Yesu ametufundisha somo zuri sana juu ya KIFO kwanini hamtaki kuelewa?
Alipomwambia yule muuaji msalabani, Leo hii utakuwa nami Mahali pema peponi, unaamini huko peponi hawatambuani?
Musa na Elia walipomtokea Yesu mlimani wakimtia moyo, ulidhani yalikuwa maigizo Yale?
Kwa taarifa Yako, Musa na Elia na Manabii wote wa AGANO la kale wa Mungu, wapo Mbinguni,
WATAKATIFU wote wafao katika Mungu baada ya kufufuka Yesu, wako Mbinguni. Hawakai tena Mahali pa kusubiri.
MTU ni ROHO, anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI.
Mtu Hafi, anabadili form, mwili ndio unaokufa na kuoza,
Lakini pia mwili kuoza ni suala la muda tu, Yesu baada ya kufufuka, alipaa na mwili wake baada ya kubadilishwa form.
Mtu aliumbwa kuishi milele,mtenda dhambi ukifa(ukibadili form) utateswa milele, mtakatifu ukibadili form( ukifa) unafurahia maisha milele.
Ubarikiwe.