Kwa siku za hivi karibuni kumeibuka video mbalimbali zikiwemo za baadhi ya viongozi wakifanya matendo yakinyama kwa Raia . Kwa Taifa changa kama letu na kwa mitandao ilivyozagaa video hizi zinaangukia mikononi mwa watoto. Wanapoona namna wazazi wao wanavyonyanyaswa, wanavyoona namna viongozi wanavyotawala, wanavyoona hakuna mzee au Kiongozi katika ngazi ya Taifa anayechukua hatua wanajenga chuki na nchi yao.
Hii siyo njia sahihi yakulea Taifa, hii siyo njia sahihi yakuongoza Taifa, hii siyo njia sahihi yakukuza viongozi, haya ni matendo yakinyama na yanayonajisi Taifa letu.
Kwa picha na video hizi za akina Sabaya timu yake, kwa aina hii ya dharau baina ya wateule wa Rais ni wazi tumefika wakati wa baadhi yetu kuwa slave na wengine kuendelea kuwa slave master.
Ni mtizamo wangu Kama mzazi, mnaosambaza hizi video mwache msiendelee kupandikiza chuki kwa watu. Watawala tulionao wameshaona namna wanavyotawala na wameridhika na aina hii ya kututawala. Please tuvumilie haya machungu bila kuwarithisha watoto wetu, wazazi msiwashirikishe watoto dhambi hii mtawaaribu kifikra na kisaikologia.
Niombe msizisambaze hazina afya kwa ustawi wa nchi yetu, zinatweza Utanzania wetu, zinadhalilisha uchumi wetu na zinafukuza wawekezaji na majirani wema, zinatutenga na Dunia, zinaifanya Tanzania ionekane nchi yenye viongozi katili Duniani na wasioguswa.