kiboboso
JF-Expert Member
- Sep 17, 2013
- 9,323
- 12,594
Madataka ni nini na wewe?Sijui sheria inasemaje akienguliwa anaweza shitakiwa binafsi kwa madhila aliyoyenda kwa kutumia vibaya madataka?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Madataka ni nini na wewe?Sijui sheria inasemaje akienguliwa anaweza shitakiwa binafsi kwa madhila aliyoyenda kwa kutumia vibaya madataka?
Pointless....Kwa siku za hivi karibuni kumeibuka video mbalimbali zikiwemo za baadhi ya viongozi wakifanya matendo yakinyama kwa Raia . Kwa Taifa changa kama letu na kwa mitandao ilivyozagaa video hizi zinaangukia mikononi mwa watoto. Wanapoona namna wazazi wao wanavyonyanyaswa, wanavyoona namna viongozi wanavyotawala, wanavyoona hakuna mzee au Kiongozi katika ngazi ya Taifa anayechukua hatua wanajenga chuki na nchi yao.
Hii siyo njia sahihi yakulea Taifa, hii siyo njia sahihi yakuongoza Taifa, hii siyo njia sahihi yakukuza viongozi, haya ni matendo yakinyama na yanayonajisi Taifa letu.
Kwa picha na video hizi za akina Sabaya timu yake, kwa aina hii ya dharau baina ya wateule wa Rais ni wazi tumefika wakati wa baadhi yetu kuwa slave na wengine kuendelea kuwa slave master.
Ni mtizamo wangu Kama mzazi, mnaosambaza hizi video mwache msiendelee kupandikiza chuki kwa watu. Watawala tulionao wameshaona namna wanavyotawala na wameridhika na aina hii ya kututawala. Please tuvumilie haya machungu bila kuwarithisha watoto wetu, wazazi msiwashirikishe watoto dhambi hii mtawaaribu kifikra na kisaikologia.
Niombe msizisambaze hazina afya kwa ustawi wa nchi yetu, zinatweza Utanzania wetu, zinadhalilisha uchumi wetu na zinafukuza wawekezaji na majirani wema, zinatutenga na Dunia, zinaifanya Tanzania ionekane nchi yenye viongozi katili Duniani na wasioguswa.
Kuna tofauti gani kati yake na wewe? Nyie wote ni watetezi wa watu waovu. Ulikuwa mtetezi wa JIWE. SABAYA ni zao la JIWE. Kilangila.Aloyce Nyanda tangu ajiingize kwenye Tamthilia amekuwa bure kabisa!
Kumbe machozi yake kwa msiba wa JIWE yalikuwa na sababu nyingi! Kilangila.Mama Mama SSH pitia uzi huuu na ikikupendeza huyu jambazi umpumzishe anapostahili huku kesi zikifunguliwa juu yake.
Pole sana Mrs. Sabaya. Picha na video zote hizi huzioni? Kilangila.Bila ushahidi hii sio habari !
Duu huyu ni Jambazi zaidi ya JiweHivi Sabaya ana chafuliwa au Sabaya ni mchafu?? /kuna gani la uongo Swai kasema kuhusu Sabaya?
Kama Sabays kakutuma umekosea kuandika hapa. Huu ujumbe unge mpelekea mkewe kama anae. Sisi tunao mjua Sabaya hatuhitaji kuelezwa kwa ana chafuliwa. Maana Sabaya si mchafu tuu bali ni jambazi na muuaji.
VIDEO YA CCTV CAMERA IKIMUONYESHA MKUU WA WILAYA YA HAI AKITESA MTU NA WATU WAKE.
Diwani Msangi wa Sombetini afunguka juu ya kipigo alichopewa na Sabaya
Philip Kana
4th April 2021
DIWANI wa Kata ya Sombetini, Jiji la Arusha, Bakari Msangi, amefunguka namna alivyoshambuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya akiwa na walinzi binafsi.
Anadai kwamba Sabaya wakati akimshamblia, alikuwa na walinzi wake binafsi sita waliobeba silaha ikiwamo bastola mbili.
Diwani huyo ameiambia SAUTI KUBWA kwamba ameamua kuyasema hayo baada ya Sabaya na wapambe wake kusambaza taarifa kuwa Februari 9, mwaka huu, alipigwa na baaadhi ya watu baada ya kumfumania “akiwa na mke wa mtu.”
Msangi akielezea namna tukio hilo lilivyokuwa anasema, Februari 9, mwaka huu majira ya saa 11 jioni alipokea simu kutoka kwa Mohamed Asaad, akimweleza kuwa mkuu huyo wa wilaya amevamia dukani kwake, hivyo kama anafahamiana naye anaomba akamsikilize na kumsaidia. Assad ni mmiliki wa duka la mapazia la Shaahidi Storea lililopo Barabara ya Nyamwezi karibu na Soko Kuu jijini Arusha.
Msangi anasema: “Mimi nikaenda pale dukani nikakuta mlango wa chuma umefungwa nikagonga hawakufungua, nikaamua kuuvuta juu nikaingia. Kweli nikamkuta Sabaya na vijana wake sita wamewaweka chini ya ulinzi wafanyakazi na wateja waliokuwa kwenye hilo duka, wanawapiga,” anasema Msangi na kuongeza.
“Nikamuuliza Sabaya kuna shida gani? Akaniambia hawa Waarabu ni wahujumu uchumi, wanafanya biashara haramu wanauza dola feki, wanauza bidhaa hawatoi risiti, akaniorodhesha makosa kibao…
“Nikamwambia mimi kama diwani wajibu wangu ni kuwatetea wananchi wa Arusha, lakini wewe hapo ulipo siyo TRA, (Mamlaka ya Mapato Tanzania), siyo Takukuru wala Usalama wa Taifam na siyo polisi, iweje uwanyanyase hawa badala ya kutumia vyombo husika vikaja kuwakamata hawa watu?”
Msangi anasema kuwa kauli hiyo ilionekana kumuudhi Sabaya ambaye bila simile alimgeukia na kuanza kumshushia kipigo.
“Aliwaamuru vijana wake waninyang’anye simu zangu, wakachukua na fedha walizonikuta nazo kama laki tatu na elfu tisini, wakanipiga vibao wakanikalisha chini,” anasema Msangi na kuongeza.
“Walipokuwa wananikalisha, niligoma, wakaamua kunifunga pingu mikononi. Wakaanza kunipiga, nikamwambia Sabaya haki ya Mungu mtaniua, lakini sitaondoka hapa mpaka nisimamie haki ya hawa watu.
“Wakati haya yakiendelea, Sabaya alimchukua mdogo wa mwenye duka na kuingia naye chumba kingine ambako walikuwa wakizungumza. Baadaye nikagundua kuwa alikuwa akimuamuru ampigie simu kaka yake, Asaad ili aje dukani kwake…”
Diwani huyo anasema kuwa iIlipofika saa tatu usiku alimwambia Sabaya awaache, lakini aligoma na baadaye kuwapiga vibao wateja waliokuwamo ndani ya duka na wadogo wa Asaad, kisha aliwaambia waondoke.
“Sabaya akapiga simu kwa OC CID akamwambia kuna watu nimewakamata ni wahujumu uchumi nataka kuwaleta hapo polisi. Wale ndugu zake Assad wawili wakaingizwa kwenye gari la walinzi aliokuwa nao – mabaunsa, mimi nikaingizwa kwenye gari alilokuwa amepanda Sabaya…
(Sabaya)
“Msafara ukaanza kuelekea Central, tulipofika tukamkuta OC CID, Gwakisa kasimama nje anatusubiri na mimi nikataka kushuka, lakini Sabaya akanizuia.”
Diwani Msangi anasema Sabaya alimwambia hajamshusha polisi kwa sababu hajamaliza kazi naye, anataka akamuonyeshe nyumbani kwa Ally Assad Ajirin na kwa kaka yake Mohamed Assad Ajirin. Anazidi kusimulia:
“Tukaenda kwa Ally Assad Ajirin, tukafika tukagonga mlango hawakufungua. Kidogo wakati tunatoka, tukakutana na mzee mmoja anaongea na simu akajua labda ni mzee wa familia hiyo akamkamata baadaye akamuacha” anasema Msangi na kuongeza.
“Tukaondoka tukaenda kwa Mohamed Assad tulipofika akavunja mlango akaingia ndani akawaluta mke wa Mohamed na watoto. Hawakumkuta Mohamed, hivyo tukaondoka.
“Tukatoka tukazunguka mjini mimi nikiwa nimefungwa pingu. Baadaye wakaenda supermarket ya Panone pale Ngarenaro wakanunua vinywaji wakawa wanakunywa, kisha tukaondoka mpaka pale Hoteli ya Tulia, iko pale WhiteRose,”.
“Tulipofika hapo wakaingia ndani wakaniacha mimi kwenye gari wakawa kama wamenisahau. Palepale nikaona mfuko waliokuwa wameweka simu, nikavivuta nikafanikiwa kuchukua simu.
“Simu kubwa nikaiicha ndani ya chupi nyingine ndogo nikaitumia kumpigia mke wangu. Nikamwambia yote yaliyonikuta, nikamwambia anifuate ila aje na jirani yetu hapo nyumbani.
“Baadaye kidogo, Sabaya akatoka akiwa kabadili nguo, mwanzo alikuwa kavaa kaunda suti sasa ametoka kavaa koti, akaja kwenye gari akaniambia nasikia kuwa watu wanakutafuta ni nani, nikamwambia sijui…
“Sabaya akasema itakuwa ana simu huyu embu mpigeni ‘teru’ (mkagueni). Walinikagua, lakini walishindwa kuziona kwa sababu zilikuwa ndani ya suruali.
“Sabaya alimuona mke wangu eneo lile, jirani na gari lake, akahoji akisema ‘huyu malaya anayekufuatilia ni nani?’
“Akawa anawaagiza mabaunsa wake waende wakamchukue, nikawaambia mtamchukuaje mke wangu, baadaye nikaamuriwa kwenda kuzungumza naye nikiwa chini ya ulinzi…
“Sabaya akaja akamtolea mke wangu bastola akamwambia leo naenda kumuua Bakari. Mke wangu akapiga ukunga, Sabaya akaona kuna shida, lakini mimi nikamwambia mke wangu asiwe na wasiwasi kwani hapo walipofika hawezi kufanya chochote nikamwambia akanisubiri Arusha Technical …
“Mabaunsa wakaniingiza kwenye gari tukaondoka tulipofika pale Petrol Station ya Mount Meru, kabla ya taa za barabarani, wakasimamisha gari wakaniambia nishuke nikimbie. Nikagoma, wao wako na bunduki na bastola nakimbia vipi? Wangeweza kunipiga risasi nikawaambia wanipeleke mahali mke wangu yupo…
“Wakaenda wakanishusha pale Arusha Technical ambapo mke wangu alikuwa wakanipiga mkwara. Nikaondoka kufika nyumbani ndiyo nikaanza kusikia maumivu, nikawapigia viongozi wenzangu sikuwapata ….
“Nikaamua kumpigia simu Mkuu wa Mkoa, Iddi Kimanta nikamweleza kila kitu, yule mzee alilia kabisa wakati naongea naye. Akawapigia RPC na OCD akawaeleza kisha akaniambia tukutane Polisi, nilipofika nikawakuta viongozi wamejaa …
“Ilikuwa saa sita usiku, wakaniandikia PF3 nikaenda hospitali kutibiwa, hivi napokwambia naendelea na matibabu na polisi wako kwenye uchunguzi.”
Diwani huyo alisema kuwa hakuweza kutambua namba za gari alilokuwa akitumia Sabaya kwani wakati wakitoka dukani kwa Assad alikuwa ameweka namna za DFP na walipokuwa wakitoka hoteli ya tulia alikuwa amebandika namna za UN.
Kamanda wa Takukuru mkoani Arusha, James Ruge alisema endapo tukio hilo lilitokea, halina uhusiano na taasisi anayoiongoza, na kubainisha kuwa “hiyo ni jinai.”
Sabaya hakujibu simu za mwandishi wetu wala ujumbe mfupi wa simu uliomtaka azungumzir sakata hili na tuhuma hizi.
Arusha ndio ilikua sehemu yake kuu ya kufanya ujambazi na kikosi chake hata cctv za bank zitaonyesha wakiwa wawazi si walikua wanaenda na mteja bank kuchukua rushwa huyo jambazi mkubwa kabisa huyo...Zipo CCTV nyingine Sabaya anavamia duka la nguo Arusha na inaonekana walivyojichotea pesa. Huyu hafai kwa serikali ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan.
Ujinga mtupu.Kwa siku za hivi karibuni kumeibuka video mbalimbali zikiwemo za baadhi ya viongozi wakifanya matendo yakinyama kwa Raia . Kwa Taifa changa kama letu na kwa mitandao ilivyozagaa video hizi zinaangukia mikononi mwa watoto. Wanapoona namna wazazi wao wanavyonyanyaswa, wanavyoona namna viongozi wanavyotawala, wanavyoona hakuna mzee au Kiongozi katika ngazi ya Taifa anayechukua hatua wanajenga chuki na nchi yao.
Hii siyo njia sahihi yakulea Taifa, hii siyo njia sahihi yakuongoza Taifa, hii siyo njia sahihi yakukuza viongozi, haya ni matendo yakinyama na yanayonajisi Taifa letu.
Kwa picha na video hizi za akina Sabaya timu yake, kwa aina hii ya dharau baina ya wateule wa Rais ni wazi tumefika wakati wa baadhi yetu kuwa slave na wengine kuendelea kuwa slave master.
Ni mtizamo wangu Kama mzazi, mnaosambaza hizi video mwache msiendelee kupandikiza chuki kwa watu. Watawala tulionao wameshaona namna wanavyotawala na wameridhika na aina hii ya kututawala. Please tuvumilie haya machungu bila kuwarithisha watoto wetu, wazazi msiwashirikishe watoto dhambi hii mtawaaribu kifikra na kisaikologia.
Niombe msizisambaze hazina afya kwa ustawi wa nchi yetu, zinatweza Utanzania wetu, zinadhalilisha uchumi wetu na zinafukuza wawekezaji na majirani wema, zinatutenga na Dunia, zinaifanya Tanzania ionekane nchi yenye viongozi katili Duniani na wasioguswa.
Sabaya mwisho wake umefika alikuwa hovyo mno!Anaandika Mtozi Alloyce Nyanda
Nimeona Video ya Mfanyabiasha Cathbert imepostiwa na @kumbushodawson
Kumbuso ni rafiki yangu sana na kwa kuwa sisi sote huwa ni waumini wa ujenzi wa hoja basi kabla ya kuingia katika mjadala wa msingi napenda maswali haya yajibiwe kisha tuje sasa kwenye Hoja hiyo hapo juu.
1. Huyu Bwana Cathbert mwaka 2019 aliwahi kusema kuwa Mkuu wa wilaya Sabaya aliwahi kuvamia hotelini kwake na makundi ya watu na kupora hela na kulazimisha kuchukua mwanamke kwa nguvu na kwamba Bwana Cathebert alisema atatoa Video ya CCTV ikionyesha huo unyama wa Sabaya lakini tangu mwaka 2019 hadi leo ni miaka 2 hakuna hiyo Video; je Video ipo wapi?
2. Anadai Sabaya alimzuia mwekezaji wa maonyesho ya nyoka kufanya hivyo Hai! unajua nyoka ni maliasili na nyara muhimu za serikali? umewahi kumuuliza kama alikidhi vigezo na taratibu za kisheria kumruhusu kufanya hivyo?
3. Huyu bwana katika Video hapo
Juu anasema amekimbia na kujificha kutokana na vitisho vya Sabaya na anamuomba mama Samia amsaidie! Swali mtu anasema amejificha wakati anasema yupo pahala flani kwenye shamba tena mchana kweupe na yupo Tanzania je Kumbuso kujificha ndo huku ambapo Mimi na wewe hatupo Kilimanajaro ila tumeshajua huyu bwana yupo wapi!
4. Asante Tours Ooshi si Arusha na kwamba kuna video ikionyesha kwamba mwezi wa pili mwaka huu kampuni na ofisi iliuzwa kwa mnada na bank ya CRDB mil 600 kutokana na madeni ya bwana huyu anayodaiwa toka mwaka 2009 huko nako Sabaya alikuwa Hai?
6. Zimekuwepo tuhuma za huyu bwana kupora maeneo na kuyabadilisha hati kisha anaenda kukopa bank na kuyatumia kwa
Manufaa yake na DC alishwahi kuyarudisha mashamba kwa wenyewe, je Kumbuso unafahamu Hilo? Je, alishawahi hata kujirekodi kusema kuwa ni uwongo?
Baada ya uteuzi wa mawaziri,makatibu wakuu mhe Rais alisema sasa anakuja kwa ma Rc na kina sabaya,Haya nayo yakazuka,common sense inasemaje?
Naomba Tuanze na haya kisha twende kwenye hoja ya Msingi ya bwana Mfanyabiashara ambae yupo shambani alipojirekodi kutupa habari amejificha.
Acha fiksi mkuu mbona hatujawahi kusikia mtu kala bullet pande hizo ukiachana na lile la mwamwindi la miaka ya 70Ujinga mtupu.
They are lucky to be alive.
Hao viongozi wakafanye hiyo upuuzi sehemu kama Mbeya au Iringa, nakuhakikishia mtu anakula bullet na anajisalimisha polisi.
Mwamwindi legacy.
Hao watu wafundishwe uongozi, kuna red line hata nani hawezi cross.
Mbona wewe ni mtetezi wa Halima Mdee na Esther Bulaya!Kuna tofauti gani kati yake na wewe? Nyie wote ni watetezi wa watu waovu. Ulikuwa mtetezi wa JIWE. SABAYA ni zao la JIWE. Kilangila.
Mwulize RC Chalamila, aliingia kwa fixi, wazee walimpa dokezo, kapoa.Acha fiksi mkuu mbona hatujawahi kusikia mtu kala bullet pande hizo ukiachana na lile la mwamwindi la miaka ya 70
Swai ni ukoo bora utumie majina yake yote. AsanteAnaandika Mtozi Alloyce Nyanda
Nimeona Video ya Mfanyabiasha Cathbert imepostiwa na @kumbushodawson
Kumbuso ni rafiki yangu sana na kwa kuwa sisi sote huwa ni waumini wa ujenzi wa hoja basi kabla ya kuingia katika mjadala wa msingi napenda maswali haya yajibiwe kisha tuje sasa kwenye Hoja hiyo hapo juu.
1. Huyu Bwana Cathbert mwaka 2019 aliwahi kusema kuwa Mkuu wa wilaya Sabaya aliwahi kuvamia hotelini kwake na makundi ya watu na kupora hela na kulazimisha kuchukua mwanamke kwa nguvu na kwamba Bwana Cathebert alisema atatoa Video ya CCTV ikionyesha huo unyama wa Sabaya lakini tangu mwaka 2019 hadi leo ni miaka 2 hakuna hiyo Video; je Video ipo wapi?
2. Anadai Sabaya alimzuia mwekezaji wa maonyesho ya nyoka kufanya hivyo Hai! unajua nyoka ni maliasili na nyara muhimu za serikali? umewahi kumuuliza kama alikidhi vigezo na taratibu za kisheria kumruhusu kufanya hivyo?
3. Huyu bwana katika Video hapo
Juu anasema amekimbia na kujificha kutokana na vitisho vya Sabaya na anamuomba mama Samia amsaidie! Swali mtu anasema amejificha wakati anasema yupo pahala flani kwenye shamba tena mchana kweupe na yupo Tanzania je Kumbuso kujificha ndo huku ambapo Mimi na wewe hatupo Kilimanajaro ila tumeshajua huyu bwana yupo wapi!
4. Asante Tours Ooshi si Arusha na kwamba kuna video ikionyesha kwamba mwezi wa pili mwaka huu kampuni na ofisi iliuzwa kwa mnada na bank ya CRDB mil 600 kutokana na madeni ya bwana huyu anayodaiwa toka mwaka 2009 huko nako Sabaya alikuwa Hai?
6. Zimekuwepo tuhuma za huyu bwana kupora maeneo na kuyabadilisha hati kisha anaenda kukopa bank na kuyatumia kwa
Manufaa yake na DC alishwahi kuyarudisha mashamba kwa wenyewe, je Kumbuso unafahamu Hilo? Je, alishawahi hata kujirekodi kusema kuwa ni uwongo?
Baada ya uteuzi wa mawaziri,makatibu wakuu mhe Rais alisema sasa anakuja kwa ma Rc na kina sabaya,Haya nayo yakazuka,common sense inasemaje?
Naomba Tuanze na haya kisha twende kwenye hoja ya Msingi ya bwana Mfanyabiashara ambae yupo shambani alipojirekodi kutupa habari amejificha.
Dokezo la nini?Mwulize RC Chalamila, aliingia kwa fixi, wazee walimpa dokezo, kapoa.
SABAYA UMEHARIBU SANA, HATA HIZI ACCOUNT UNAZOTUMIA KUJISAFISHA NI ZAKO SABAYA ZIPO HUMU KIMKAKATI, UKIZUNGUMZWA NA WATU KWA MEMA BASI MBELENI HUWA KWEMA.....ONA MAMA SAMIA-RAIS WA JMT ALIZUNGUMZWA VYEMA NA WALIMWENGU ONA LEO ALIPO, NA SIO HAPO TU ANAELEKEA AFRICA NA ULIMWENGUNI WEE MWENYEWE UTAONAAnaandika Mtozi Alloyce Nyanda
Nimeona Video ya Mfanyabiasha Cathbert imepostiwa na @kumbushodawson
Kumbuso ni rafiki yangu sana na kwa kuwa sisi sote huwa ni waumini wa ujenzi wa hoja basi kabla ya kuingia katika mjadala wa msingi napenda maswali haya yajibiwe kisha tuje sasa kwenye Hoja hiyo hapo juu.
1. Huyu Bwana Cathbert mwaka 2019 aliwahi kusema kuwa Mkuu wa wilaya Sabaya aliwahi kuvamia hotelini kwake na makundi ya watu na kupora hela na kulazimisha kuchukua mwanamke kwa nguvu na kwamba Bwana Cathebert alisema atatoa Video ya CCTV ikionyesha huo unyama wa Sabaya lakini tangu mwaka 2019 hadi leo ni miaka 2 hakuna hiyo Video; je Video ipo wapi?
2. Anadai Sabaya alimzuia mwekezaji wa maonyesho ya nyoka kufanya hivyo Hai! unajua nyoka ni maliasili na nyara muhimu za serikali? umewahi kumuuliza kama alikidhi vigezo na taratibu za kisheria kumruhusu kufanya hivyo?
3. Huyu bwana katika Video hapo
Juu anasema amekimbia na kujificha kutokana na vitisho vya Sabaya na anamuomba mama Samia amsaidie! Swali mtu anasema amejificha wakati anasema yupo pahala flani kwenye shamba tena mchana kweupe na yupo Tanzania je Kumbuso kujificha ndo huku ambapo Mimi na wewe hatupo Kilimanajaro ila tumeshajua huyu bwana yupo wapi!
4. Asante Tours Ooshi si Arusha na kwamba kuna video ikionyesha kwamba mwezi wa pili mwaka huu kampuni na ofisi iliuzwa kwa mnada na bank ya CRDB mil 600 kutokana na madeni ya bwana huyu anayodaiwa toka mwaka 2009 huko nako Sabaya alikuwa Hai?
6. Zimekuwepo tuhuma za huyu bwana kupora maeneo na kuyabadilisha hati kisha anaenda kukopa bank na kuyatumia kwa
Manufaa yake na DC alishwahi kuyarudisha mashamba kwa wenyewe, je Kumbuso unafahamu Hilo? Je, alishawahi hata kujirekodi kusema kuwa ni uwongo?
Baada ya uteuzi wa mawaziri,makatibu wakuu mhe Rais alisema sasa anakuja kwa ma Rc na kina sabaya,Haya nayo yakazuka,common sense inasemaje?
Naomba Tuanze na haya kisha twende kwenye hoja ya Msingi ya bwana Mfanyabiashara ambae yupo shambani alipojirekodi kutupa habari amejificha.
Tuma na ya kutolea tuweke bundle tukutumie