Mtoto wangu anayeishi na mama yake tulieachana analelewa ndivyo sivyo, ustawi wa jamii imeshindikana kumchukua, mama yake hataki niwe nae, nifanyeje?

Kwahiyo mtoa mada huyo mtoto akila chips mayai unahisi atakuwa sh*ga au sio??? Acha mawazo potofu…Tafsiri ya sh*ga ni mtu ambae pia kakosa sifa ya uanaume kama wewe hapo wa kushindwa kubeba jukumu la uwajibikaji kwa mwanao
 
Mwanamke anakupangia ukae au usikae na mtoto uliyempata kabla ya ndoa,?Lakini mwanamke huyo huyo ndugu zake watakuja watakaa wanavyotaka hapo kwako.Simama kama mwanaume mwanamke hana mamlaka ya kukupangia ukae au usikae nae.Ingekuwa ni mimi ningemleta na kukaa angekaa vizuri tu.Maana huko mbeleni unatengeneza bonge la bomu akija kuwa kijana mkubwa atasema baba hakuwa kuwa na muda na mimi na hapo kumbuka mama yake anamlisha sumu juu yako.Hatakumbuka ulilipa ada wala kuwa unatoa hela ya matumizi.Watu wanangangania kukaa na watoto kwa sababu ndio kipindi pekee utatengeneza bond na mtoto!
 
Chukua mtoto wako mapema hii dunia imeharibika
 
Bibi na Babu zake vipi
Yaani azae yeye asumbue bibi na babu.. hebu achani wazee wamalizie maisha yao kwa raha.. wakulee wewe na wamlee mwanao.. hii tabia ya kipuuzi ikome sasa. Binafsi sitakubali huu ujinga, kila mtu abebe mzigo wake.
 
Yaaani mkeo anakutaza kuleta mtoto wako uliezaa nje tena damu yako, na wewe unakubali? Kweli wanaume wanazidi kupungua, na ww una shida aisee
 
KAKUONA WEWE NI MKOPO WA KOREA WA SAMIA
 
Binadamu wabinafsi hapo anajua mtoto hata amchukue atapata tabu , mda huo ana mwanamke wmingine ambaye atamtesa ...Huu ndio ujinga wa kuzaa ni kumkatili mtoto .

walioachana washapata wenza ila mtoto hawezi kupata malezi mazuri milele.
Wote waweke ubinafsi wao pembeni, na mtoto atapata malezi mazuri tu kote kote!!
 
Yaaani mkeo anakutaza kuleta mtoto wako uliezaa nje tena damu yako, na wewe unakubali? Kweli wanaume wanazidi kupungua, na ww una shida aisee
Mimi sikatai damu yangu hata kama naishi Kizimkazi,lazima niisogeze karibu yangu hata kama Kizimkazi atakwazika,maana ni swala la muda tu watazoweana na kua marafiki chini ya usimamizi wangu kama Baba Kizimkazi!!
 
Hiyo Sheria ya miaka saba inatoka wapi? Binti yangu nilimchukua kwa mama yake akiwa na 4yrs. Nafikiri ustawi wanaangalia zaidi wapi mtoto atalelewa vizuri
Miaka 7 ni kama mama yupo vema hana tatizo eneo la malezi ila kama ni wa hovyo then unaweza mchukua hata kama ana miezi miwili.
 
Mbembeleze mkeo kwa maneno matamu,ikibidi washirikishe wazee wa dini yenu,Mungu mwema utafanikiwa!
 
Sema wanangu huwa mnayumba sana😁😁,yaani unadate na mwanamke unamwambia issue za mtoto wako anakwambia hawezi kaa naye nawewe unamuoa😅😅😅.

Sasa huyo ni mwanamke au ni takataka??ulionyesha udhaifu mkubwa sana mkuu.

Haya kachukue mtoto umpeleke kwa bibi yake,mama yako nk.
 
Mmmmh kaka apo ulishavamia mtumbwi wa vibwengo tulia tu
 
Wallah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…