Mtoto wa nje ya ndoa anaruhusiwa kurithi, mahakama ya rufaa yasema

Yaani mtu azae mtoto halafu aseme hatambuliki kidini wala simila. Kwa sheria za sasa atarithi tu upende usipende. Yeye hajachagua baba na mama wa kumleta duniani nyie ndio mmemleta kwa hiyo ni lazima apate haki zake.
 
Kwa utaratibu wa dini ya uislam mtoto wa nje ya ndoa hana urithi labda baba wa mtoto ampatie chake kabisa
 
Hivi mnajua hakuna mtoto wa nje ya ndoa kwa mwanaume.

Kwa mwanamke ndio nje ya ndoa yake.

Kwako mwanaume ni mtoto kama walivyo watoto wengine. Walipotoka hao uliowqpata kwa mke mlieandikishiana mkataba wa kisheria kuoana mkaita ndoa ndipo alipopatikana huyo uliyemzaa bila mkataba wa kuoana.


Kuanzia leo, wanaume hakuna kuita watoto wako nje ya ndoa hata kama umezaa na wanawake 100. Wote ni watoto wako halali
 
lakini hiyo kesi bado imewachinjia baharini watoto wa nje ya ndoa kwenye mirathi ya kiislam. labda tukubaliane na hilo. watoto wa nje ya ndoa wanaotambulika kwenye urithi kwa mujibu wa maamuzi hayo ni wale wa kikristo, wale wapagani, wahindu na wengine ambao sio waislam. ila kama mirathi inagawanywa kwa kiislam, mtoto wa nje ya ndoa msimamo upo palepale, HARITHI CHOCHOTE, ni mtoto haram, labda kama kulikuwa na share kweney wasia isiyozidi 1/3. ambayo nayo atapata sio kama mrithi, ni zawadi tu anayoweza kupewa mtu mwingine yeyote.

sheria ya kiislam inaumiza sana watu kwenye mirathi, ninyi wazazi mmezini huyo mkazaa mtoto nje ya ndoa, mtoto aliyezaliwa ana kosa gani? yeye amejikuta tu amezaliwa ila anaadhibiwa kwa makosa ya wazazi wake, haki ipo wapi hapo?

nawakaribisha masingle mothers, ambao ni waislam muukimbie uislam mara moja kwa sababu watoto wenu wanatambulika ni haram na hawatarithi chochote toka kwa baba yao. na ninyi msio waislam, jipendekezeni tu kwa waislam wawatie mimba, hat akama ni tajiri mwenye mabasi kisheria mwanao hatarithi chochote, labda kwa wosia ambao ni wachache huwa wanakumbuka kuandika.
 

Attachments

Mi nafikiri wanaume mridhike na wake zenu
Short of that pimeni DNA na andikeni wosia kutunza watoto wote
 
Sheria za dini zisikutishe, Mahakama ndiyo inatafsiri sheria zilizotungwa na Bunge letu tukufu,wala usihofu,na Mahakama ya juu kabisa imeshapigilia msumari!!
 
Mtoto wa nje ya ndoa yupi maana wapo wawili,
  1. Yule aliyezaliwa na mke
  2. Yule aliyezaliwa na mume
 
Sheria za dini zisikutishe, Mahakama ndiyo inatafsiri sheria zilizotungwa na Bunge letu tukufu,wala usihofu,na Mahakama ya juu kabisa imeshapigilia msumari!!
we ni mwanasheria? nimekuwekea kesi hiyo hapo, isome. ndio imesema hivyo, mtoto wa kambo kwa waislam imebaki palepale, ni mtoto haram.
 

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…