Mtoto wa nje ya ndoa anaruhusiwa kurithi, mahakama ya rufaa yasema

Wosia ukiandikwa unahifadhiwa wapi??

Ova

Zipo sehemu zinazokubalika kosheria na kiutaratibu kuhifadhi wosia.
1. Benki
2. Mahakamani
3. Kwenye ofisi ya mwanasheria
4. Kwenye ofisi ya kabidhi wasii mkuu- RITA
5. Kanisani au Msikitini panaweza kutunza Wosia halali. Mahakama ya Kadhi inaweza kutunza Wosia halali wa marehemu kwa upande wa Zanzibar.
 
Sawa,je wosia anayetunza ana tunza kwa siri au ?

Ova
 
Sawa,je wosia anayetunza ana tunza kwa siri au ?

Ova

Wosia ni siri mkuu. Pili mnufaika wa mirathi hatakiwi kufahamu juu ya nini kimeandikwa kwenye Wosia. Mashahidi wa wosia hawatakiwi kiwa wanufaika, na wanaapa kutunza siri hiyo mpaka pale utakapo hitajika (Baada ya marehemu kufariki).

Maeneo hayo yametajwa kisheria kutunza Wosia kwa kigezo cha Usiri na Usalama wa wosia wenyewe.

Wosia unatolewa punde tuu, mwenye wosia anapofariki. Wapo watu wanaandika kwenye wosia wao hadi namna ya Maziko yao kama mwongozo wanavyotaka wazikwe.
 
Aise asanye kwa kunipa elimu
Kuna wakati fulani niliendaga msiba mmoja baada ya kuzika
Alisimama jaji samata alitaja wosia aliouacha mzee si mchezo
Akupindisha maneno yaani pale ilikuwa nyeupe nyeupe nyekundu nyekundu 😄
Kila mtu alijuwa mstakabali wake

Ova
 
mtoto wa nje ya ndoa ndio kitu gani kwanza

mtoto atambulike kwa mzazi wake basi haya ya ndoa ndio kitu gani
 
Mwanangu Nyafwili utaingia kwenye vita 3 ya dunia 😄
Maana tumbo moja watoto wanatoana ngeu sembuse wewe
😄

Ova
Vita ya mirathi ni mbaya sana mkuu ... 😁😁, mpaka sasa wawili wamekufa kwa vifo vya ajabu ajabu.. Mimi nipo na wa-zoom tu 🧐🧐


. Mwenyezi mungu alichonipa kinanitosha kabisa kwa maisha ya hapa duniani 🙏🙏
 

Mkuu Mrangi kuna kuwaga namna kelele, ambae hajaridhika anaruhusiwa mwenda kuupinga Wosia mahakamani.
 
Watoto ni watoto tu nnje ya ndoa ndio ujinga gani huo🤔
 
Sehemu yoyote ambapo kuna binadamu, kufanya mabadiliko yoyote kwenye wosia inawezekana.
Ni muhimu unapokuwa hai kuweka mazingira kwa kila mmoja mnufaika, ajue anatakiwa asimaie wapi kwenye mali za familia.​
 
Nasikitika kwenye hilo shauri waliokuwa wakibishana wote ni Waislamu,wameenda kuwasaidia wanaopinga mirathi ya Kiislamu.
 
Kifo kipo tu hata usipogombea mirathi bado utakufa tu!!
 
Saiv ni mwendo wa ndomu mwanzo mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…