Mtoto wa miezi 7 kamili ameharisha mara 13, dawa akipewa anaicheua

Mtoto wa miezi 7 kamili ameharisha mara 13, dawa akipewa anaicheua

Habar wakuu msaada wenu wa mawazo binti yangu ana miezi saba kamili sasa.

Awali ya yote tangu ijumaa kaanza kuugua malaria akapewa doze ya mseto, sasa tangu alfajiri ya leo kaanza kuharisha na na tumbo kulisikia kama linatoa sauti. Kaharisha mara 13 tangu alfajiri.

Asubuh tukachukua jukumu la kumpeleka zahanati alipotibiwa akaangaliwa dokta akashauri amalizie dozi ya malaria
Sasa kufika saa kumi jion bado akawa anaharisha tukamrudisha zahanati tena kwa dokta,

Akapimwa malaria, ikaonekana malaria imeshuka toka 9 hadi 5 ila mtoto akawa na joto sana ikabidi achomwe sindano yakushusha joto. Dokta akashauri apewe dawa ya kukata kuharisha pia akashauri aanzishiwe sindano kwa ajili ya malaria.

Pia dokta akakagua choo cha mtoto akasema mtoto anaharisha maziwa ya mama ni machafu ikabid mama mtoto akamue maziwa yatoke machafu kwa ushauri wa dokta walau mtoto apate maziwa fresh zoezi lilifanyika tukarud nyumba

Sasa mtoto akapewa dawa ya kukata kuharisha mida hii ya saa kumi na mbili lakini mtoto baada ya dakika 15 mtoto akaicheua dawa yote pamoja na chakula chote alichokula pia baada ya kama nusu saa akaharisha tena.

Msaada wenu wakuu hii, Hali ya kuharisha na pia mtoto kushindwa kuinywa dawa anaicheua nifanyaje?

Maana hii kuhara mtoto mara zaidi ya kumi naona anapoteza maji mwilini, nahisi hatari nisije nikamkosa mtoto wangu nahitaji ushauri wenu wakuu
Hao madoctor hawana akili,mtoto kwa stage aliofikia hastahili tena kupewa dawa za kunywa hapo ni drip na sindano tu ndio salama yake,kingine usilale na mtoto nyumbani hama hiyo zahanati nenda kituo cha afya kikubwa ukalalie huko...
 
Pamoja na kushauriwa dawa nzuri sana
Mpeleke huyo mtoto hospitali haraka sana, anaweza kuishiwa maji kwani sijui kama anapata maji ya kutosha labda kama mama yake anamaziwa mengi sana; nikimaanisha Oral hawezi kunjwa nyingi...
Hiyo kucheua ni kwa sababu tumboni kuna joto (bado ana homa)
Homa inatatiza uyeyushaji wa chakula, na ndio sababu mtu akiwa na homa na hamu ya kula huisha.
Hata hivyo inaweza kuwa ni meno tu yanatoka.... ILA usilale naye nyumbani, mpeleke Hospitali
 
Chuma hicho
 

Attachments

  • IMG-20241008-WA0011.jpg
    IMG-20241008-WA0011.jpg
    78.9 KB · Views: 1
  • IMG-20241008-WA0012.jpg
    IMG-20241008-WA0012.jpg
    44.5 KB · Views: 1
  • IMG-20241008-WA0011.jpg
    IMG-20241008-WA0011.jpg
    78.9 KB · Views: 1
Daah pole sana mkuu..
Kuna mkuu hapo juu amekupa dawa nzuri sana...
 
Back
Top Bottom