Mtoto wangu wa pili kamzidi kaka yake ujasiri, ujanja, uwajibikaji. Hii ni kawaida?

Jitahidi kupunguza kunywa kidogo for enjoying usipambane na pombe hutoiweza.

Epuka company mbaya upuka kunywa kwa kupambana na stress itakuharibia..

After time utakaa sawa.
 
Utachagua mwenyewe Sasa, unataka Kupanga au Kilaza ila mjanja mjanja 🀣🀣
 
Wakwanza ni introvert wapilli ni ambivert yani ka mix u introvert na extrovert!, so nenda katazame sifa za watu wenye hizo tabia utaelewa!.
Lakini umesema wa kwanza sio jasiri ni muoga!.. Hii sifa haifai sana haswa zaidi kwa mtoto wakiume!.

Weka namna ufanye juu chini uhakikishe anaongeza ujasiri nakupunguza uoga!, mfanye ajiamini mchanganyishe na watu!, mfanye awe talkative muulize hata swali ambalo litamfanya atoe maelezo yakutosha ama uwe unapiganae stori.. toka nae fanya nae vitu ambavyo vitakuwa effective ktk kumuongezea ujasiri, mpe kuku achinje!, kama akipata likizo peleka kijijini akalime huko atachangamana na watu pia!, hivi vitu vikimkaa kwa muda utaona ujasiri wake unaanza kuongezeka!.
nyumbani kuna manyasi mpe fyekeo afyeke, kuna mti unataka ukate mpe msaidizane na umuelekeze!.. yani hata kama unataka kufanya sherehe sijui umeleta kimbuzi mnataka mkichinje muite awepo na ashike hata mkia wakati mnachinja na kuchuna achune!. yani huyo kwenye swala la ujasiri kuwa ngangari haswa!.
Nakusisitiza tena ni vibaya sana mtoto wakiume kukosa ujasiri mkunje sasa ili akikua awe ameshakunjika kuna opportunity atakuja kuzipoteza kisa ujasiri!..

Mengine utajiongeza nawewe!.
 
Ni kawaida mbona sasa wekeza kwa huyo mdogo kwenye talanta yake halafu uwe karibu na mkubwa na usisahau kumpa.nafqsi yake ya kwanza. Utakuja kutengeneza ugomvi mkubwa ukiwa upande mmoja. Ila usisahau kila mtu ni genius kwenye eneo lake. So huyo nae kuna eneo atakushangaza. Waombee watoto na uwatolee sadaka.
 
Madarasa umesoma Hadi langap mkuu? Nauliza Kwa uzur tu,,
 
Ni kawaida kabisa hata wa kwangu wako hivyo na hata kwenye uzao wa mama yangu hivyo hivyo.
Uchagani ilibidi wapewe majina yao rasmi ya kuwatambua watoto wa pili kuzaliwa kwasabu ni watu weny makeke, korofi, wasioambilika.
Ukisikia Manka sio jina la kila mwanamke kama wengi wasio wachaga wanavyoamini, hilo ni jina specific kwa mtoto wa pili wa kike.
Ukisikia Lelo hilo ni la mtoto wa pili wa kiume.
Ni watu wenye mambo kama uliyosema huyo wako anayo
 
Watu hawafanani,kuzaliwa tumbo moja sio sababu ya kufanana.Nahisi kama unamnyanyapaa huyo mmoja kwa tofauti zake na kuna unayoshabikia kutoka kwa mdogo wake wala hayana hata mantiki. Kwa mfano kupigana,huko baadae ukiambiwa anakaba Watu bado utashangilia?.Nimeshapona familia nyingi ziko hivyo hakuna cha ajabu hapo.
 
K Kudos. Umeeleza vyema.
 
You need to know hata vidole vyako havifanani na
Uthibitisho kwamba spare nazo hazilingani zipo zenye moto na zipo za baridi

Ilihali zote zimetoka kwenye kiuno chako
 
Watu hawafanani. Hata ukirejea kwenye Bible kwenye ile story ya mapacha Yakobo na Esau. Esau baba yake alimchukulia kama kidume mwenye uwezo wa kuwinda ila Yakobo alichukuliwa kama "mtoto wa mama" kazi yake ilikuwa ni kutengeneza mchuzi wa dengu na kazi nyingine za nyumbani.

Ila mwishowe Yakobo alichukua baraka za mzaliwa wa kwanza na ndiyo chanzo cha taifa la Israel.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…