Mtoto wangu ananishangaza

Mtoto wangu ananishangaza

Malezi na mazoea yana nafasi kubwa.Wangu,wa kwanza, by mwaka na miez miwili alikua anaamka mwenyewe.Nepi na pampas aliacha mapema sana.

Wa pili alikua mbali nami, mwaka jana, akiwa na miaka 2 na miez 5 hivi, akawa anashusha kila kitu kwenye nguo, nikamchukua kukaa nae baada ya mwezi anaenda mwenyewe chooni kwa haja ndogo, haja kubwa anatamka...na anaendelea hivyo hadi kesho.

So, kwa uzoefu wangu, kama mtoto hana shida yeyote,malezi yana mchango mkubwa sana kwenye hivyo,na vingine vingi sana.
 
Ukiona hivyo ujue una bwana mkubwa hapo! Mlee vizuri, mheshimu, usimchape wala kumfokea, huwa hao ni watoto wa kipekee hawahitaji kelele, wana akili kubwa ni wastaarabu na wanakuja kuwa WATU wa maana. Ila pia chunga nyota yake isichezewe na majuha mtaani.

Mweke chini ya ulinzi wa Mungu Mwenyezi, usimfanyie matambiko kamwe, wala kumvika hirizi. Kama kuna hirizi umemvika ondoa mara moja, una mharibu.

Mpeleke shule ya uhakika, mpe anachotaka, vitu vya kuchezea, mpe uhuru wake! Unaye bwana mkubwa hapo! Huyo ni sharrif kwa maneno mengine.
 
Kawaida sana hiyo Mkuu.

Wanangu wote wametembea na miezi nane. Na mwaka mmoja na nusu hawakojoi kitandani. Mama yangu aliniambia nami nilikuwa hivyo hivyo.
Watu wa namna hiyo ni wa pekee, wewe unajionaje una ishara zozote za kuwa mtu wa pekee au ni kawaida tu ya kitaani?
 
Niaje wakuu

Tusichoshane.

Mtoto wangu ametimiza miaka miwili mwezi wa kwanza. Kinachonishangaza ni kuwa hajikojolei wala kujinyea.

Akitaka kukojoa au ku poop anasema na usiku hata ukimvalisha pampas anaamka anakuambia anataka ku poop au jojoa.

Nimenunua kibunda cha pampas mwezi wa 11 ila hakijaisha. Na kula anakula hachagui chakula na kunywa maji, juice anakunywa kila siku ila hajikojolei.

Huyu chaliangu ni jembe.

Au wamama mnasemaje? Dr Lizzy Simara Culture Me cocastic Sky Eclat Joanah Bushmamy Numbisa Shunie Depal Makiwendo Evelyn Salt Hannah Stress Challenger Chaliifrancisco
Na wangu pia yuko hivo.
 
Back
Top Bottom