Mtoto wa nje ya ndoa anaruhusiwa kurithi, mahakama ya rufaa yasema

Bashir Yakub

Member
Joined
May 27, 2013
Posts
96
Reaction score
1,745
Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241 .

Tarehe 13/09/2024 Mahakama ya rufaa imeelekeza kuwa mtoto wa nje ya ndoa anatakiwa kupata urithi.

Imeelekeza kuwa urithi wake utakuwa sawa kabisa na watoto wengine ambao wamezaliwa kwenye ndoa. Hakutakuwa na tofauti katika mgao(share).

Imesema jambo la msingi ni kuwa marehemu kabla ya kifo chake awe amemtambua kama mtoto wake.

Na ikasema kumtambua ni pamoja na kuwa amemtambulisha mtoto huyo kwa ndugu na jamaa au namna nyingine ya wazi kuwa huyu alikuwa mtoto wake.

Mahakama ya rufaa ndiyo Mahakama ya juu zaidi na ya mwisho Tanzania ambapo maamuzi hutolewa na Majaji watatu.

Soma Pia: Watoto wa nje ya ndoa hawana haki ya kurithi mali zilizopatikana ndàni ya ndoa

Mahakama imeyasema hayo katika rufaa Na.686/2023 kati ya MIRAJI SALIM NYANGASA dhidi ya RAMADHAN OMARY SEWANDO.

Mahakama imesema hivyo wakati ikitafsiri vifungu vya 5(2) na 10 vya Sheria ya Mtoto 2009 pamoja Ibara ya 2(1) ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki ya Mtoto wa 1989.

Kwa msingi huu yeyote ambaye angetaka mtoto wake wa nje ya ndoa aweze kurithi baada ya kifo chake ni vema kumtambulisha na kuhakikisha ndugu wanamjua. Sio lazima wawe ndugu wote lakini hata baadhi.

Ikiwa utamficha na hakuna ndugu yeyote anamjua akaja kuletwa baada ya kifo chako ataweza kukosa urithi. Na hatakosa kwasababu ni mtoto wa nje ya ndoa bali kwasababu hatambuliki.

Kwahiyo msifiche watoto, japo huwa mnaogopa wake au waume zenu. Mtambulishe hata kwa baadhi tu ya ndugu unaowaamini ili asipoteze haki yake utakapokuwa umeondoka.
 
Hii imekaa poa sana,wanaume watatumia sana condoms safari hii 🤭
Eti utakulaje pipi na Ganda lake.Okee okee🥴
 
Hapa inawapa nafasi wadada wenye Michepuko waume za watu kwenda kutoa vijiti,kuacha kuchoma sindano,kuacha kumeza vidonge.

P2 zinaelekea kukosa soko🥴🤒
 
Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241 .

Tarehe 13/09/2024 Mahakama ya rufaa imeelekeza kuwa mtoto wa nje ya ndoa anatakiwa kupata urithi.

Imeelekeza kuwa urithi wake utakuwa sawa kabisa na watoto wengine ambao wamezaliwa kwenye ndoa. Hakutakuwa na tofauti katika mgao(share).

Imesema jambo la msingi ni kuwa marehemu kabla ya kifo chake awe amemtambua kama mtoto wake.

Na ikasema kumtambua ni pamoja na kuwa amemtambulisha mtoto huyo kwa ndugu na jamaa au namna nyingine ya wazi kuwa huyu alikuwa mtoto wake.

Mahakama ya rufaa ndiyo Mahakama ya juu zaidi na ya mwisho Tanzania ambapo maamuzi hutolewa na Majaji watatu.

Mahakama imeyasema hayo katika rufaa Na.686/2023 kati ya MIRAJI SALIM NYANGASA dhidi ya RAMADHAN OMARY SEWANDO.

Mahakama imesema hivyo wakati ikitafsiri vifungu vya 5(2) na 10 vya Sheria ya Mtoto 2009 pamoja Ibara ya 2(1) ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki ya Mtoto wa 1989.

Kwa msingi huu yeyote ambaye angetaka mtoto wake wa nje ya ndoa aweze kurithi baada ya kifo chake ni vema kumtambulisha na kuhakikisha ndugu wanamjua. Sio lazima wawe ndugu wote lakini hata baadhi.

Ikiwa utamficha na hakuna ndugu yeyote anamjua akaja kuletwa baada ya kifo chako ataweza kukosa urithi. Na hatakosa kwasababu ni mtoto wa nje ya ndoa bali kwasababu hatambuliki.

Kwahiyo msifiche watoto, japo huwa mnaogopa wake au waume zenu. Mtambulishe hata kwa baadhi tu ya ndugu unaowaamini ili asipoteze haki yake utakapokuwa umeondoka.
. Mimi nilinyimwa mirathi kwa sababu ya kuwa mtoto wa nje.... Na dingi alikuwa na mawe ya kutosha 🥸🥸🥸..
.
 
Back
Top Bottom