Mtozi Aloyce Nyanda nini kilitokea jana kipindi cha Agenda 2020?

kindikwili

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Posts
1,862
Reaction score
2,875
Ndugu zangu habari za asubuhi!

Kama kawaida siku ya jana rafiki na ndugu yetu Alloyce Nyanda alijitokeza kwenye kipindi chake tajwa hapo juu na aliwaalika vijana wawili ndg John Pambalu (mwalimu, kamanda na kiongozi wa BAVICHA Taifa) huyu walikuwa naye Ilemela Mwanza studioni. Mwingine alikuwa kada wa chama cha mapinduzi ndugu Magoiga kama sijakosea yeye akiwa dodoma. Mada ilikuwa UTENDAJI KAZI WA BUNGE LA 11.

Baada ya kuwakaribisha wageni alimtaka ndg Pambalu kuipongeza CCM kwa kufanya makubwa hasa katika ujenzi wa miundombinu ya kimkakati mfano ununuzi wa ndege. Ndugu Pambalu akamuomba wajielekeze kwenye mada iliyowaleta lakini hata hivyo akasema ununuzi wa ndege ulikuwa na manufaa kwa watanzania kama 5% tu ambao ndiyo wana uwezo wa kuzipanda huku karibia 95% wakiwa hawana uwezo wala ndoto ya kuja kupanda ndege hizo. Akasema hizo ndege tangu zimenunuliwa hazijawahi hata kuchangia pato la taifa hata kwa 0.01% wala hakuna data rasmi kwamba watalii waliongezeka kwasababu ya ununuzi wa ndege hizo. Akasema hizo hele zingeelekezwa kuboresha kilimo karibia 65% ya watanzania wangefaidi moja kwa moja na uhakika wa kuongeza pata la taifa na ajira ungekuwa wa uhakika na hivyo maisha ya watu yangeboreka zaidi.

Pambalu akasema ni taabu sana kumpongeza baba aliyejenga gorofa na kuweka samani za kifahari huku watoto wakiwa na nyongea, unyafuzi na mama yao ni choka mbaya. Akitaja sekta ya kilimo kuhemea mashine, wafanyakazi wa umma wakiwa hohe hahe miaka 5 bila nyongeza ya mishahara, wafanyabiashara na wajasirimali wakiwa hoi bin tabaan.k. Akaendelea kusema JPM akiwa anachukua nchi uchumi ulikuwa unakuwa kwa 7% kwa mwaka na ndani ya mika yake 5 uchumi bado uko na ukuaji wa 7% na huenda ukapungu. Hakuishia hapo akaendelea kusema ndege hizo zinazosifiwa zilinunuliwa bila hata bajeti kupitishwa na bunge.

Mtozi Nyanda alitaka kijana wa CCM ajibu mapigo lakini mitambo haikuwa vizuri basi ikabidi aweke tangazo kisha arudi kwa Pambalu. Hapo sasa wakajikita kwenye mada juu ya ufanisi wa bunge la 11. Ndugu Pambalu alikataa katakata kuita bunge hili bunge la 11 na kuamua kuliita bunge la Ndugai na kwamba bunge hili lilikuwa ni bunge kibogoyo (nyanda akamwambia hilo neno siyo la kistaarabu) , akasema basi ni bunge la hovyo na dhaifu kuliko mabunge yote tangu uhuru wa nchi hii. Mtozi Nyanda akasema hili bunge ndilo limepitisha bajeti zilizoleta maajabu ya miundombinu nchini kwanini uliite legelege?. Pambalu akafafanua kazi za bunge kwa mujibu wa katiba na kutoa hoja zake kwanini ni bunge la hovyo kuliko mabunge yote.

Hoja ya kwanza ni kwamba badala ya bunge kulisimamia serikali kama katiba inavyotanabaisha kwenye bunge la ndugai serikali ndiyo ilikuwa inaisimamia na kuliongoza bunge nini cha kufanya. Mfano ukatolewa kwamba Mheshimiwa sana Rais wa JMT alimuagiza spika kuwashughulikiwa wabunge wa upinzani bungeni kisha yeye atawashughulikia nje ya bunge. Kwa mujibu wa Pambalu maelekezo hayo yalilitekelezwa na spika kwa ari na nguvu mpya. Akasema baada ya agizo hilo akina Halima mdee, Ester Bulaya, Godbless Lema na wapinzani wengine wa cdm walishughulikiwa kisawasawa.

Hoja ya pili ni kwamba badala ya bunge kupanga mipango ya serikali kazi hiyo ilichukuliwa na serikali na kupelekea ununuzi wa ndege na ujenzi wa kiwanja cha ndege ambao si tu kwamba haukujadiliwa na kupitishwa na bunge lakini hata pesa zake hazikutengwa na bunge kwa mijibu wa katiba. Hapo nyanda akamtaka pambalu aelezee sheria ya matumizi ya pesa (financial act) na kama inakataza reallocation of fund pambalu japo hakusema sheria lakini akajitetea kwamba hakuna sheria inayoweza kwenda kinyume na katiba na kwamba hata kama ikiwepo bado katiba itatamalaki akimaanisha hakuna sheria inaweza kutungwa kuipoka bunge kazi yake ya kupanga na kuridhia matumizi ya pesa za umma.

Nyanda aliporudi dodoma kwa mwana ccm mawasiliano hayakuwa mazuri na kuomba waende kwenye matangazo warudi , baada ya matangazo nikapigwa na butwaa kuona kipindi cha BBC. Nikasubiri kwamba watarejea hola akatoweka bila hata kutuomba radhi sisi watazamaji wake. NDIPO SASA NASEMA MTOZI NYANDA NINI KILITOKEA NDUGU YETU MBONA ULITUACHA BILA HATA KUTUAGA AU ULIPOKEA AMRI KUTOKA JUU? AU HOJA 5 ZA PAMBALU JUU YA UDHAIFU (kwa majibu wake) wa bunge la ndugai zilikutisha ukaamua yanini malumbano ukajiweka pembeni? Jitokeze utuombe radhi kwa kilichotokea lakini pia utupe sababu .

NB: Sababu za mtu wa dodoma kutokusikika haikuwa sababu maana nakumbuka kuna siku umewahi kuendesha kipindi na mtu wa chadema mpaka kikaisha kwasababu mawasiliano wa mtu wa ccm aliyekuwa dodoma hayakuwa mazuri. Naomba pambano lirudiwe na wawili hawa waalikwe tena maana jana sisi wana ccm hatukusikika kabisa na tuna mengi ya kujivunia awamu hii. Uliwapa watu wa cdm ushindi wa mezani au ulituona hatuna uwezo wa kujibu hoja ukaamua ututolee aibu kwa kuweka mpira kwapani?

Kindikwili.
 
StarTv na vipindi vyake sijawahi kuiamini, na haitatokea kamwe niwaamini.

Mpaka watakapobadilisha mmiliki, kuwa na mmiliki mwenyekiti wa CCM Mkoa StarTv inakuwa zaidi ya TBC.
 
Mkuu mimi nataka nyanda aje atuambie nini kilitokea jana maana kutuacha solemba vile ni utovu wa nidhamu
 
Jamaa aliona mataga wanachezea za chembe ikabidi awasitiri kwa kuua kipindi gafla 🤣🤣🤣
 
Mtozi nyanda

Kipindi hakina wadhamini nikawaida kukihairisha au kukifuta
Tusimlaumu
 
Hicho ndio kilitokea jana star TV, kipindi cha ajenda 2020.
 
Kiashiria Cha dictatorship na unfair treatment kwenye siasa za Tanzania
 
Natamani kusema kitu ila kwasababu no Uhuru. Ngoja niache.
 
StarTv na vipindi vyake sijawahi kuiamini, na haitatokea kamwe niwaamini.

Mpaka watakapobadilisha mmiliki, kuwa na mmiliki mwenyekiti wa CCM Mkoa StarTv inakuwa zaidi ya TBC.
Mbona vipindi vya Voice of America huwa wanaviacha au kwa kuwa vinatumia kimalkia hivyo wanajua audience itakuwa ndogo
 
Ndugu zangu habari za asubuhi!

Kama kawaida siku ya jana rafiki na ndugu yetu Alloyce Nyanda alijitokeza kwenye kipindi chake tajwa hapo juu na aliwaalika vijana wawili ndg John Pambalu (mwalimu, kamanda na kiongozi wa BAVICHA Taifa) huyu walikuwa naye Ilemela Mwanza studioni. Mwingine alikuwa kada wa chama cha mapinduzi ndugu Magoiga kama sijakosea yeye akiwa dodoma. Mada ilikuwa UTENDAJI KAZI WA BUNGE LA 11.

Baada ya kuwakaribisha wageni alimtaka ndg Pambalu kuipongeza CCM kwa kufanya makubwa hasa katika ujenzi wa miundombinu ya kimkakati mfano ununuzi wa ndege. Ndugu Pambalu akamuomba wajielekeze kwenye mada iliyowaleta lakini hata hivyo akasema ununuzi wa ndege ulikuwa na manufaa kwa watanzania kama 5% tu ambao ndiyo wana uwezo wa kuzipanda huku karibia 95% wakiwa hawana uwezo wala ndoto ya kuja kupanda ndege hizo. Akasema hizo ndege tangu zimenunuliwa hazijawahi hata kuchangia pato la taifa hata kwa 0.01% wala hakuna data rasmi kwamba watalii waliongezeka kwasababu ya ununuzi wa ndege hizo. Akasema hizo hele zingeelekezwa kuboresha kilimo karibia 65% ya watanzania wangefaidi moja kwa moja na uhakika wa kuongeza pata la taifa na ajira ungekuwa wa uhakika na hivyo maisha ya watu yangeboreka zaidi.

Pambalu akasema ni taabu sana kumpongeza baba aliyejenga gorofa na kuweka samani za kifahari huku watoto wakiwa na nyongea, unyafuzi na mama yao ni choka mbaya. Akitaja sekta ya kilimo kuhemea mashine, wafanyakazi wa umma wakiwa hohe hahe miaka 5 bila nyongeza ya mishahara, wafanyabiashara na wajasirimali wakiwa hoi bin tabaan.k. Akaendelea kusema JPM akiwa anachukua nchi uchumi ulikuwa unakuwa kwa 7% kwa mwaka na ndani ya mika yake 5 uchumi bado uko na ukuaji wa 7% na huenda ukapungu. Hakuishia hapo akaendelea kusema ndege hizo zinazosifiwa zilinunuliwa bila hata bajeti kupitishwa na bunge.

Mtozi Nyanda alitaka kijana wa CCM ajibu mapigo lakini mitambo haikuwa vizuri basi ikabidi aweke tangazo kisha arudi kwa Pambalu. Hapo sasa wakajikita kwenye mada juu ya ufanisi wa bunge la 11. Ndugu Pambalu alikataa katakata kuita bunge hili bunge la 11 na kuamua kuliita bunge la Ndugai na kwamba bunge hili lilikuwa ni bunge kibogoyo (nyanda akamwambia hilo neno siyo la kistaarabu) , akasema basi ni bunge la hovyo na dhaifu kuliko mabunge yote tangu uhuru wa nchi hii. Mtozi Nyanda akasema hili bunge ndilo limepitisha bajeti zilizoleta maajabu ya miundombinu nchini kwanini uliite legelege?. Pambalu akafafanua kazi za bunge kwa mujibu wa katiba na kutoa hoja zake kwanini ni bunge la hovyo kuliko mabunge yote.

Hoja ya kwanza ni kwamba badala ya bunge kulisimamia serikali kama katiba inavyotanabaisha kwenye bunge la ndugai serikali ndiyo ilikuwa inaisimamia na kuliongoza bunge nini cha kufanya. Mfano ukatolewa kwamba Mheshimiwa sana Rais wa JMT alimuagiza spika kuwashughulikiwa wabunge wa upinzani bungeni kisha yeye atawashughulikia nje ya bunge. Kwa mujibu wa Pambalu maelekezo hayo yalilitekelezwa na spika kwa ari na nguvu mpya. Akasema baada ya agizo hilo akina Halima mdee, Ester Bulaya, Godbless Lema na wapinzani wengine wa cdm walishughulikiwa kisawasawa.

Hoja ya pili ni kwamba badala ya bunge kupanga mipango ya serikali kazi hiyo ilichukuliwa na serikali na kupelekea ununuzi wa ndege na ujenzi wa kiwanja cha ndege ambao si tu kwamba haukujadiliwa na kupitishwa na bunge lakini hata pesa zake hazikutengwa na bunge kwa mijibu wa katiba. Hapo nyanda akamtaka pambalu aelezee sheria ya matumizi ya pesa (financial act) na kama inakataza reallocation of fund pambalu japo hakusema sheria lakini akajitetea kwamba hakuna sheria inayoweza kwenda kinyume na katiba na kwamba hata kama ikiwepo bado katiba itatamalaki akimaanisha hakuna sheria inaweza kutungwa kuipoka bunge kazi yake ya kupanga na kuridhia matumizi ya pesa za umma.

Nyanda aliporudi dodoma kwa mwana ccm mawasiliano hayakuwa mazuri na kuomba waende kwenye matangazo warudi , baada ya matangazo nikapigwa na butwaa kuona kipindi cha BBC. Nikasubiri kwamba watarejea hola akatoweka bila hata kutuomba radhi sisi watazamaji wake. NDIPO SASA NASEMA MTOZI NYANDA NINI KILITOKEA NDUGU YETU MBONA ULITUACHA BILA HATA KUTUAGA AU ULIPOKEA AMRI KUTOKA JUU? AU HOJA 5 ZA PAMBALU JUU YA UDHAIFU (kwa majibu wake) wa bunge la ndugai zilikutisha ukaamua yanini malumbano ukajiweka pembeni? Jitokeze utuombe radhi kwa kilichotokea lakini pia utupe sababu .

NB: Sababu za mtu wa dodoma kutokusikika haikuwa sababu maana nakumbuka kuna siku umewahi kuendesha kipindi na mtu wa chadema mpaka kikaisha kwasababu mawasiliano wa mtu wa ccm aliyekuwa dodoma hayakuwa mazuri. Naomba pambano lirudiwe na wawili hawa waalikwe tena maana jana sisi wana ccm hatukusikika kabisa na tuna mengi ya kujivunia awamu hii. Uliwapa watu wa cdm ushindi wa mezani au ulituona hatuna uwezo wa kujibu hoja ukaamua ututolee aibu kwa kuweka mpira kwapani?

Kindikwili.
[emoji1]
 
Back
Top Bottom