BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Katika pitapita zangu mitandaoni, nimekutana na makala hii inayohusu mahojiano aliyoyafanya huyu jamaa anaitwa Frank ambaye anasema ni mtoto wa Mchungaji Zachary Kakobe, nimeona si vibaya nikishea hapa inawezekana kama ni kweli basi ujumbe umfikie kwa urahisi mtumishi kwa kuwa najua JF ni platform kubwa na inafika mbali.
@@@@
Naitwa Frank Zachary Kakobe, mimi ni mzaliwa wa Tuliani, Wilayani Mvomelu Mkoani Morogoro, nilisoma Elimu ya Msingi Mwenge Mwaka 1986 hadi 1993 baada ya hapo nikaenda Real High School ipo Thiker Nchini Kenya
Baada ya hapo nikasomea masuala ya kompyuta nikapata Diploma katika chuo cha Techno Brain, sijui sasa hivi kinaitwaje.
Nina umri wa miaka 43, nina Watoto watatu na baada ya kuhitimu masomo yangu nilifanya kazi kadhaa za kiufundi.
Nia yangu ya kujitokeza kuzungumza hapa ni baba yangu apate taarifa juu ya uwepo wangu, tangu nilipoachana naye miaka 17 hadi 20 iliyopita, nimejaribu mara kadhaa kumtafuta kwa njia nyingi kupata mawasiliano naye lakini imekuwa ngumu.
Nimewahi kukaa pale Kanisani zaidi ya wiki sijaonana naye, nilipowaona viongozi wa Kanisa lake wakaniambia niandike barua ndio nitafanikiwa kumuona, nikafanya hivyo kwa kuandika barua za zaidi ya 300 lakini sijafanikiwa.
Nimetuma SMS za simu nyingi tu lakini hakuna mafanikio, ninachokumbuka nimewahi kukutana naye mara kadhaa akiwa anaingia kwenye gari nikawa naishia kumsalimia “Shikamoo Baba”, basi baada ya hapo inaishi hivyohivyo.
Nimeshaenda nyumbani Mbezi Beach lakini sijafanikiwa kuonana naye, hata wiki mbili zilizopita nilienda nikakutana na mlinzi ambaye akaniambia niandike barua.
Nikawa najiuliza niandike barua tena? Akaniambia ndio utaratibu, nikajiuliza niandike barua kuingia nyumbani!
Nakiri kuwa hali ya mazingira kama hayo ikanifanya niwe mlevi, mara kadhaa nikawa nalewa licha ya kuwa mimi sipendi pombe.
Kuna muda nilikuwa nalewa kisha naenda Kanisani kumtafuta baba yangu kutokana na mawazo, nilikuwa nalala hapohapo Kanisani lakini hakuna mafanikio.
Sijui kuna ukuta upi uliotokea kati yangu na baba hadi anifanyie yote hayo, nakumbuka mara ya mwisho kupata mrejesho ilikuwa wakati nahitaji vyeti vya Watoto, nilituma SMS zaidi ya 80, ndipo nikajibiwa kuwa nifike getini nikachukue hivyo vyeti.
Nilienda na nikasaini kisha baada ya hapo sijawahi kupata mrejesho wowote.
Nilikuwa kimya muda mrefu, lakini nimeamua kufunguka na kumtafuta, mimi sina madai yoyote kuhusu baba, kwamba ndani ya miaka yoye hiyo ambayo sijamuona nadai kitu fulani, Hapana.
Unajua yeye ndiye kanilea kuanzia nikiwa mdogo nina miaka mitatu.
Kuhusu ukaribu wa wadogo zangu na mimi haupo, sijui wanapokaa wala wao hawajui ninapokaa na wala sijawahi kukaribishwa wala kushirikishwa kama familia licha ya kuwa mimi ndio nilikuwa ninawalea kwa kuwa walinikuta kaka yao.
Naamini barua ambazo nimekuwa nikituma inawezekana zinamfikia au hazimfikii, hivyo nimeamua kutumia nafasi hii kuweka wazi ili kama kuna ukuta upo kati yetu uweze kubomoka.
Matatizo katika familia yapo na ni kawaida kutokea, sijajua tatizo lililopo kati yangu mimi na yeye (Kakobe), kiasi kwamba kumekuwa na ukuta huo mkubwa.
Mfano mimi sinywi pombe kwa starehe, lakini imetokana na mawazo na kuathirika kisaikolojia, pia kwa kuwa nimeathirika kimaendeleo basi hata familia yangu pia imeathirika kwa njia moja au nyingine.
Baba yangu ni mtumishi na ninajua ana upendo sana, naamini haya mambo anaweza kuyatatua watu wakasameheana kama kulikuwa na shida.
Pia nina dada yangu anaitwa Mage ambaye naye hajaonana na baba kwa muda mrefu inawezekana zaidi hata ya ilivyo kwangu.
Chanzo: OnTV