Mtoto wa nyoka ni nyoka; Isack Mwigulu atoa msaada wa ream paper kwa Uvccm Singida

Mtoto wa nyoka ni nyoka; Isack Mwigulu atoa msaada wa ream paper kwa Uvccm Singida

Like father, like son!
Kuna mahali nimesema hivi kuhusu CCM kubadilisha Watanzania tulivyoitana "ndugu" na kutaka wao waitwe "waheshimiwa"'

"Basi leo tunaona matokeo na laana hii ya ubaguzi wa ndani ambao chama hiki kinachotawala, CCM, kiliianzisha. Matokeo sasa ni kwamba Tanzania imezaa tabaka la viongozi (vigogo) ambao wanajiona wako tofauti na hata sheria za nchi haziwahusu. Tuna hili kundi la viongozi, "waheshimiwa" ambao halitaki kusikia maoni ya mtu mwingine ambae haitwi mheshimiwa. Wao wanajiona wanajua kila kitu na hawapaswi kuulizwa, na wako juu ya sheria, na Polisi, Usalama wa Taifa na hata JW wakati fulani, wapo kwa ajili ya kuwalinda wao, nafasi zao na utajiri wao ambao kila mtu anajua umetokana na ufisadi na sio mishahara yao. Wameamua kwamba mtu yeyote asie mheshimiwa, akileta ubishi au maoni tofauti wasiyopenda, atekwe, apigwe hata kuuawa ikibidi!

"Hawa "waheshimiwa" na familia zao wamekuwa wakibebana katika nafasi za serikalini, na hata kutengeneza mazingira ili watoto wao waje waurithi "uheshimiwa" hapo baadaye, jambo ambalo limeleta wingu kubwa la vigogo ambao baba zao walikuwa vigogo huko nyuma!"


Utawala wa Rais Mwinyi ulileta neno "Mheshimiwa" badala ya "ndugu" kwa viongozi na sasa wamekuwa tabaka lenye kujiona wako juu ya Watanzania wengine!
 
Back
Top Bottom