Mtoto wa nje ya ndoa anaruhusiwa kurithi, mahakama ya rufaa yasema

Watoto wa nje ya ndo wasiruhusi kurithi maana hawatambuliki kidini Wala kimaila
Mtoto ni mtoto, hakuna cha dini wa Wala bibi wa kidini hapa...Mimi nikizaa nje nitampa kila kitu kama watoto wengine.
 
Hii mada ni nzuri sana. Mimi ni moja ya mtoto wa nje ya ndoa, baba yangu alizaa na mama yangu lakini alikua na mke wake pembeni, ambapo alikua na watoto wa 3 kwa huyo mke. Ila kwa mama nipo peke yangu tu.

Turudi kwenye mada, mwezi huu wa 10 niliambiwa baba yangu amefariki kwakua hakua mtu aliye nilea wala kunisomesha (nimesomeshwa na mama tu) nikazipokea zile taarifa. Lakini baba mimi aliwahi nitambulisha kwa ndugu zangu watatu wale wengine na tulifahamiana.

Suala linakuja baada ya kuchunguza nimegundua baba aminiachia mirathi yake kama moja wa watoto wake. Lakini mama yangu hajaniambia chochote kuhusu hiyo mirathi, ambayo ni milioni 25 ambazo zilikua bank. Maana alistaafu mwaka jana hivyo alikua na hela nyingi, ndio amegawa kwa watoto wake.

Sasa mama yangu ndio kapokea kupitia account yake ya bank toka mwezi wa 9, na aliniambia uongo kuwa baba kafariki mwezi wa 10, na hiyo milioni 25 kapokea yeye kupitia account yake. Lakini mimi kama mtoto sijaambiwa chochote, na nilimuuliza mama kasema baba yangu hajaacha chochote bali tuendelee kumuombea tu. Nipo dillema nina mpenda sana mama yangu, lakini juu ya hili nashindwa nifanyaje.

Naombeni ushauri
Mama kakupiga
 
Mtoto ni mtoto, hakuna cha dini wa Wala bibi wa kidini hapa...Mimi nikizaa nje nitampa kila kitu kama watoto wengine.
Kumpa unaruhusiwa ila kurithi wataamua watakaokuwa hai maana wewe utakuwa ushakufa labda uwe umemweka kwenye wosia
 
Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241 .

Tarehe 13/09/2024 Mahakama ya rufaa imeelekeza kuwa mtoto wa nje ya ndoa anatakiwa kupata urithi.

Imeelekeza kuwa urithi wake utakuwa sawa kabisa na watoto wengine ambao wamezaliwa kwenye ndoa. Hakutakuwa na tofauti katika mgao(share).

Imesema jambo la msingi ni kuwa marehemu kabla ya kifo chake awe amemtambua kama mtoto wake.

Na ikasema kumtambua ni pamoja na kuwa amemtambulisha mtoto huyo kwa ndugu na jamaa au namna nyingine ya wazi kuwa huyu alikuwa mtoto wake.

Mahakama ya rufaa ndiyo Mahakama ya juu zaidi na ya mwisho Tanzania ambapo maamuzi hutolewa na Majaji watatu.

Soma Pia: Watoto wa nje ya ndoa hawana haki ya kurithi mali zilizopatikana ndàni ya ndoa

Mahakama imeyasema hayo katika rufaa Na.686/2023 kati ya MIRAJI SALIM NYANGASA dhidi ya RAMADHAN OMARY SEWANDO.

Mahakama imesema hivyo wakati ikitafsiri vifungu vya 5(2) na 10 vya Sheria ya Mtoto 2009 pamoja Ibara ya 2(1) ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki ya Mtoto wa 1989.

Kwa msingi huu yeyote ambaye angetaka mtoto wake wa nje ya ndoa aweze kurithi baada ya kifo chake ni vema kumtambulisha na kuhakikisha ndugu wanamjua. Sio lazima wawe ndugu wote lakini hata baadhi.

Ikiwa utamficha na hakuna ndugu yeyote anamjua akaja kuletwa baada ya kifo chako ataweza kukosa urithi. Na hatakosa kwasababu ni mtoto wa nje ya ndoa bali kwasababu hatambuliki.

Kwahiyo msifiche watoto, japo huwa mnaogopa wake au waume zenu. Mtambulishe hata kwa baadhi tu ya ndugu unaowaamini ili asipoteze haki yake utakapokuwa umeondoka.
Je kama hakutambulishwa lakini akaomba DNA ifanyike kuthibitisha kuwa ni mtoto wa marehemu?
 
Kwani vipimo hakuna kwanini hoja ya mahakama isingesema vigezo viwili maana wapo watoto feki wa nje ya ndoa na watoto feki mpaka wa ndani ya ndoa yani watoto wa kubambikiwa pasipo kujua ...baba anaweza kumtambulisha mtoto wa nje ya ndoa kumbe huyo mtoto kabambikiwa bila ya yeye kujua ...kanini hizo mahakama pumbavu za ccm zisiseme na vipimo vikidhibitisha hivyo au hata kama hakutambulishwa basi vipimo vya kisayansi vikisibitisha kuwa ni mtoto wake kweli....
 
. Mimi nilinyimwa mirathi kwa sababu ya kuwa mtoto wa nje.... Na dingi alikuwa na mawe ya kutosha 🥸🥸🥸..
.
Kwani Kwenu ujulikani namaanisha Kwa Babu na bibi, Baba zako wakubwa na wadogo na Mashangazi? Na hujawahi kwenda kuishi pamoja na ndugu zako pamoja na Baba yako?
 
Hii mada ni nzuri sana. Mimi ni moja ya mtoto wa nje ya ndoa, baba yangu alizaa na mama yangu lakini alikua na mke wake pembeni, ambapo alikua na watoto wa 3 kwa huyo mke. Ila kwa mama nipo peke yangu tu.

Turudi kwenye mada, mwezi huu wa 10 niliambiwa baba yangu amefariki kwakua hakua mtu aliye nilea wala kunisomesha (nimesomeshwa na mama tu) nikazipokea zile taarifa. Lakini baba mimi aliwahi nitambulisha kwa ndugu zangu watatu wale wengine na tulifahamiana.

Suala linakuja baada ya kuchunguza nimegundua baba aminiachia mirathi yake kama moja wa watoto wake. Lakini mama yangu hajaniambia chochote kuhusu hiyo mirathi, ambayo ni milioni 25 ambazo zilikua bank. Maana alistaafu mwaka jana hivyo alikua na hela nyingi, ndio amegawa kwa watoto wake.

Sasa mama yangu ndio kapokea kupitia account yake ya bank toka mwezi wa 9, na aliniambia uongo kuwa baba kafariki mwezi wa 10, na hiyo milioni 25 kapokea yeye kupitia account yake. Lakini mimi kama mtoto sijaambiwa chochote, na nilimuuliza mama kasema baba yangu hajaacha chochote bali tuendelee kumuombea tu. Nipo dillema nina mpenda sana mama yangu, lakini juu ya hili nashindwa nifanyaje.

Naombeni ushauri
Huyo mama yako kwa sasa ana watoto wengine?
 
Kwani Kwenu ujulikani namaanisha Kwa Babu na bibi, Baba zako wakubwa na wadogo na Mashangazi? Na hujawahi kwenda kuishi pamoja na ndugu zako pamoja na Baba yako?
Najulikana fresh tu..... Kwenye vikao vya familia nahudhuria kama kawaida. Sema niliamua kuachana na masuala ya kutegemea mirathi nikazitafuta za kwangu.
 
Kwani vipimo hakuna kwanini hoja ya mahakama isingesema vigezo viwili maana wapo watoto feki wa nje ya ndoa na watoto feki mpaka wa ndani ya ndoa yani watoto wa kubambikiwa pasipo kujua ...baba anaweza kumtambulisha mtoto wa nje ya ndoa kumbe huyo mtoto kabambikiwa bila ya yeye kujua ...kanini hizo mahakama pumbavu za ccm zisiseme na vipimo vikidhibitisha hivyo au hata kama hakutambulishwa basi vipimo vya kisayansi vikisibitisha kuwa ni mtoto wake kweli....
DNA sio kipimo cha mwisho cha kuthibitisha ,kama baba kamtambulisha kakubali basi inakuwa hivo .sijui kwenye sheria imekaaje
 
mtoto wa nje ya ndoa ndio kitu gani kwanza

mtoto atambulike kwa mzazi wake basi haya ya ndoa ndio kitu gani
Ndio nashangaa. Mtoto akishaletwa duniani ana haki sawa na watoto wengine, haijalishi kapatikana wapi. Mlitumwa mumzae?
Mimi sinaga shida na mali za mtu, kama ana mtoto wa nje huko ahakikishe anamtunza na hata kama nikijua nitamshauri atekeleze majukumu yake.
Na mali atapata kama wanae wengine.
 
Hii inahusu kwa watoto waluoletwa na wanaume vipi wakiletwa na mke ? Atakubalika kurithi ? Labda alimpata kabla hajaolewa hakumsema mapema akajasema baadae na yeye atapata mgao ?
 
Back
Top Bottom