Attachments

  • WA_1782415703142.jpeg
    WA_1782415703142.jpeg
    123.2 KB · Views: 14
Bado wanaweza kui challenge kwa court (see screenshot), hasa kama uli exclude baadhi ya warithk wako kwenye hiyo gift. Au AI kanipotosha?
Sio kweli, zawadi unampa utakaye. Wosia ndio unaweza ku challenge uki exclude legal heirs bila sababu za msingi.
NB: AI sometimes anapotosha sana hususani kwenye mambo yenye kuhitaji TAALUMA.
Find a lawyer for estate planning
 
Back
Top Bottom