Mtoto wa miaka mitatu aliwa na fisi Mwanza wakati akienda kuoga kwenye dimbwi

Mtoto wa miaka mitatu aliwa na fisi Mwanza wakati akienda kuoga kwenye dimbwi

Ukiua/ukigonga fisi unapewa uhujumu uchumi

Ukiuwawa/ukiliwa na fisi unapewa pole na kuzikwa kwa gharama za serikali [emoji26]
 
Dah ,kama Mzazi inaumiza sana kwa tukio kama hili..Mola awajalie nguvu na subira katika kipindi hiki kigumu
 
#HABARI Mtoto Emanuel Marco Nyagela mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa Kijiji cha Mwangika kata ya Mwabomba wilayani Kwimba mkoani Mwanza amefariki dunia baada ya kuliwa na fisi wakati akienda kuoga kwenye dimbwi akiwa na wenzake

Tukio hilo jana Desemba 27/2022 saa 12 jioni kijijini hapo baada ya mtoto huyo kunyakuliwa na Fisi na kutokomea nae kuelekea msituni

Baba wa mtoto huyo aitwaye Marco Nyangela amesema alisikia yowe kutoka kwa wanakijiji wakisema mtoto wake ameliwa na fisi ndipo wakaanza kumsaka mtoto huyo na kuishia kuona damu zikiwa zimetapakaa kuelekea kwenye msitu huo

Hadi kufikia leo Desemba 28/2022 asubuhi wamefanikiwa kuona nguo alizokuwa amevaa mtoto huyo, fuvu la kichwa, ubongo pamoja na meno mawili

Germanus Masala ni mwenyekiti wa kijiji hicho na Amede Ssteness àmbae ni diwani wa kata ya Mwabomba wamesema wataendelea kushirikiana na wanakijiji kuwasaka fisi hao huku wakiwataka wazazi kuwa makini na watoto wao hasa nyakati za usiku #EastAfricaTV
 
Kuna mkanganyiko wa title hapa
 

Attachments

  • SmartSelect_20221229-091135_Chrome.jpg
    SmartSelect_20221229-091135_Chrome.jpg
    21.1 KB · Views: 2
  • SmartSelect_20221229-091123_Chrome.jpg
    SmartSelect_20221229-091123_Chrome.jpg
    36.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom