Mtoto wa miezi 2 analia mpaka napata wasiwasi na maziwa hataki kunyonya na nipo mbali na hospitali tatizo linaweza kuwa ni kwa wenye udhoefu wa watoto

Mtoto wa miezi 2 analia mpaka napata wasiwasi na maziwa hataki kunyonya na nipo mbali na hospitali tatizo linaweza kuwa ni kwa wenye udhoefu wa watoto

Kizinga mpemba

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2018
Posts
218
Reaction score
194
Msaada wa haraka mtoto wa miezi 2 analia mpaka napata wasiwasi tatizo linaweza kuwa nini mbaya zaidi maziwa hataki kunyonya.

Kuwa ni kwa wenye udhoefu wa watoto
 
Msaada wa haraka mtoto wa miezi 2 analia mpaka napata wasiwasi tatizo linaweza kuwa nini mbaya zaidi maziwa hataki kunyonya
Kulia sana kwa mtoto wa umri huo ni ishara kwamba maziwa anayonyonya kutoka kwa mama yake hayamtoshi au hayana virutubisho vyote anavyovihitaji mtoto.

Kwa maneno machache ni kuwa hashibi huyo! Jitahidi upate maziwa ya kopo umuanzishie sambamba na maziwa machache ya mama.
 
Kulia sana kwa mtoto wa umri huo ni ishara kwamba maziwa anayonyonya kutoka kwa mama yake hayamtoshi au hayana virutubisho vyote anavyovihitaji mtoto. Kwa maneno machache ni kuwa hashibi huyo!... Jitahidi upate maziwa ya kopo umuanzishie sambamba na maziwa machache ya mama.
maziwa ya mama yanajitosheleza kila kitu anyonye hayohayo ata maji asipewe wala kupondewa makande
 
maziwa ya mama yanajitosheleza kila kitu anyonye hayohayo ata maji asipewe wala kupondewa makande
Asilimia 70 ya mwili wa binadamu ni maji!.. Hata mtoto aliyezaliwa jana ni sharti apewe maji. Maziwa unaweza kuyaona yakitiririka lakini yasiwe na virutubisho vinavyotakiwa, na hasa kama afya ya mzazi haiko vizuri.... Usikariri tu meku!.
 
Jitahidi umfikishe hospitali, lkn katika hali ya dharura, jitahidi yawezekana mtoto hashibi muongezee kitu kingine.

Waweza hata kumkorogea uji mwepesi yaani ule unga unauchekecha uwe laini kisha unaufanya uji mwepesi.

Kama unahisi ni maumivu ya tumbo, jaribu kumpa maji kidogo ya vuguvugu uliochanganya na sukari kidogo na chumvi kidogo.
 
Mresho naona ni tumbo maana nimempa maji ya uvuguvugu yalichangwanya na chumvi na sukari kama memba alishauri kanyamaza na usingizi juu
 
Mchunguze kitovu, sikuhiz limekuwa tatizo Sana, unajua kapona kumbe bado anaumia
 
Asilimia 70 ya mwili wa binadamu ni maji!.. Hata mtoto aliyezaliwa jana ni sharti apewe maji. Maziwa unaweza kuyaona yakitiririka lakini yasiwe na virutubisho vinavyotakiwa, na hasa kama afya ya mzazi haiko vizuri.... Usikariri tu meku!.
Acha upotoshaji. Maziwa ya mama yanajitosheleza kwa miezi sita ya mwanzo Yana Maji na virutubisho vyote vinavyotakiwa kwenye ukuaji wa mtoto.
 
Hilo litakuwa tumbo la watoto wachanga Kitaalamu inaitwa colic.

Hutokea watoto wengi, Hali hiyo haina dawa ya kutibu ila vitulizo tu Kama grip water.

Hakikisha Kila baada ya kumnyonyesha unambeulisha kwa kumuweka begani halafu unamsugua mgongo Hadi abeue kuto Ile gas iliyoingia wakati ananyonya.Sababu gas nayo huchangia tumbo la uchanga kuuma

Tumbo la uchanga Huisha yenyewe mtoto akifikisha miezi mitatu. Pole ndo umama
 
Labda wewe ni chadema, na Mungu hampendi Tundu Lisu, who knows?
 
Ni kweli hospitali wanashauri asipewe chochote zaidi ya maziwa ya mama mpaka miezi sita.

Hata mimi mwanangu alikua na hili swala. Mama akaniambia huyo mtoti hashibi, kwahiyo wewe koroga uji mwepesi uwe unampa.

Nikamuambia mama mtoto kwahiyo dogo akaanza kunywa uji akiwa na miezi 2. Leo hii ana mwaka na miezi 4.

Yuko poa. Nampenda, I guess na yeye ananipenda coz hata akiwa wapi akisikia sauti yangu ataniita na kutaka nimbebe.
 
Msaada wa haraka mtoto wa miezi 2 analia mpaka napata wasiwasi tatizo linaweza kuwa nini mbaya zaidi maziwa hataki kunyonya
1. Anza na kumwona daktari wa watoto. Kama huna bima ya kwenda hospitali kama Regency na unaweza kulipia matibabu ya kuanzia Sh50,000 (au Sh70,000/-) unaweza pia kwenda hospitali kama Tikaya (Buyuni, Chanika), Agha Kan Polyclinic (kama uko maeneo ya Tabata au Banana (maana wana tawi pale karibu na Kituo cha Daladala cha Majumba Sita) Usikimbilie maziwa ya kopo (unless kama mfuko uko vizuri sana), ila kiafa pia siyo mazuri. Hizo ni hospitali za binafsi, unaweza kwenda za serikali pia.

2. Hakikisha mama anakula vizuri (balance diet ya kutosha).

3. Unaweza kuongeza uji wa ulezi, uji wa mbegu za maboga na ndizi za mtoli (mchanganyiko wa ndizi na nyama au sumu).

4. Hakikisha pia hana tatizo lingine kiafya.
 
Labda wewe ni chadema, na Mungu hampendi Tundu Lisu, who knows?
You're insane, upo so obsessed na Lisu hata kujadili hoja za maana unashindwa.

Mungu hampendi Lisu? Anakupenda wewe au? What an imbecile!
 
Labda maziwa hayatoshi mpe ya kopo pia au ni hewa inaingia haswa wakati akinyonya. Muweke kwenye mabega halafu rub mgongoni hadi atoe hewa utamsikia tu akifanya hivyo na atatulia heea ikipungua.

Kuna watoto kama alivyokuambia mdau hapo juu ni wanakuwa colic na wengine inawasumbua sana sana wengine kidogo wengine hata haiwasumbui.

Fanya haya usiku huu ya kumtoa hewa kama bado anakusumbua sasa hivi.
Tatizo likiendelea kamuone daktari
 
Ni kweli hospitali wanashauri asipewe chochote zaidi ya maziwa ya mama mpaka miezi sita.

Hata mimi mwanangu alikua na hili swala. Mama akaniambia huyo mtoti hashibi, kwahiyo wewe koroga uji mwepesi uwe unampa...
Haikuwa njaa Wala Nini labda Kama ulikuwa huna maziwa kabisaaa. Ni Hilo tumbo la uchanga husumbua asilimia 70 ya watoto wachanga

Maziwa yako yanajitosheleza kwa kitu so Hakuna kitu Kama njaa kwa mtoto wa miezi miwili.
 
Hahaha mkuu mimi ni me.

Anyway, mama alisema hata mimi nilikua hivyo in fact ukoo mzima tupo hivyo so hilo suluhisho ndilo limekuepo miaka yote.
 
Back
Top Bottom