Hivi zile namba za kuripoti mtoto akifanyishwa kazi kwa umri mdogo ni ngapi?
Kwa Tanzania sidhani kama bado znatumika labda za USA zitapatikana
Hivi zile namba za kuripoti mtoto akifanyishwa kazi kwa umri mdogo ni ngapi?
Hata bila kumpiga, that’s illegal child labor!Mtoto anayefahamika kwa jina la Nikson (13), ambaye alikuwa akifanya kazi katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, ameripotiwa kupata majeraha makubwa baada ya kile kinachodaiwa kuwa kipigo kutoka kwa mwajiri wake.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, mtoto huyo alikuwa akiomba arejeshwe kwao Makambako akieleza kuwa amekuwa akikumbana na manyanyaso ya mara kwa mara akiwa kazini.
Inadaiwa kuwa kabla ya ombi lake kutekelezwa, alishambuliwa na kujeruhiwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo uso, mgongo na mikono.
Nikson amedai kuwa tukio hilo si la kwanza kutokea, bali amekuwa akipata vipigo mara kwa mara wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.
Tukio hilo limeibua maswali kuhusu usalama na ustawi wa watoto wanaofanya kazi katika mazingira mbalimbali ya mijini, pamoja na umuhimu wa kulindwa dhidi ya ukatili na unyanyasaji.
Mamlaka husika zinatarajiwa kufuatilia na kuchunguza madai hayo ili kubaini ukweli wa tukio na kuchukua hatua stahiki endapo yatathibitika.
View attachment 3612485
Maelezo mengi lakini hata kueleza Tu alikuwa akifanyishwa kazi gani haifahamiki? Hit to the point acheni siasaMtoto anayefahamika kwa jina la Nikson (13), ambaye alikuwa akifanya kazi katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, ameripotiwa kupata majeraha makubwa baada ya kile kinachodaiwa kuwa kipigo kutoka kwa mwajiri wake.