Mtu akifa anaenda wapi?

Hili bara la kijinga sana mkuuu werevu kama wewe au mimi ni wachache mno ....wakutafuta na tochi.....
Kwasasa napata picha kwanini philosophers kama kina SOCRATES na wengine walikuwa wanauwawa,...kuwa miongoni mwa watu kama hawa pia ni hatari kwa usalama sio wa akili tu, bali pia kwa uhai wako kwa ujumla....
 
Naamini nitakuwa sijui lolote kama ambavyo nilikuwa sijui kabla ya hata shahawa kutungwa
 
Ikiwa mtu ni wa milele maana yake pia alikuwepo hata kabla hajazaliwa, na pia atakuwepo hata baada ya kufa....

sasa wewe una kumbuka ulikuwa wapi kabla hujazaliwa?...
Kaa chini ufundishwe,

(Yeremia 1:5)
"Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla ya Kutoka tumboni nalikutakasa,nimekuweka kuwa Nabii wa mataifa."

Ndipo ujue maisha ya mwanadamu hayaanzi tumboni au anapozaliwa, ni way back.

Kuthibitisha Hilo, tangu Leo, ulalapo uwe unatilia Umakini ndoto unazoota.

Ukiwa katika Ulimwengu wa Roho wa NDOTO, hakuna time,

Unaweza kuona future na past Kwa pamoja,Sema tu lugha ya ndoto Huwa ya mafumbo.

Tafuta sana Maarifa, usijizungushie uzio.
 
Mkuu, maisha ya kiimani za kiroho na maisha nje ya imani za kiroho ni tofauti mno. Mmoja anatumia ubongo na mwingine anatumua hisia za imani.

Unapoishi kiroho unakuwa na mambo kama haya unayosema ila kama unaishi kwa kutumia akili ya mwanadamu huwezi kuwa na hayo mambo utaona ni ujinga.

Ukielewa hilo utajua namna ya kujadili hoja na mtu asiyeishi kiroho anayetumia akili ya kawaida ya binadamu na utaelewa kuwa kabla ya kutumia biblia kama ref basi kwanza una kazi ya kuigeuza akili ya unayemwelewesha kuamini mambo ya rohoni.

Kinyume na hapo hiyo biblia kwake ni hadithi za kutunga kwa watu wajinga.
 
kama kuna kitu sina mashaka nacho basi ni SCIENCE, maana there is a logic behind every idea, na pia inakubali kukosolewa na kupingwa kupitia TAFITI,....


shida ya hizi imani waliozishikilia ukiwapiga maswali hawawezi kujibu, hawataki kukosolewa wala kupingwa, na Wakati huo hawana uthibitisho wowote ule....
 
Wapiramu ndiyo wakina nani?
Anajaribu kuwatusi wale asiowapenda sababu hawaamini kama yeye; wao wanamuabudu Mungu tu na si kina deacon sijui beacon.....sijui. Nikiangalia maelfu ya miaka ya mahangaiko ya kuwafuta watu hao na imani yao, tena kutoka kwa watu wenye akili na uwezo, bila madankkio; natamani nimshauri achukue jembe tu akalime.
 
kama kuna kitu sina mashaka nacho basi ni SCIENCE, maana there is a logic behind every idea, na pia inakubali kukosolewa na kupingwa kupitia TAFITI,....
Upo sawa
shida ya hizi imani waliozishikilia ukiwapiga maswali hawawezi kujibu, hawataki kukosolewa wala kupingwa, na Wakati huo hawana uthibitisho wowote ule....
Shida ya watu msio na imani za kiroho ni kuwa mnataka kujadili masuala ya kiroho kwa kutumia logic ya akili ya kawaida ya binadamu. HAIWEZEKANI. Haya mambo ya kiimani na akili ya kutengeneza logic hayaendi pamoja.

Wewe ni Logic gani utatengeneza kwenye binadamu kujaza wanyama, wadudu na ndege wawili wawili kwenye meli moja ya mbao na lami?

UKITAKA KUFAHAMU MAMBO YA ROHONI, ACHANA NA LOGIC SIJUI AKILI KUBWA. KWENYE MAMBO YA KIROHO NI MIUJIZA MIUJIZA, IMANI, MAMBO YASIYOWEZEKANA KATIKA ULIMWENGU WA LOGIC YA AKILI YA BINADAMA WA KAWAIDA.
 
Haya mambo yamepitwa sana na wakati.
 
kwahiyo ili uelewe imani ni lazima uwe empty-headed?πŸ€§πŸ˜†πŸ˜…πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ sasa si wazimu huo, ubongo kazi nini tena kama sio kufikiri?....
 
Wewe ni mpuuzi tu kama walivyo wapuuzi wengine.
 
kwahiyo ili uelewe imani ni lazima uwe empty-headed?πŸ€§πŸ˜†πŸ˜…πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ sasa si wazimu huo, ubongo kazi nini tena kama sio kufikiri?....
Ndo fomula. Ili uishi kiroho lazima uamini wewe si lolote si chochote na option uliyonayo ni chaguzi kati ya nguvu mbili zenye uwezo wa kuendesha maisha yako na maisha yanaanzia rohoni ndipo yanatokea katika uhalisia wa mwili na haya maisha ya mwili ni temporary ili kujiandaa na maisha ya rohoni ambayo mfumo wake unategemeana na nguvu uliyoichagua iendeshe roho yako. Nguvu ni mbili tu, mwanga na giza, wema na ubaya, Shetani na MUNGU. Vyovyote utakavyoziita.

Au

Uishi kwa kutumia ubongo wako, utegemee sayansi, usiamini katika uwepo wa MUNGU wala shetani, kila kitu kwako kisicho na logic kiwe ni cha kufikirika na cha kukipuuza.

Binafsi naamini nguvu iliyotuumba ilitupa ubongo kwa sababu maalum. Nimeamua kuutumia ila kama jambo silielewi kabisa na ubongo umegoma kutengeneza logic silidharau na kusema halipo, ninachofanya ni kuliacha kama lilivyo kwanza.
 
Unaweza kufanua?

Kwa sababu imani ina misingi yake. Au uko kwenye kundi moja na wale wadhainio kwamba ilimradi umeamini chochote, basi kitatokea?

Imani isiwe kichaka cha kufichia ujinga wa kiroho.
Kikubwa imani!
 
kwahiyo ili uelewe imani ni lazima uwe empty-headed?πŸ€§πŸ˜†πŸ˜…πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ sasa si wazimu huo, ubongo kazi nini tena kama sio kufikiri?....
Ni logic gani iliyopo Kwa wewe kuishi hapa Duniani?


I mean kwanini unaishi?
 
Mtu asiyemwamini Mungu ama mambo ya kiimani kwa usahihi ana jina lake la kitaalam nalo ni "Mshenzi"
 
Katika kipindi cha Elisha kulikuwa na wenye ukoma wengi katika Israel ila ni Naamani pekee aliyetakaswa wakoma wengi walikufa na ukoma wao kwa hiyo imani yako ndio itakayokuponya au kukuangamiza. Haijalishi unaamini life after or not you can not change the reality of life after death.
 
Kinachokufa ni mwili roho inakuwapo bila kasha lake
 
ukifa ndio umekufa hayo mengine ni masimulizi tu..
Tumia akili walau kidogo. Kama ukifa umekufa sasa nini lengo la sisi kuishi na kuwa hai. Akili iliyo salama unakataa hili.
 
Mtoa mada kaweka maandiko hapo ili kuhalalisha hoja zake ila turudi kwenye jambo moja. Katika Biblia kuna waandishi waliandika mitazamo yao na sio Neno kutoka kwa Mungu moja kwa moja bali ni mitazamo tu. Mfano Kitabu cha Mhubiri ni hekima za Suleimani na mitazamo yake mfano kila kitu kakiita ubatili na kujilisha upepo n.k.
Sasa katika mtizamo wa maisha mara baada ya kifo kila nabii alikuwa na mtizamo wake maana Biblia au Mungu alikaa kimnya na pengine kuzungumza kwa mafumbo. Mfano kitabu cha Mwanzo anapomlaani Adamu anamwambia " wewe ni mavumbi na mavumbini utarudi " hapohapo Kaini anamuuwa nduguye Abili na anapoulizwa na Mungu yuko wapi nduguye anamjibu Mungu shit kisha Mungu anamwambia "damu ya ndugu yako inanilia kutoka ardhini swali kama watu wakifa wanapotea au kurudi mavumbini hiyo damu iliyokuwa inatoa sauti Mungu alikuwa anasema na mzimu wa Abel?.

Kumbuka mwanadamu wa asili hawezi kuyatambua mambo ya rohoni kwani yanatambulika kwa jinsi ya roho. Hivyo wewe mwanadamu wa asili kamwe usijaribu mambo ya rohoni waachie wa rohoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…