Mtoto wa mwezi mmoja afariki baada ya wazazi kumuangukia wakipigana

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Taarifa za kusikitisha kutoka nchini Zambia zilianza kuenea wiki iliyopita baada ya mtoto wa mwezi mmoja na wiki tatu kufariki dunia baada ya wazazi wake kumwangukia wakiwa wanapigana.

Tovuti ya Diamond Tv ya nchini humo imesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Reuben Wilaya ya Shiwangandu Mkoa wa Muchinga, ambapo wazazi wa kichanga hicho waliamka asubuhi majira ya saa moja, wakiwa wanapigana ndipo walipomuangukia mtoto wao aliyekuwa amelala kitandani.

Inaelezwa muda mfupi baada ya kugundua mtoto wao amefariki waliamua kumjulisha jirani yao ambaye aliripoti kisa hicho kwa jeshi la polisi.

Baada ya kubaini uzito wa jambo hilo, wapenzi hao waliamua kukimbia nyumba na hadi sasa hawajulikani walipo.

Wazazi hao waliotambulika kwa jina la Shadrick Chanda mwenye umri wa miaka 50 na mkewe, Rebecca Mbikiloni mwenye umri wa miaka 45 kwa sasa wanasakwa na jeshi la polisi.

Mwananchi
 
Daaah inasikitisha sana.........kisheria imekaaje mawakili wetu wa pale mawasiliano? Au nayo itahesabika MANSLAUGHTER
 
Kazi ya shetani hio msipoujua ulimwengu usioonekana unaweza tenda kazi mtakuwa watumwa, mlengwa alikuwa ni mtoto mission possible.
 
Ujinga wa watu wawili wazima umemponza mtu asiye na hatia, mahakama iwapige mvua za kutosha iwe fundisho wa wengine!
 
Huyo mwanamke atakuwa na mdomo sana….wanaume wa kizambia wanapenda sana wanawake na watoto zao
 
Taarifa za kusikitisha kutoka nchini Zambia zilianza kuenea wiki iliyopita baada ya mtoto wa mwezi mmoja na wiki tatu kufariki dunia baada ya wazazi wake kumwangukia wakiwa wanapigana.

Tovuti ya Diamond Tv ya nchini humo imesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Reuben Wilaya ya Shiwangandu Mkoa wa Muchinga, ambapo wazazi wa kichanga hicho waliamka asubuhi majira ya saa moja, wakiwa wanapigana ndipo walipomuangukia mtoto wao aliyekuwa amelala kitandani.

Inaelezwa muda mfupi baada ya kugundua mtoto wao amefariki waliamua kumjulisha jirani yao ambaye aliripoti kisa hicho kwa jeshi la polisi.

Baada ya kubaini uzito wa jambo hilo, wapenzi hao waliamua kukimbia nyumba na hadi sasa hawajulikani walipo.

Wazazi hao waliotambulika kwa jina la Shadrick Chanda mwenye umri wa miaka 50 na mkewe, Rebecca Mbikiloni mwenye umri wa miaka 45 kwa sasa wanasakwa na jeshi la polisi.

Mwananchi

Miaka 50 na 45 bado wana mtoto wa mwezi, wanaendelea kuzaa, Halafu wanapigana, Hawa wana akili kama ya Mayala.
 
Utokea Sana hii ipo moja mtoto hadi Leo ni mlemavu mama anapigwa na fimbo ana mtoto mgongoni kukwepa kiboko kimemfikia mtoto wa chini ya mwaka mmoja aliyebebwa.
Hadi Leo mtoto ni mlemavu
 
Back
Top Bottom