Mtoto wangu wa pili kamzidi kaka yake ujasiri, ujanja, uwajibikaji. Hii ni kawaida?

Kapime DNA kwanza
 
Mtoto wa kwanza mlimtisha, kumuadhibu na kumkemea vikali hivyo kapoteza kujiamini.
 
Wakiwa wakubwa watakuwa hawapatani, watakuwa wanakaa hata miezi 4 bila kupigiana simu.
Kwanini? Hakuna cha kuwaunganisha, mifumo haisomani.
 
Wakiwa wakubwa watakuwa hawapatani, watakuwa wanakaa hata miezi 4 bila kupigiana simu.
Kwanini? Hakuna cha kuwaunganisha, mifumo haisomani.
Kadogo katajifanya kakubwa, Hilo vurugu lake...................................................

Ogopa huyo mpole na mkimya, hiyo familia kitakuja kuwaka sana.
 
Achana naye mwache alivyo mimi nilizaliwa mkimya na vutwa vutwa weh nilipokuwa 17 hadi naleo naitwa shindikanaaa
 
Your browser is not able to display this video.
 
Nakuhakikishia, mtoto wako mkubwa ni genius na mwerevu Sana, time will tell
 
I wish mtoto wa pili angekuwa wa kwanza
ukilionesha hilo wazi utawajengea chuki hao watoto.

Kuna childhood trauma jamaa mmoja anayo sabb udogoni walikuaga wanamwambia kwamba mdogo wake kamzidi kama ww unavyosema hapa.

Hii ilikuja kutengeneza chuki fln ukubwani ambayo inamcost mchukiaji, ofcoz chuki siku zote inamcost mchukiaji
 
Mleta mada zingatia Sana alivhokisema huyu mshauri, EPUKA kumkemea mbele ya huyo mdogo wake kwamba yeye ni mzembe mdogo wake anamshinda, hii itamjengea kiburi mdogo mtu na kufanya sifa zaidi lakini huyu mkubwa ndio atazidi kusinyaa na kujitenga lastly inatengenezwa chuki baina yao. Be careful
 
Nadhan Harris gani sana na hawa wa kwetu huku! Wote wa kiume! Ila huyu wa pili nyie ni zaidi ya mtu mzima! Ana fanya mazungumzo km mtu mzima na huwa anatoa ushauri! Yuko darasa la 4! Kweli kila mtoto ana namna yake aisee! Wa kwanza mpaka Nahisi labda tulimtisha sana akiwa mdogo ama niaje! Muoga, anapenda sana kucheza mpira, ukimsemesha kwa Kumkanya angalia! Yani halafu sasa hana mwili kabisaaaaaaaa ila mdogo wake aaah ni kibonge kweli kweli mpaka sasa inabidi akomae na mazoezi ya kuendesha baiskeli apungue kidogo!
 
Kawaida Sana. Kila mtu ana vipawa vyake
 
Nani alikwambia undugu "kufanana"? Kila mtu Mungu alimpa kitu cha pekee ambacho mwingine hana.
 
Sikia watoto kamwe hawawezi kufanana lakini kuna mtego utauingia ambao kwa sasa hutauona,

Ukiamini sana huyo wa pili ndio mjanja mjanja ni wazi kabisa utaanza kumpa nafasi kubwa katika mambo kuliko huyo wa kwanza hapo ndio utakapoharibu mambo kabisa kabisa ,

Cha kufanya jaribu kumuwekea mazingira ya kujiamini na yeye kuliko siku moja ajione kama haeleweki kwenye familia
 
Huyo mtoto wa kwanza atakufaa baadae sio sasa.

Ndivyo inavyokuwa. Utanishukuru baadae
 
Ko unataka wafanane kila kitu?
Unahitaji kujitafakari zaidi unawajua introverts?
Hamna genius mwenye mambo mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…