Fred Mwakitundu
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 227
- 382
Wakati wananchi wa Kilimanjaro wakiwa bado na kumbukumbu za tukio baya la kuuawa kikatili mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Scolastica miaka michache iliyopita,mapya yameibuka katika shule hiyo.
Taarifa mpya kutoka kwa watumishi wa shule hiyo zinatonya kuwa,mtoto wa tajiri wa shule hiyo aitwaye Elizabeth Shayo anadaiwa kuendesha vitendo vya kikatili kwa watumishi wa shule hiyo.
Eliza amekuwa akiwadhalilisha watumishi hao pamoja na kuwatolea lugha chafu ,kuwafokea ovyo hasa wanapokuwa wakidai maslahi yao na baadhi wamejikuta wakifukuzwa kazi bila tararibu za kazi kufuatwa..
Baadhi ya watumishi walioomba hifadhi ya majina yao wanadai kuwa vitendo hivyo vimekuwa sugu huku kukiwa hakuna hatua za kumchukulia kwa vile ni mmoja wa wakurugenzi wa shule.
Watumishi hao kutoka Idara ya ualimu,upishi,usafi,ulinzi na watumishi wasio waalimu wanadai kumekuwepo na matabaka kati ya walimu kutoka nchini Kenya na wazawa ambako wakenya wamekuwa wakipewa upendeleo katika maeneo mengi.
Unataka kujua mengi kuhusu vitendo vinavyofanywa na mtoto wa tajiri huyo?,kaa mkao wa kula mengi zaidi yanakuja