Zanzibar 2020 Mtoto wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ni Mshauri wa Mgombea Urais wa CCM Dkt. Hussein Mwinyi

Zanzibar 2020 Mtoto wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ni Mshauri wa Mgombea Urais wa CCM Dkt. Hussein Mwinyi

Zanzibar ni Mali ya Ukoo kwa hiyo tuwaache waamue wenyewe hatma yao.
Haki haitolewi kwenye sahani kama ubwabwa.

Nitawashangaa sana wazanzibari waliovamia CCM iliyoasisiwa kwa malengo ya kuwavuruga na kuua chama Chao cha ASP na Uhuru wao kama ilivyofanya Tanganyika. Tuliua Uhuru wetu baada ya kutupa Jina la Tanganyika ,Nchi yetu na kutupa Bendera yetu iliyopandishwa 9/12 / 1961.

Wazanzibari Mchagueni Maalim Seif anayejua nini maana ya Umoja wa Kitaifa ili kurudisha Furaha kwenye nchi yenu. CCM wanawaweka mbele watoto wa wenzao wanaowaajiri kulinda nchi kwa ajili ya kujipatia madaraka tuu na sio vinginevyo. Dola inatumika kuhalalisha dhulma.

Hussein Mwinyi Asipate kura hata 20% ili Wazanzibari mheshimike na msitukanwe kuwa hamuwezi kujua wala kumchagua kiongozi bora kwa maslahi ya Wazanzibari.

Mwinyi alichovuna kwenye kodi za watanzania kinatosha . Nchi sio Mali yao. Na wengine nao wameumbwa ili waishi sio wao peke yao.
Ufalme sasa basi.!!
 
Zanzibar ni Mali ya Ukoo kwa hiyo tuwaache waamue wenyewe hatma yao. Haki haitolewi kwenye sahani kama ubwabwa.

Nitawashangaa sana wazanzibari waliovamia CCM iliyoasisiwa kwa malengo ya kuwavuruga na kuua chama Chao cha ASP na Uhuru wao kama ilivyofanya Tanganyika...

Endelea kujidanganya na kujifurahisha kwenye keyboard.
 
Kwa hiyo kosa lake ni kuwa mtoto wa jaji mstaafu ambae ni mwenyekiti wa tume au kuwa msaidizi wa Mgombea? Naamini familia yenu ingesoma kwa bidii wewe ungepata moja izo nafasi mbili.

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Aliyevaa koti ni Azizi Hamid Mahmoud, mtoto wa Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)

Huyu Azizi ambaye ni Mwanasheria, ndiye mshauri wa kisheria wa Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi, Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.

Inasemwa kwamba haki sio tu itendeke bali ionekane inatendeka. Kwa hili la Uchaguzi huru na wa haki je?
Kwani haruhusiwi au ulitaka mtoto wako ndio awe mshauri wa mgombea?
 
Unaota mchana, hivyo sivyo mchezo ulivyo.
Lazima Raisi wa Zanzibar atokee chama former ASP(CCM)
Sharti la pili awe na damu ya utanganyika asilia

Sharti la tatu asizaliwe Pemba au kutoka Pemba.
Na hayo sio masharti ya CCM la hasha, haya ni masharti ya waliounda Muungano katika siku 100,wala si Nyerere wala Karume.Waulize Washington au London.

Kila uchaguzi Maalim hapewi ushindi na bado anagangania kugombea mfululizo bila jawabu.
 
Kwa tofauti hii ya tarehe maana yake ni kwamba
JWWTZ
JKT
Polisi
Magereza
Mgambo
Jeshi la akiba (jeshi haramu)

Wote hawa toka Tanganyika watapakiwa ktk majahazi wiki moja kabla kwenda kupiga kura ili kumpa ushindi Mwinyi.
Kumbuka wanapiga kura siku mbili kqbla ya siku ya uchaguzi
 
Kwa tofauti hii ya tarehe maana yake ni kwamba
JWWTZ
JKT
Polisi
Magereza
Mgambo
Jeshi la akiba (jeshi haramu)

Wote hawa toka Tanganyika watapakiwa ktk majahazi wiki moja kabla kwenda kupiga kura ili kumpa ushindi Mwinyi.
Kumbuka wanapiga kura siku mbili kqbla ya siku ya uchaguzi
hao unawataja hapa wameiandikisha huko au ndo mnaandaa lawama?
 
Back
Top Bottom