Mtu akifa anaenda wapi?

Mtu akifa anaenda wapi?

Mawili ndio hufa na kuoza ila roho ndio haifi. Ndio maana Kuna makabila huwa wanaomba mizimu.
 
Habari wakubwa,
Naomba kwa pamoja tulijibu hili swali.
Binadamu akifa anakwenda wapi?

Usisahau kuweka ushahidi
Mimi nakumbuka nikipata nafasi ya kukaa na jamaa akiyekufa alafu akafufuka alafu baada ya wiki akafa alipata kuniambia haya .

Watu Malaya _ kuzimu kwa shetani na kila siku ni fimbo tisini kwa muda wa nusu saa Ila hakuna chakula kwa hao watu kwa muda wa mwezi na hawafi ng'o

Wezi mfano mafisadi _ wao watenda mpaka mbinguni alafu huko wataulizwa na mhasibu wa mbingu kuwa walivyoiba walimwachia nani ili mbingu iweze kuja duniani na kumrithisha mtu sahihi ,baada ya hapo watapigwa fimbo Mia hamsini kila ijumaa

Stay tuned nitaendelea ngoja nifike kilabuni kwanza
 
C ungoje ufe mkuu Kwanzaa alafu ndio ujue unaendaa wp ,km tulivyosubiri miezi Tisa kuzaliwa hatukujua tunakuja wapi na kifo nacho ndio hvyo hvyo mpk ufee ndio ujuee unaenda wapii...

Kuwa na subira zamu Yako yajaa...
 
mwili ni chombo tu, lakini mtu kama mtu ni akili, na akili inabebwa kwenye ubongo

sasa ubongo ukifa, akili inatoweka, unakuwa si kitu

unakuwa kama ulivyokuwa kabla ya kuzaliwa kwako

ndo nionavyo mimi
 
unaishi kaburin hadi kiama.
siku ya mwisho Yesu anakuja unafufuka unapaa kuelekea mbinguni ukifika hukumu inatoka kama ulikua mtenda dhambi unakula nyundo unatupwa kwenye tanuru la moto forever
hahhhahha, Yesu aje kutoka wapi? unafufuka uende wapi na ili iweje?Tukifa mambo hesabu imeisha
 
Hili swali unapowauliza walio hai unakuwa unakosea sana. Labda kama humu tuna member active walio RIP watuambie walipo.
 
Kasome kisa cha tajiri na lazaro ndo utajua mtu akifa anaenda wapi! Lakini pia unaweza kuingia youtube ukasearch mtu anaitwa aston adam mbaya ameeleza vizuri maana ni muanga wa kifo! Lakini mimi pia mdogo wangu àmewahi kukakata moto kwa masaa kadhaa wakati anaandaliwa kupelekwa mochwari akarudi aliyoyasimulia ni makubwa! Sisi wanadamu akili zetu ni fupi sana! Wengi hatumjui Mungu wala uwezo wake! Ni kweli kwamba kuna kuzimu na mbinguni ukifa tu immediate unapelekwa ulipopachagua ulipokuwa unaishi hapa duniani! Kama wewe hukumpokea Yesu na kuishi maisha matakatifu sawasawa na zaburi 16:3, 1petro 1:15 jua kwamba ukifa utaenda kuzimu ya moto! Huku ukisubiri hukumu ya mwisho ya kutupwa kwenye ziwa la moto ( ufunuo 21:8)

Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

Luka 16:22

Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.

Luka 16:23

Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.

Luka 16:24

Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

Luka 16:25
Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.

Luka 16:26

Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,

Luka 16:27

kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.

Luka 16:28


Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.

Luka 16:29

Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.

Luka 16:30

Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.

Luka 16:31

Hiyo sio stori ni uhalisia lakini imefunua siri ya baada ya kifo
 
unaishi kaburin hadi kiama.
siku ya mwisho Yesu anakuja unafufuka unapaa kuelekea mbinguni ukifika hukumu inatoka kama ulikua mtenda dhambi unakula nyundo unatupwa kwenye tanuru la moto forever
Ukilewa na mamba au fusion je unaenda wapi??
 
Yesu ametufundisha somo zuri sana juu ya KIFO kwanini hamtaki kuelewa?

Alipomwambia yule muuaji msalabani, Leo hii utakuwa nami Mahali pema peponi, unaamini huko peponi hawatambuani?

Musa na Elia walipomtokea Yesu mlimani wakimtia moyo, ulidhani yalikuwa maigizo Yale?

Kwa taarifa Yako, Musa na Elia na Manabii wote wa AGANO la kale wa Mungu, wapo Mbinguni,

WATAKATIFU wote wafao katika Mungu baada ya kufufuka Yesu, wako Mbinguni. Hawakai tena Mahali pa kusubiri.

MTU ni ROHO, anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI.

Mtu Hafi, anabadili form, mwili ndio unaokufa na kuoza,

Lakini pia mwili kuoza ni suala la muda tu, Yesu baada ya kufufuka, alipaa na mwili wake baada ya kubadilishwa form.

Mtu aliumbwa kuishi milele,mtenda dhambi ukifa(ukibadili form) utateswa milele, mtakatifu ukibadili form( ukifa) unafurahia maisha milele.


Ubarikiwe.
Amen. umenena vema mtumishi. Ila kwenye hicho kipengele cha watakatifu kuwa wako mbinguni kwa sasa kiangalie upya.

kwa sasa Watakatifu wote na wote wanaolala mauti katika Kristo huwa wanakwenda peponi (paradiso). Hili ni eneo la kupumzikia na baada ya hukumu ya mwisho, watu wote walioko hapa ndipo watapelekwa mbinguni, yaani katika mbingu mpya na nchi mpya, na kukaa na Bwana milele na kupata raha naye milele.

kwa wale waliokufa wakiwa waovu, wasiomcha Mungu; kwa sasa wako kuzimu. Kuzimu ni hatua moja kabla ya jehanamu (ziwa la moto). Baada ya hukumu ya mwisho, ndipo wenye dhambi (wote ambao majina yao hayatoonekana katika Kitabu cha uzimana cha Mwanakondoo) hawa watatupwa katika ziwa hili la moto na kuteseka na shetani milele.

yapo Maandiko mengi yanayosapoti hili ninalolisema hapa, mfano: yule mwizi msalabani aliambiwa hivi na Bwana YESU, "leo hivi utakuwa na Mimi peponi" na sio "utakuwa nami mbinguni"
 
Back
Top Bottom