Mtozi Alloyce Nyanda: Kuna watu wanamtumia Swai kumchafua Sabaya?

Mtozi Alloyce Nyanda: Kuna watu wanamtumia Swai kumchafua Sabaya?

Kwa siku za hivi karibuni kumeibuka video mbalimbali zikiwemo za baadhi ya viongozi wakifanya matendo yakinyama kwa Raia . Kwa Taifa changa kama letu na kwa mitandao ilivyozagaa video hizi zinaangukia mikononi mwa watoto. Wanapoona namna wazazi wao wanavyonyanyaswa, wanavyoona namna viongozi wanavyotawala, wanavyoona hakuna mzee au Kiongozi katika ngazi ya Taifa anayechukua hatua wanajenga chuki na nchi yao...
Kaa kwa kutulia wewe!

Yaani watu wanyamaze na wanaonewa????
 
Sasa mimi kwa macho yangu nimemuona Sabaya anakuja Arusha na msafara wa wapambe na mademu wa chuo na walinzi wamebeba bunduki SMG huku wamevaa maspy koti, na chimbo lake alilokuwa anapenda Ni Hotel ya Point Zone pale mianzini,swali anakuja na mabunduki kila siku arusha kufanya nini na sio eneo lake la kazi? Pili Sabaya ana rekodi anaingia Bar anakula,anakunywa na wapambe wake zaidi ya 10 na walinzi wake, ikifika muda wa kulipa bill anajifanya "amepigiwa simu na muheshimiwa", anaingia kwenye gari anaondoka. Amesababisha wahudumu wengi sana kukatwa mishahara yao ili kulipia bill za Sabaya na wapambe wake. Tatu, uliza maduka ya Arusha hasa ya electronics yaliyopo stand ndogo, Sabaya anaenda anachukua Tv hadi za million 3 anasema atakuja kulipa,akipigiwa simu kukumbushwa deni hapokei simu. Jambo linanishangaza unapata wapi ujasiri wa kumtetea mtu muovu kama huyo? Sisi tunamjua personal, sio mambo ya kuhadithiwa na mtu. Amerusha pesa watu wengi sana, ametesa watu wengi sana.Mama Samia asipomshugulikia, MUNGU atamshugulikia.
Sabaya kumbe ni mtu mbaya sana
 
Sabaya ni jambazi alikua anaenda Arusha na wahuni wenzie anawapa pesa wananunua kwenye duka harafu jamaa adai risit anatoka haraka baadae wanakuja wao kujifanya wamemkamata kumbe ni mchongo huku wamechunguza mpaka account yako na kukuambia usipotoa milioni hamsini unapewa kesi ya uhujumu uchumi mimi nilisema zambi ya kuua ntaipata waje wafanye huo ujinga kwangu bahati nzuri kwao hawakuonekana tena kwenye maduka ya stand kubwa...huyo ni jambazi jambazi
Haya ni swala la muda tu, jiwe kwa jiwe, moto kwa moto
 
Ipo siku tutaanza vita vya wenyewe kwa wenyewe na hivi vitaanza kama njia yakujilinda dhidi ya watu/mtu fulani kisha vitahamia kwenye kabila la mtu huyo fulani mwishowe ni vurugu ya nchi nzima.

Chuki ni kubwa sana huu muda, hadi watu wanashangilia kifo cha raisi wao. Hii si dalili nzuri
 
Anaandika Mtozi Alloyce Nyanda

Nimeona Video ya Mfanyabiasha Cathbert imepostiwa na @kumbushodawson

Kumbuso ni rafiki yangu sana na kwa kuwa sisi sote huwa ni waumini wa ujenzi wa hoja basi kabla ya kuingia katika mjadala wa msingi napenda maswali haya yajibiwe kisha tuje sasa kwenye Hoja hiyo hapo juu.

1. Huyu Bwana Cathbert mwaka 2019 aliwahi kusema kuwa Mkuu wa wilaya Sabaya aliwahi kuvamia hotelini kwake na makundi ya watu na kupora hela na kulazimisha kuchukua mwanamke kwa nguvu na kwamba Bwana Cathebert alisema atatoa Video ya CCTV ikionyesha huo unyama wa Sabaya lakini tangu mwaka 2019 hadi leo ni miaka 2 hakuna hiyo Video; je Video ipo wapi?

2. Anadai Sabaya alimzuia mwekezaji wa maonyesho ya nyoka kufanya hivyo Hai! unajua nyoka ni maliasili na nyara muhimu za serikali? umewahi kumuuliza kama alikidhi vigezo na taratibu za kisheria kumruhusu kufanya hivyo?

3. Huyu bwana katika Video hapo
Juu anasema amekimbia na kujificha kutokana na vitisho vya Sabaya na anamuomba mama Samia amsaidie! Swali mtu anasema amejificha wakati anasema yupo pahala flani kwenye shamba tena mchana kweupe na yupo Tanzania je Kumbuso kujificha ndo huku ambapo Mimi na wewe hatupo Kilimanajaro ila tumeshajua huyu bwana yupo wapi!

4. Asante Tours Ooshi si Arusha na kwamba kuna video ikionyesha kwamba mwezi wa pili mwaka huu kampuni na ofisi iliuzwa kwa mnada na bank ya CRDB mil 600 kutokana na madeni ya bwana huyu anayodaiwa toka mwaka 2009 huko nako Sabaya alikuwa Hai?

6. Zimekuwepo tuhuma za huyu bwana kupora maeneo na kuyabadilisha hati kisha anaenda kukopa bank na kuyatumia kwa
Manufaa yake na DC alishwahi kuyarudisha mashamba kwa wenyewe, je Kumbuso unafahamu Hilo? Je, alishawahi hata kujirekodi kusema kuwa ni uwongo?

Baada ya uteuzi wa mawaziri,makatibu wakuu mhe Rais alisema sasa anakuja kwa ma Rc na kina sabaya,Haya nayo yakazuka,common sense inasemaje?

Naomba Tuanze na haya kisha twende kwenye hoja ya Msingi ya bwana Mfanyabiashara ambae yupo shambani alipojirekodi kutupa habari amejificha.
Unajaribu kusafisha shimo la choo, utaweza?
Ni nani ambaye hakusikia ujinga wa huyo unayemtetea? Aibu yake na laana yake vitamfuata hadi kizazi chake cha saba, usijaribu kununua matatizo ya mpuuzi
 
Mtozi Aloyce Nyanda inabidi adeclare interest kwa sabaya ,Sabaya alimchangia fedha nyingi sana Mtozi kwenye Harusi yake...Sabaya ndio Financier wa Mtozi.....Ni lazima Mtozi atoke povu maana sabaya akiondolewa basi na yeye atakosa pesa za sabaya.
Na pesa alizochangiwa ni za kupora wafanyabiashara , hii ndoa ikimaliza mwaka huu itakuwa ajabu sana !
 
Viandishi vyabongo vingine vijingavijingaaaa...vinajua kujipendekeza kuliko kazi!!!
1.) Rais amewahi agiza watu waanzishe zoo zao. Hata arusha kuna snake park sasa mambo ya nyara za serikali yanakujaje? Kwanini DC asimshauri mwekezaji njia sahihi ili kukuza uchumi na ajira hai?
2.) Kuhusu kujificha nyanda anakuwa mjinga zaidi,kwani ukijificha huwezi kutoka ukaenda mahali ukarekodi ukarudi ulipojificha, anahisi kujificha ameingia shimo la majitaka kama sadam? Au kaenda torabola? Hopeless!!!
3.) Huyu alishindwa kesi ya shamba LA mh. Mbowe,kwanini tusiamini ananyang'anya watu bila kufata sheria.
4.) Anakamata na kufunga watu hovyo na mkuu wa mkoa alipomsihi aache alionesha dharau na kumkebehi huku akivua miwani na kumwangalia kwa hasira na kumng'ong'a hadharani mbele ya watendaji na video ipo ikionesha hayo.
Swali ni je? Alitumwa hai kwenda kumaliza uwekezaji na kutesa wawekezaji? Assignment yake ni kuifanya hai maskini? Kwanini anapambana sana na wafanyabiashara na wawekezaji? Je, angekuwa Chato angetesa nduguze mwenda kama afanyavyo hai??
Yote yanamwisho Huyo nyanda aendelee kujinyandika kwa dikteta mjinga
 
SWALI LA 1: SIONI MANTIKI KWA NYANDA KUMUULIZA SWALI HILI KUMBUSHO. KWANZA SIO KUMBUSHO ALIYEDAI KUWA NA HIYO VIDEO. PILI, ILE VIDEO YA CCTV IWEPO AU ISIWEPO HAIONDOI TUHUMA ZILIZOPO DHIDI YA SABAYA, KWA KUWA UTENDAJI KAZI WAKE UMEJAA VITENDO VYA KIHUNI NA USIOZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI. TATU, KIMBUSHO HATOI TUHUMA, TUHUMA ZINATOLEWA NA SWAI.

SWALI LA 2. SWAI HASEMI KAMA HUO MRADI WA NYOKA ULIZUIWA NA WATU WA MALIASILI, KUMBUSHO HANA SABABU YA KUWAULIZA WATU WA MALIASILI KWA KUWA ANAMNUKUU TU MLALAMIKAJI ANAYEDAI SABAYA NDIYE KAMZUIA. SWALI AMBALO YEYE MWENYEWE MTOZI ANAPASWA KUJIULIZA NANI AMBAYE ANGEZUIA MRADI HUO KIUTARATIBU, KAMA HOJA NI VIGEZO-NI SABAYA KAMA DC AU WATU WA MALIASILI?

SWALI LA 3. KWANINI NYANDA ASILICHULIE TU KWAMBA SUALA LA SWAI KUWA JIPE KAMA KUJIFICHA KWA MAANA YA KWAMBA ENEO LILE HALIKO KATIKA MAMLAKA YA SABAYA KAMA DC?

SWALI LA 4. NANI AMEMWAMBIA ALOYCE NYANDA KUWA KAMA MALI ZA SWAI ZIMEUZWA ARUSHA KWA MNADA NA CRDB BASI ANAKOSA HAKI YA KULALAMIKA DHIDI YA SABABYA KAMA ANAONA KUNA MAMBO MABAYA AMEFANYIWA? HII NDIO CRITICAL THINKING YA WATANGAZAJI WA STARTV?

SWALI LA 5. JIBU LAKE NI SAWA NA JIBU LA SWALI NAMBA 4.

* HUYU NYANDA ACHUNGUZWE, INAWEZEKANA AMEPEWA MSHIKO KUMTETEA SABAYA!
Huyo Nyanda usikute ni bebi wake huyu jambazi Sabaya, siyo kwa kujitoa ufahamu kiasi hiki.
 
Back
Top Bottom